Mkata Mtaa
Senior Member
- Jun 10, 2016
- 136
- 141
Hii sheria ya TRA kwamba kama uliuza gari lakini aliyenunua akubadilisha umiliki kodi utadaiwa wewe kwa nini gari yenyewe isijisimamie yenyewe, kama hailipiwi kodi ikamatwe gari husika maana kila gari inajitegemea kwa usajiri wake.
gari kama iko geraji kutokana na mtu kukosa pesa ya kutengeneza au kutokuwepo vipuri vyake, kwa nini wasisubiri siku ikiingia barabarani ikamatwe.
Mwisho kuna gari zimepata ajali ambazo gari hazitengenezeki kabisa, watu wakauza kama chuma chakavu na ripoti za polisi wakatupa maana walijua mwisho wa gari umefika, mfano kuna mabasi na malori, malori mengine yamepata ajali nje ya nchi kama Congo au Zambia wakakata kama chuma chakavu watalipaje hizo faini kubwa hivyo, maana wengine wameshapoteza malori na mabasi mengi aliyopata ajali.
TRA yenyewe ilikuwa haitoi elimu vizuri kuhusu kodi za gari,
Ili kunusuru watu kwenye hili janga ni bora kuwaambia watu wote wenye gari gereji ambazo hazitengeneki na waliyokata kama chuma chakavu waripoti TRA ili zifutwe baada ya hapo ndio sheria ianza kutumika ipasavyo, la sivyo wananchi wengi wataingia kwenye matatizo makubwa maana wengine hiyo pesa hawana tena na hawakufanya kwa maksudi.
Nawasilisha.