Kodi ya mwaka

Ghost

JF-Expert Member
Apr 20, 2010
428
53
Wandugu naomba mwongozo, hii biashara ya kulipa kodi mwaka mzima au nusu ilianzaje?
Mbona kazini hatulipwi mishahara ya mwaka...
Mwenye nyumba anataka kodi ya mwaka, mwenye frame ya biashara hivyohivyo, shuleni kwa dogo kadhalika, ila wao kwa installments...
Sasa jamani itakuasje na kila mwaka kodi hizi zinapanda...
Niende kitengo gani niweze kuashitaki niweze kulipa kwa mwezi...
Msaada tafadhali...
 
Mimi nadhani bei na masharti ya kupanga nyumba vinaenda kwa kufuata mfumo wa soko - nyumba zikiwa pungufu kulinganisha na mahitaji masharti yanakuwa magumu na bei zinakuwa juu; na nyumba zitakapozidi mahitaji masharti yatalegezwa na bei zitashuka.

Kwa sasa uchache wa nyumba za kupanga unawafaidisha wenye nyumba.
 
Pmwasyoke, nakubaliana nawewe, lakini kwanini tusilipe kwa mwezi?
Naomba kuuliza kama kuna nchi nyingine inayotumia mpango huu?
 
Mimi nadhani bei na masharti ya kupanga nyumba vinaenda kwa kufuata mfumo wa soko - nyumba zikiwa pungufu kulinganisha na mahitaji masharti yanakuwa magumu na bei zinakuwa juu; na nyumba zitakapozidi mahitaji masharti yatalegezwa na bei zitashuka.Kwa sasa uchache wa nyumba za kupanga unawafaidisha wenye nyumba.
ni sawa lakini sheria ipo inayowalinda wapangaji
 
Ingawa kuna suala la sokohuria lakin sidhani kama nchi yetu inafuata hilo kwa 100%, ndo maana kuna vitu kama ewura ambavyo vinapanga bei ya mafuta.
hivyo hata kwenye hili serikali ikiamua kupanga mfumo wa ulipaji kodi inawezekana pia
 
Idadi ya vituo vya mafuta ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya nyumba za kupanga, na bado mafanikio ya EWURA ni haba - Hiyo taasisi itakayosimamia kodi za nyumba kweli itaweza?
 
Pmwasyoke, nakubaliana nawewe, lakini kwanini tusilipe kwa mwezi?
Naomba kuuliza kama kuna nchi nyingine inayotumia mpango huu?

Sielewi kuhusu nchi nyingine - lakini kama nilivyosema kwenye hoja ya msingi, hapo nyumba zitakapokuwa nying kulinganisha na mahitaji, wapangaji watabembelezwa hata kwa kukubaliwa kulipa kila mwezi, na labda hata kulipa baada ya kukaa.
 
Hio ya kulipa baada ya kukaa naona tutasubiri sana
 
Back
Top Bottom