KLH News On Saturday...

We MKJJ angalia we! utapigwa vibao naona unaanza kumgusa vibaya Waziri!
 
Mkijiji,
Muulize, Magazeti yaliyo mnukuu Dr. slaa akitaja mafisadi ynatishiwa kushitakiwa, lakini yenyewe yali ripoti na kunukuu aliye ongea, kwanini yashitakiwe? je sheria inayo timika hawaoni kwamba imepitwa na wakati na je wanampango ngani wa kuirekebisha??

.. iweke vyema mkuu..
 
Naomba mwulize:

Je katika hao viongozi wa serikali anaosema wanazunguka mikoani kuelezea budget ya serikali, Mshitakiwa wa Mauaji Ditto ana cheo gani serikalini? Nani analipia hizo gharama zake? Je ni sawa kwa serikali kuongozana na wauaji kwenye mikutano yao
 
Huyu jamaa Fa*** sana hii ni mikataba yetu ya wananchi na sio ya akina karamagi na wakoloni hao
 
Hawa watu wa serikali wana kiburi sana wanafikiri ni haki yao kufanya wanavyotaka. ITS TIME OUT.
 
Jamaa hajui kuwa dunia kijiji yaani watu wa kigoma anasema hawajui masuala ya Buzwagi.....na kuzomewa sio kweli??? jamaa msanii hana anachosema......Bora Nilewe mvinyo tu
 
Yale yale ya waziri wa Saddam, mpaka mabomu yanaanguka nyuma ya sehemu anakofanyia mkutano bado akawa anasema wamefukuziwa mbali.

Huyu naye hakubali hata kwamba CCM wanazomewa.
 
Kwenye kuzomewa ananikumbusha uvamizi wa Iraq....waziri wa propaganda (habari) anaulizwa kuhusu vifaru vya Wamarekani na yeye anajibu kwa kuuliza swali..."tanks....what tanks"...Lol
 
huyu braza Khatibu naye mtu wa pwani nini, mjanja njanja sana wa maneno, ...anamtoa mwkjj kwenye mada kwa majibu ya juu juu... kaaazi kweli kweli!.
 
Mkjj, vipi tena leo, miye naona ungelikuwa umekubaliana muda ambao ungetumia kuongea naye ili kumfunga katika kipindi... kisha speed ya maongezi ungei control kidogo na kuivuta ingekuwa bora zaidi.. pia ungemwambia kuwa atabidi asikilize muziki kidogo hapo katikati. By the way sitokulaumu sana maana unaweza kuwa umeyafikiria haya yote... ila bahati ya kupata kuongea naye labda naye alitoa masharti yake... siwezi kujua.
Ahsante kwa kufanya maongezi.

SteveD.
 
Back
Top Bottom