Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,Tanzania ninchi ya amani na utulivu,lakini nia na lengo la watu hawa ni kujenga fitina baina ya wananchi na uongozi,kitu ambacho mizizi yake ikishika na kuota basi mjue kuwa mwisho wake itachanua na Tz ya jana na leo itakuwa kumbukumbu tu,nikikatisha maneno itakuwa hapatawaliki,na hakuna serikali itakayokaa madarakani ikaongoza ,mambo yatakuwa haya haya au zaidi ya haya ya kupandikiziana chuki,amani tuliyonayo itapotea kabisa na kurudi kwake itakuwa kwa mbinde,nasema watu hawa kama wana ushahidi wa uhakika kwa nini wasifungue kesi mahakamani,sababu wanayo sheria zipo,leo kupita Tanzania nzima kueneza sumu ambayo hata wao wakiachiwa madaraka basi wasifikirie kuwa sumu wanayoipanda itakuwa imekuwa diluted kwa kuwepo kwao kwenye ngazi za uongozi,huko itakuwa kujidanganya na kutudanganya,haya mambo hayafai kuzungumzwa na kukaa kama makonda wanaopiga debe safari za mabasi wataishia kupigana wenyewe kwa wenyewe wakati abiria yuko ndani ya basi.
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.
Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe.
Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.
Juzi mmepigwa shule ya bure kuwa "Amani sio sera bali ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na siasa safi" Kama unataka tukurudishe shule sawa tu.