kliniki bora kwa wajawazito

Kat

New Member
Jul 8, 2009
3
0
hi nilikuwa, naomba mnipatie msaada wa wapi ninaweza kupata huduma za kliniki kwa hapa dar, kwani mie ni mjamzito na huu ni wa kwanza, na sijui ni gynecologist gani ninaweza kwenda na tayari nakaribia miezi minne.
 
Nenda Burhan Charitable hospital,unaweza ukapata huduma nzuri,kama uko Gongo la Mbogto/Tegeta nenda kwa wakatoriki pale.
 
thanks for a quick reply, am sure gharama zake ni za kawaida?
 
Kwenye gharama za juu nenda regence au TMJ wapo vizuri. Ila kwa gharama za kawaida Lugalo is the best ile ya jeshi wanawataalamu wazuri sana sema tu a bit of que.
 
asanteni kwa ushauri wenu, i will take all into consideration, kama kuna yeyote anayejua zaidi nitafurahi.
 
Kat dr kapesa yupo shurimoyo kariakoo ni mzuri sana na hana bei kubwa kumwona ni tsh 15000/ hhospitali yake inaitwa tms pia nasikia amefungu branch mbezi tangi bovu ni dr wa muhimbili.
 
Lugalo hawawezi kukupokea maana huwa wanapenda kuanza na mama akiwa na mimba ya mwezi mmoja au pale unapojua imetunga tu na ukapima ukajikuta unayo but miezi mnne sijui kama watakupokea ndugu yangu walimkatalia baada ya kuampima wakakuta ni kama yako miezi 4
 
asanteni kwa ushauri wenu, i will take all into consideration, kama kuna yeyote anayejua zaidi nitafurahi.
but mummy inategemea uko pande ipi ya Dar,ila mie nilikuwa naenda pale Muhimbili First track kwa Kamugisha yuko poa ila anapendaga kutoa maamuzikama yeye na labda sio majibu ya utrasound ila uzuri wa huduma yake ni masaa 24 hata usiku wa manane, but also kuna Dr.Mgaya yuko poa sana
 
try first track Muhimbili, Dr Kamugisha ni mzuri sana ingawa ana queue ndefu sana, ila anapatikana mda wote, he is so kind and knowledgable. Kuna wengine pia ambao ni wazuri. Last year ilikuwa sh 6,000 kila unapoenda na kujiandikisha elf 13. hizi ni rate za mwaka jana. sina uhakika kama wameongeza au la
 
Hongera mdada. Muhimbili ni nzuri kwako ukizingatia ni uzazi wako wa kwanza. Fast Track nzuri, Kamugisha mzuri ingawa kila mtu anamkimbilia, hivyo foleni. Dr Kapona pia mzuri. Faida yake kubwa ni kwamba Madakrati pale ni wengi, hata kama Dr utakayemchagua akuhudumie (kama utaenda Fast Track) hayupo, bado unapata huduma nzuri siku ya kujifungua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom