habari zimeingia asubuhi hii zinasema super coach syllesaid mziray amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya aga khan jijini dar alikokuwa amelazwa akisumbuliwa n malaria. Habari za mipango ya mazishi zitafuata mara tu baada ya kupatikana.
coach mziray , aliyekuwa mwajiriwa wa chuo kikuuu huria kama mhadhiri, atakumbukwa kwa umahiri katika ufundishaji soka katika vilabu mbalimbali hadi timu ya taifa iliyoshinda ubingwa wa nchi za afrika mashariki. Alifundisha pia pilsner, simba, yanga, pan african na kabla ya mauti kumkuta alikuwa mwalimu wa viungo na saikolojia wa klabu ya simba.
globu ya jamii inaungana na watanzania wote kuomboleza msiba huu mzito ambao ni pigo kwa tasnia ya michezo nchini ukizingatia tuna makocha wachache waliosomea fani hiyo na kubobea.
mola aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - amin
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.