Kocha Syllersaid Mziray Hatunae tena

Status
Not open for further replies.

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
kocha maarufu nchini, syllersaid mzirai amelazwa katika hospitali ya regency jijini na hali ya ni mbaya sana kiugua maradhi ya malaria. Watanzania tumuombee kocha huyo wa zamani wa timu za simba,, yanga na taifa stars....

kocha mziray alazwa hospitali

mziray1%281%29.jpg

kocha syllersaid mziray

wakati wachezaji wa klabu ya simba wakiendelea kujifua jijini mwanza kujiandaa na mechi yao ya ligi kuu tanzania bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, yanga, kocha wao syllersaid mziray hayuko na kikosi hicho baada ya kuugua na kulazwa jijini dar es salaam.taarifa ambazo nipashe ilizithibitisha jana, zilidai kuwa mziray ‘super coach', alilazwa katika hospitali ya regeny medical centre ya upanga jijini dar na kwamba, kwa zaidi ya wiki moja sasa, amekuwa akisumbuliwa na malaria.
Ilidaiwa kuwa kocha huyo ambaye husaidiana na kocha mkuu, mzambia patrick phiri, alipatwa na ugonjwa huo kabla ya mechi yao ya ligi kuu dhidi ya toto african kwenye uwanja wa ccm kirumba jijini mwanza.
Mwandishi wa nipashe aliyekuwa na wenzake, wakiwemo deus mhagale wa gazeti la mtanzania na doto mwaibale wa jambo leo, walifika hospitali ya regency jana na kuthibitishiwa na uongozi wa hospitali hiyo kuwa kweli, mziray amelazwa hapo katika wodi ya vip iliyoko ghorofa ya pili.
"ni kweli… tunaye mgonjwa huyo," alisema dk. Ameesh mehta, mmoja wa viongozi wa hospitali hiyo.
Hata hivyo, jitihada za waandishi kumjulia hali mziray na kisha kutoa taarifa sahihi kwa mashabiki wa soka nchini, hasa wa klabu yake ya simba, ziligonga mwamba baada ya wanafamilia wa kocha huyo kuwazuia, huku wakiwajia juu na kuwabwatukia kwa maneno makali.
Miongoni mwa wanafamilia hao, wakiwemo mmoja aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa mziray na mwingine wa kike aliyedai kuwa ni binti wa kocha huyo, waliwataka waandishi kwenda kuandika watakavyo kuhusu afya ya mpendwa, lakini wasithubutu kumsogelea hospitalini hapo.
"ondokeni hapa… hatutaki kuwaona," alisema jamaa aliyejitambulisha kuwa ndiye kaka wa mziray.
Kama hiyo haitoshi, ‘binti' na ‘kaka' wa mziray waliwarushia matusi waandishi, huku wakiungwa mkono na mlinzi mmoja hospitalini hapo aliyepuuza hata ujumbe wa maandishi wa kuwaruhusu waandishi hao kutoka kwa bosi wake, mkurugenzi wa utawala, dk. Mehta.
Haikufahamika mara moja ni kwa sababu ipi hasa iliyowafanya ndugu hao kuzuia waandishi kumjulia hali mziray, kipenzi cha mashabiki wa soka nchini na mhadhiri katika chuo kikuu huria (out).
Wakati huo huo, renatha msungu anaripoti kuwa kocha phiri aliyekwenda kuhudhuria mazishi ya binamu yake nchini kwao zambia, alirejea juzi usiku na moja kwa moja akaelekea mwanza kuungana na wachezaji wake.

source: nipashe of 11 october 2010

habari zimeingia asubuhi hii zinasema super coach syllesaid mziray amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya aga khan jijini dar alikokuwa amelazwa akisumbuliwa n malaria. Habari za mipango ya mazishi zitafuata mara tu baada ya kupatikana.
 
Malaria ni ugonjwa ambao unasababishwa na uchafu uliokithiri ambao unawapa nafasi mbu kuzaliana kwa wingi. Na wa kulaumiwa hapa ni halmashauri za majiji na Serikali kuu. Pole sana Mziray.
 
Pole mzirai.
Lawama si suluhisho kama kila kitu ni lawama tutaisha. Cha muhimu tuwajibike kila familia,kaya kupambana na mbu.
ndani ya nyumba na nje ya nyumba mazingira yawe safi, then serikali ifikirie suluhisho la kudumu.
I think DDT ikitumika vyema itapunguza saan kama si kuondoa kabisa malaria.Nasikia zenj wamefanikiwa sana war against malaria.
 
ugua pole MWANANGU..ukipata nafuu kidogo usikose kwenda kupiga kura
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom