KLH Exclusive:Mhe Anne Kilango Malecela Alonga!

Mkuu Nyangumi heshima mbele, unajua wewe ukiwa na haya maoni mazito hivi, basi sio vibaya ku-call a day, kuliko kuendelea kulishwa sour grapes!

Mkuu Kuhani,

Strong analysis, lakini kumbuka kuwa bongo au duniani sio viongozi wote wana akili perfect ya siasa kama wewe mkuu!
 
Kuhani Mkuu, Mwanakijiji,FMES,Sam,

..Mama Kilango Melecela ametukumbusha kwamba matatizo haya yalianza tangu miaka ya mwisho ya 80. Mimi nafikiri kuna uwezekano yalianza hata kabla ya hapo.

..Kitu ambacho hakutueleza kwamba tangu miaka hiyo ya 80 na 90 walikuwepo wabunge wa CCM ambao walikuwa wakipigia kelele ufisadi. Ndiyo, walikuwepo kina Oyombe Ayila, Semindu Pawa, Patrick Qorro, Mateo Qares, Juma Akukweti, Jenerali Ulimwengu, na wengine wengi. Tatizo ni kwamba hawakusikilizwa.

..Hili suala la kusema tatizo haliko CCM ni kutulaghai tu na nadharia. Chama hakiwezi kujitofautisha na viongozi wake, na matokeo ya utendaji wao. Tukiendelea kwa namna hiyo tunaweza hata kusingizia kwamba kile chama cha makaburu wa SA kilikuwa kizuri tu, waliokuwa na matatizo ni kina Pieter Botha, na viongozi wachache.

..Ufisadi umeendelea kwa vipindi vya Maraisi watatu wa CCM. sasa how can we continue to claim kwamba CCM haina matatizo, na kwamba tubadili watu wachache hapa na pale tu?

..Labda sikumuelewa tu, lakini ktk utetezi wake wa CCM inaelekea Mama Kilango Malecela anafikiri Nelson Mandela alikuwa kwenye chama tawala cha makaburu. Nadhani dunia nzima inaelewa kwamba kilichobadilika Afrika Kusini siyo sera, bali hata chama tawala kiliondoka madarakani.

..halafu hii hotuba ya Kikwete ina maana gani kama haiendani na matendo? haya mambo yote hayakufichuka kutokana na juhudi binafsi za Raisi na serikali yake. tumeona jinsi Waziri Mkuu na mawaziri, kwa maana nyingine serikali, ilivyokuwa ikijaribu kuficha ukweli. kwa msingi huo sidhani kama tunapaswa kuitilia maanani ile hotuba ya Raisi bungeni.

..ile kauli ya Raisi ya "tusije kulaumiana mbele ya safari" ndiyo kielelezo kwamba Uraisi wake una UBIA. sijapata kusikia kauli inayofanana na hiyo toka kwa Raisi yeyote yule wa Tanzania.

..ukweli ni kwamba kuna kikundi kilichofanya kazi "kubwa" mpaka Kikwete akaingia madarakani. sasa hao ndiyo anawalenga Kikwete kwamba wasije wakamlaumu mbele ya safari ikiwa atalazimika kufanya mambo "visivyo." kama Raisi hana "ubia" na mtu yeyote hizo "lawama" zitatoka kwa nani?

..Labda mbele ya safari Mama Kilango Malecela will realize kwamba tatizo ni CCM. labda ataelewa kwamba short of kukiondoa chama hicho madarakani, yanahitaji mabadiliko makubwa mno[complete overhaul] ya uongozi ndani ya CCM.
 
Kuhani mkuu,
Anasema suluhisho la matatizo yetu ni kubadilisha mfumo wa kiuchumi ambao unaruhusu wachache kumiliki mabilioni ya pesa huku walio wengi hawana kitu. Halafu hapo hapo anasema hayo mapesa yanayomilikiwa na wachache sio yao bali, ni ya Serikali. Tatizo la kutoelewa au labda kushindwa kujieleza linajitokeza hapa. Kama wachache wanamiliki pesa zisizo kuwa zao basi hilo ni tatizo la ufisadi, tatizo la wizi, na sio tatizo la mfumo wa Uchumi. Utabadilisha mfumo, na hata ukafufua Azimio la Arusha, lakini kama kujapigana na ufisadi, mfumo wako mpya labda ndio utakuongezea matatizo maana utazidi kujichanganya. Sasa hivi Watanzania tumechanganyikwa juu ya mfumo wa Siasa na Uchumi tunaofuata, kati ya Ujamaa na Kujitegemea au Ubepari unaoruhusu njia kuu za uchumi kumilikiwa na wachache. Kubadili mfumo wa Kiuchumi peke yake hakuwezi kutatua ufisadi

Mkuu hapa nitatofautiana na wewe ktk hili...sehemu hii tu kidogo inanipa shida..
Mimi namkubaliana na mama Malecela kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni mfumo wa Azimio la Zanzibar ambao unalindwa kisheria kwa watu wachache kushika utajiri wa nchi yetu. Ni mfumo wa Ubaguzi wa rangi (Apartheid) uliopigwa vita South Afrika, walishindwa kutazama matatizo yanayokuja na ubaguzi huo kiasi kwamba leo hii hakuna ubaguzi lakini uchumi wa nchi hiyo bado unashikiliwa na wachache, hivyo vita yao haikuwa uchumi haswa isipokuwa nafasi sawa kwa wananchi wote..
Sisi Tanzania swala letu kubwa ni hawa mafisadi ambao wanalindwa na mfumo mzima..Sasa sisi hatutaishia kubadilisha mfumo isipokuwa ni pamoja na kuwaondoa Utawala mzima na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake, kwa sababu Mapinduzi yoyote yale huanza pale wanapopingana na mfumo uliopo, kisha wahusika wa mfumo huo hufikishwa mahakamani kwa sababu ya sheria zao zilizowakandamiza wengine. Hata huyo Saadam alikuwa akiyafanya yote kwa mfumo unaolindwa na sheria za Udikteta alizoziunda yeye na chama chake..Baada ya kuondolewa alifikishwa mahakamani na sheria mpya iliweza kumhukumu pamoja na kwamba hata katika utetezi wake alisema wazi kuwa aliyafanya yote hayo kwa sababu ya Usalama wa Taifa lake. Ukitazama sheria zilizotangulia huwezi kumhukumu Saadam wala mtu yeyote hata Hitler angekuwa hana makosa isipokuwa unatazama sheria Mpya zinazopingana na zile zilizotangulia kuonyesha makosa..
Binafsi vita yangu ni CCM nzima na mfumo wake wote na ndio maana nasisitiza kuiondoa madarakani laa sivyo hawa kina Mama Malecela hawana nguvu kabisa ya msukumo kisheria ndani ya Utawala huu hata kama wanayaona makosa yote.
 
Mkandara,

..mama kilango malecela amezungumzia kuhusu "mfumo wa uchumi" ulioruhusu watu wachache kumiliki rasilimali za taifa. sikumsikia akizungumzia rasilimali hizo ni zipi. badala yake mama malecela akazungumzia fedha zilizokopwa toka BOT tangu miaka ya 80,90, na hivi karibuni.

..mimi nakubaliana na Kuhani Mkuu kwamba hapa tuna tatizo la WIZI, na siyo mfumo wa uchumi. matatizo haya yalianza tangu Azimio la Zanzibar halijapitishwa.

..hata wakati Ujamaa umechachamaa bado kuna wajanja walikopa NBC na THB[Tanzania Housing Bank] mpaka benki hizo zikafilisika. Viwanda vya umma vilifilisika way back kabla ya Azimio la ZNZ. Tatizo ni WIZI, sheria za kushughulikia wezi zipo, lakini hazifuatwi.
 
Msiwaone hivi hawa viongozi wa CCM ambao wako nje ya chungu! Anne Kilango kama alikuwa rafiki wa kupika na kupakua wa Sophia Simba mnatagemea kwamba naye si mmoja wao? Subirini JK ampe uwaziri muone atakavyobadilika! Hawa wenzetu wakiishaingizwa kwenye chungu kwa kupewa uwaziri wanabadilika kabisaaaa na kama ilivyo ada wanaanza kutetea yale yale waliyokuwa wakiyapinga walipokuwa nje! Tanzania itajengwa na Wazalendo wenye Moyo wa dhati!
 
Mama Kilango ninavyomfahamu ni kwamba akiingia uwaziri, basi biashara zake za miaka karibu 30 iliyopita zitaishia kuharibika tena sana, je ameshindwa kupata uwaziri? Hapana hajataka,

je inapaswa kuwa kipimo cha uongozi wetu kuwa ni lazima tujue in advance kuwa mbunge huyu au yule akipewa uwaziri atakuwa the same? Sasa hivi anamalizia Degree yake ya Uchumi pale Open University,

ninaheshimu sana critic zilizotolewa hapa kuhusiana na maneno yake kwenye interview na MMJ, kuna ambazo ni za muhimu sana kwake kupewa kwa ajili ya maendeleo yake kisiasa na kiuongozi!
 
Msiwaone hivi hawa viongozi wa CCM ambao wako nje ya chungu! Anne Kilango kama alikuwa rafiki wa kupika na kupakua wa Sophia Simba mnatagemea kwamba naye si mmoja wao? Subirini JK ampe uwaziri muone atakavyobadilika! Hawa wenzetu wakiishaingizwa kwenye chungu kwa kupewa uwaziri wanabadilika kabisaaaa na kama ilivyo ada wanaanza kutetea yale yale waliyokuwa wakiyapinga walipokuwa nje! Tanzania itajengwa na Wazalendo wenye Moyo wa dhati!

LOL! Jina lako linanifurahisha sana....ntilie na mimi basi kidogo hilo chuzi zito zito....:)

Nimeshalisema hili kwamba miaka ya nyuma wale wabunge 'wakorofi' bungeni walikuwa wanazibwa midomo kwa kupewa uwaziri na huyu mama si ajabu akaukwaa muda si mrefu ujao. Si mnajua kwamba katika sirikali ya muungwana kunakuwa na mabadiliko ya baraza la mawaziri kila baada ya miezi miwili...:). Lakini nina imani na huyu mama kwamba hata kama atapewa uwaziri bado anaweza kuendelea kuzungumza bila woga dhidi ya ufisadi mkubwa unaofanywa dhidi ya Watanzania. Tusubiri tuone, lakini mimi nina imani naye.
 
Nimemaliza kusikiliza, nikaenda moja kwa moja kuangalia CV yake kwenye web ya bunge. She talks the talk ila kuna vishimo vingi kwenye hiyo interview, anaonekana yuko naive kweli au yupo hapo kupiga debe tu. Na unavyosema FMES kwamba hataki uwaziri, well, unaweza usiwe waziri ukawa mpiga spin tu wakati na wewe unafaidika. This is my opinion, sio kwamba yuko hivyo.

MKJJ, asante kwa interview. Nimependa, yuko very articulate, na kama FMES unasema anachukua digrii ya uchumi, itamsaidia sana. Lakini kama ndio anamalizia halafu analysis yake ya mambo ndio hii, na mnapigia debe huyu ndo mmoja wa wakombozi wa Tanzania, then am sorry, I see no bright future. I mean, kiongozi makini huwezi ukakaa ukafananisha apartheid na matatizo yetu. I am sorry, but she was wishy washy. Her kind of language can win her votes though with Tanzanians in the villages!!

Sam, nimekuwa nikiuliza muda mrefu hapa, Nyerere aliachia madaraka vipi? Mimi naamini matatizo yameaanza 1985.
 
Nimemaliza kusikiliza, nikaenda moja kwa moja kuangalia CV yake kwenye web ya bunge. She talks the talk ila kuna vishimo vingi kwenye hiyo interview, anaonekana yuko naive kweli au yupo hapo kupiga debe tu. Na unavyosema FMES kwamba hataki uwaziri, well, unaweza usiwe waziri ukawa mpiga spin tu wakati na wewe unafaidika. This is my opinion, sio kwamba yuko hivyo.

MKJJ, asante kwa interview. Nimependa, yuko very articulate, na kama FMES unasema anachukua digrii ya uchumi, itamsaidia sana. Lakini kama ndio anamalizia halafu analysis yake ya mambo ndio hii, na mnapigia debe huyu ndo mmoja wa wakombozi wa Tanzania, then am sorry, I see no bright future. I mean, kiongozi makini huwezi ukakaa ukafananisha apartheid na matatizo yetu. I am sorry, but she was wishy washy. Her kind of language can win her votes though with Tanzanians in the villages!!

Mkuu Nzokanhyilu, ahsante!

Nakwambia pale alipo analogize apartheid na CCM ndio alinichosha akili! LOL!

Ahsante mkuu. Na hayo mengine yote ni sawa sawa na yale niliyo yasema. Mama yuko naive ile mbaya. Nadhani Mwnkjj kamshtukia sema ni mgeni wake asingeweza kumbana sana mbavu. LOL!

Yani, imagine yule Mama ndio hope yetu! LOL! Maaaan! Yani sina mbavu, siamini!
 
Gap kubwa kati ya utajiri mkubwa waliokuwa nao mafisadi na hali halisi ya maisha ya Watanzania walio wengi unaweza ukaifananisha na apartheid ambapo weusi wa Afrika kusini walikuwa wanabaguliwa kielimu, kiuchumi, n.k. Pamoja na SA kuwa na kiwango na uchumi mzuri ukilinganisha na nchi yeyote ya kiafrika lakini weusu walikuwa hawafaidiki na uchumi huo mzuri. Ukiangalia hili ndilo linaloendelea sasa hivi Tanzania watoto kutoka katika familia za kimaskini wanabaguliwa kielimu, kiuchumi. Wengi hawapati mikopo ya kuwawezesha kupata elimu ya juu, wale wanaobahatika kupata elimu ya juu kwa sababu majina ya wazazi wao hayajulikani na hayana uzito wowote inawawia vigumu mno kupata ajira, tumeona mfano wa BoT ambako watoto wa vingunge wamejazana huko na katika mawizara mengine mbali mbali. Inapotokea kijana fulani anapata kazi kutumia jina la baba yake au mama yake na mwingine anakosa kazi hiyo kwa kuwa jina la baba yake au mama yake halina uzito wowote Tanzania, huo ni ubaguzi.

Hivyo kuna similarities za kiasi fulani kwamba sasa hivi Tanzania kuna kikundi cha watu wachache wanatumia nyadhifa zao kuwabagua walio wengi na hatimaye wengi wa Watanzania wanaanza kukata tamaa ya maisha.
 
Bubu, lets agree to disagree. Hiyo ya apartheid ni cha mtoto. Alichonimaliza ni kum-quote JK. Nadhani Mkandara kawahi kumaliza hapo kila kitu. Na ndio maana tunasema aidha ni naive, au kapandikizwa apige debe. Nitakuwa wa kwanza kumwomba msamaha aki prove otherwise. The woman has potential, but longway to go, and I would love for her to reach that potential that can move Tanzania.

So far, the way i see it, she is just a politician playing her cards! We really are desperate for a genuine leader aren't we?
 
The woman has potential, but longway to go, and I would love for her to reach that potential that can move Tanzania.

Sawa sawa na hapa tuko ukurasa mmoja, lakini after Muungwana Tanzania tunaweza kuongozwa na anybody ninasema yoyote yule anaweza ktutongoza, kama tuliweza kuongozwa na Mwinyi come on man!!

Tanzania sasa hvivi tunahitaji kiongozi anayeweza kukeme viongozi wenziwe na anayeweza kuchukua hatua nzito za kurudisha na kusimamia mali za taifa, so far wote wenye visomo vikubwa wameshindwa, labda huyu mama ni naive, lakini sidahni kama Lowassa alikuwa naive kama huyu mama, na sasa tutamlipia maisha yake yote as a nation mpaka anakufa,

Tanzania tunaweza kuongozwa na mtu yoyote yule kwa sababu kama mama kilango ni naive, sijui sisi wananchi tunaoichagua CCm tukoje?
 
mama malecela ni kiongozi mzuri kama mbunge, ila urais hapana. kukemea tu sio sifa tosha ya kuweza kuwa rais.
bado hajakaa kwenye nafasi yenye majaribu tukaona jinsi anavyoweza kuyamudu na historia ya maisha yake haionyeshi utayari wake wa kuwatetea wanyonge "at any price".
 
Hiyo ya apartheid ni cha mtoto. Alichonimaliza ni kum-quote JK. Nadhani Mkandara kawahi kumaliza hapo kila kitu. Na ndio maana tunasema aidha ni naive, au kapandikizwa apige debe. Nitakuwa wa kwanza kumwomba msamaha aki prove otherwise. The woman has potential, but longway to go, and I would love for her to reach that potential that can move Tanzania.

So far, the way i see it, she is just a politician playing her cards! We really are desperate for a genuine leader aren't we?

Oh yes we are!

But I think that desperation won't last too long. Once this contemporary generation of leadership fades away, which naturally will happen, there will be a seismic shift in the caliber of leadership to obtain from a newer generation. Once new blood gets on board change will happen almost instantaneously. So, I'm just waiting. If we can't upend this entrenched incompetent incumbency through merit-based democracy, it will be compelled to go away by force of nature. When their legs can't run away to foreign lands to dodge justice. When their fast-talking mouths can't run as fast anymore. When their bodies can't respond to their venal minds anymore. Then we'll have a clean slate to start rebuilding our tore-up nation!
 
Nafuatilia mjadala wenu kwa kina.... nafurahia uchambuzi wa majadiliano. Niseme kwamba tulizungumza zaidi ya hayo lakini vimitambo vilikorofisha baadaye, so ninamatumaini siku si nyingi tutapata nafasi ya kuzungumzia mengine ambayo hatukuyazungumza hapo.

Hivyo, naomba tusimhukumu kwa ukali sana na tuwe fair kidogo kwa sababu huu wote ni mwanzo. Tusiwe wepesi kukatisha watu tamaa hata kwa kidogo wanachofanya. Pia lazima tutambue yule "Kiongozi Mkamilifu" ambaye tunamfikiria yupo au anakuja hayupo kwani wa aina yake hawapo duniani. Tusije tukawa kama wanaomsubiria Masiha au Mahdi au yule mjumbe wa nyakati za mwisho.

We sometimes have to do with what we have.... just the best we have.... Nimezungumza na watu wengi na viongozi wengi ni wachache wanaoweza kuja na kuzungumza nami on record. Wengine nikipiga wanachomoa tu as soon as I introduce myself. So, binafsi I feel honored kuzungumza kwa uhuru na Mhe. Malecela.

Anaweza kuimprove? absolutely! Je anaelewa nadharia zote za uchumi, siasa, sayansi na mahusiano ya jamii.. hell no! is he trying to? you betcha! Labda I'm too much a realist than an idealist I used to be.
 
Mtanzania,
samahani mkuu nitatofautiana nawe ktk hili kwa sababu nadhani unachojaribu kujenga hapa ni ile dhana ya kwamba huwezi kupigana na Ujambazi kwa sababu ulikuwepo toka enzi za Adam...
Hali ya Ufisadi nchini inatisha sasa hivi na nakataaa kuwa hali hiyo ilikuwepo toka enzi za Azimio la Arusha. Ni majungu mnayojaribu kuyapika kwa sababu tu hamkupenda Azimio lile na kama nitakuuliza leo sababu za kutolipenda Azimio la Arusha utanipa jibu tofauti kabisa pinzani na usemi wako wa awali.
Kisha Mama Malecela hakuwa na haja ya kusema ni mali asili gani wakati anaongea na Mtanzania wala Mwanakijiji hakutaka kujua kwa sababu anaelewa picha nzima..sema tu kuna vitu ambavyo hafahamu kwa sababu kaja wazi kabisa na leo hii CCM wanamwona kwa jicho tofauti kabisa, pamoja na kwamba bado alikuwa anakitetea chama
Mkuu ni wazi kabisa matatizo ya Ufisadi yamejitokeza baada ya sheria kupita..
Hata huko Arabuni wapo ubakaji upo lakini kutokana na sheria zao nadhani Saudi Arabia ndio nchi yenye crime chache kuliko zote duniani..lakini kama kesho wataruhusu madangulo, madawa ya kulevya na umalaya basi hizo criime zitazidi na kitu cha kwanza kutazama ni hilo Azimio lililopitisha kuhalalisha vitu hivyo..
Nitarudia kusema Ubaguzi upo kila sehemu duniani lakini lile Azimio la kubeba Apartheid ndilo lililowajenga wazungu chuki zaidi ya kuwatenga weusi.. leo hii baada ya kuondoa Azimio hilo ubaguzi umepungua kilichobakia ni ubaguzi kama hulka ya mtu binafsi. mwenyewe umeona hao weusi tuliwakomboa tayari wameanzisha chuki dhidi ya wakombozi wake...Kwa hiyo Ubaguzi upo tu siku zote hata hapo Bongo upo, kesho weka Azimio la kuwatenga Wapemba kisha utaona matokeo yake...
 
Msingi wa mazungumzo na Mama Malecela ni mambo makubwa matatu:

a. Tuna tatizo na tatizo letu linahusiana na umiliki na mgawanyo wa raslimali za nchi yetu. Kikundi cha watu wachache kinaanza kujitokeza kumiliki raslimali za nchi yetu na dalili ni kuwa wanafanya hivyo kwa kutumia nafasi zao, mambo nje ya sheria n.k Katika hili angeweza kutolea mfano wa Zimbabwe, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya ardhi yenye rutuba ilikuwa mikononi mwa asilimia 5 ya watu ambao ndani ya karibu asilimia 90 na zaidi walikuwa ni watu weupe. Ni jambo hilo hilo Afrika Kusini kwani tatizo lao halikuwa tu kwenye ubaguzi wa rangi bali umiliki na access ya mali ya Taifa. Mama Malecela anasema Tanzania tumeanza kuwa na tatizo hilo. Ukienda kusikiliza hotuba ya Mhe. Zitto alipokuwa Michigan utakutana na kitu hicho hicho. Watawala wetu na mfumo uliopo sasa umeanza kutengeneza watu wanaokata tamaa na kama alivyosema mama Malecela "hakuna mtu mbaya kama aliyekata tamaa".

b. CCM na wabunge wa CCM walifikiri (kwa makosa) kuwa kusimama kuitetea CCM na serikali yake bila kuangalia kwa ukaribu kinachotetewa walikuwa wanatetea viongozi wabovu. Anasema na kwa usahihi suala la Richmond lilikuwa kile kinachoitwa "unyasi uliovunja mgongo wa punda". Kwenye suala la Richmond wabunge wa CCM walitambua kuwa wametetea ubovu na Kamati ya Mwakyembe iliwaonesha hivyo; wasingeweza kusimama na kumtetea Lowassa, Karamagi au Msabaha. Hasa baada ya kuitetea CCM kwenye suala la Buzwagi, lile la Buzwagi liliitikisa CCM kutoka ndani kuliko wengi wetu tunavyofahamu na waliapa .. haitatokea tena.

c. Kwamba hatuwezi kuendelea jinsi tulivyo sasa lazima tubadilike na katika kubadilika huko ni lazima tubadilishe mfumo wa umiliki mali. Kimsingi katika hili suala la kwanza ni access, nani anaweza kuifikia raslimali ya nchi yake. Je tuna nafasi sawa ya kufanikiwa? Akitoka mtu Kigonsera au Ujiji na akaja na milioni 20 na hamfahamu mtu yeyote Dar na anataka kununua kiwanja pale Tabata au Mikocheni, kwa kiwanja chenye thamani ya 15 milioni? Lakini kuna familia ya kiongozi "X" ambao wanakitaka kiwanja hicho kwa milioni 10 lakini wakalipa milioni 5 za pembeni. Huyo mtu wa Kigoma hataki kulipa rushwa au commission yoyote ya pembeni?

Hivyo kuna tatizo hilo la access lakini la pili ni tatizo la fairness. Je mtu yeyote Tanzania atatendewa kwa haki?

d. Lazima tubadilike. Katika mazungumzo yake na ndio msingi wa yale tuliyoyaona Bungeni ni kuwa lazima tubadilike. Wao wabunge wa CCM wameona hawawezi kuendelea jinsi walivyokuwa. Sasa hivi bila ya shaka kuna new alignment in the political landscape of our country and especially within the ruling party. Suala la Mkapa ambalo liko njiani will probably draw a very sharp line ndani ya CCM; je mstari huo utabadilisha nini? Nikiangalia kutoka mbali naweza kusema hivi na ninaomba mninukuu:

CCM itatoka na kuja kuwa chama chenge nguvu zaidi, chenye kuaminika zaidi na chenye kukubalika zaidi katika kupambana na ufisadi. Endapo CCM itawachukulia hatua kina Mramba, kitaongoza mapambano ya kuirudisha Kiwira na kumcensure ex president kitajijengea nafasi kubwa sana ya kuendelea kutawala kwa muda mrefu ujao. Lakini gharama yake kubwa itakuwa ni kuangushwa kwa vigogo wa CCM na wale walioongoza mapambano haya ifikapo 20 ili mstari wa kuachana uwe permanently drawn.
 
1. Mama Kilango ni mbunge alianza kwa kupewa bure ubunge na sasa ni mbunge wa kuchaguliwa, ni vitu viwili tofauti na ni very important kwenye ku-determine msimamo wa mbunge bungeni, the point hapa ni kwamba tufike mahali bongo katiba ibadilishwe tusiwe na wabunge wa bure tena!

2. Mama ni former mwalimu wa Kisutu Sekondari, accountant ATC, Senior Accountant Gulf Air, Successful Business Woman on her own rights, na sasa mbunge wa Same East, makamu wa mwenyekiti kamati ya bunge Miundo Mbinu, mwenyekiti kamati ya bunge ya Ethics kwa viongozi wa taifa, ameweza on her own kufungua maduka makubwa ya nguo between Dodoma, Darsalama na Same, na vifaa vya ujenzi kwa kuleta bidhaa hizo kutoka USA na Europe, lakini hana nadharia ya sayansi, uchumi na mahusiano ya jamii? Pleeeeease jamani ma-professor wa JF damn!

3. Urais wa Tanzania? hivi kuna mahali popote kwenye interview ambapo amesema kuwa anahitaji ana mpango wa kugombea urais wa Tanzania? Ina maana all this nasty comments ni kwa sababu kuna wanaodhani kuwa atagaombea urais au? Kuacha Mwalimu ni nani mwingine aliwahi kuwa na hizo qualification za urais kama zinavyotakiwa hapa JF?

Ninaomba ksuema hivi, Mama Kilango anahitaji some adjustments touch ups hapa na pale kwenye view zake on important ishus za taifa, lakini sioni anything serious ambacho akiamua kugombea urais kinaweza kumzuia, kwanza ni haki yake kama Mtanzania, na kama anatimiza the most important qualification yetu CCM ya kuwa na angalau First Degree that is all what counts watakaoamua ni wananchi, na record lakini sisi wananchi wa Tanzania ndio tutakaoamua kulingana na safu ya wagombea na records zao period, personal problems za watu hazita-count kwenye taifa kama zinavyo lazimishwa hapa JF, hapana!

Mimi ninamtakia mafanikiio mema na safari njema ambayo ninajua kuwa itakuwa ni ndefu sana, maana kwa maoni mengi ninyoyaona hapa ni kwamba tayari amerithi maadui na marafiki, ninaamini kuwa anlijua hilo kwa karibu sana!

Ahsante Wakuu!
 
1. Mama Kilango ni mbunge alianza kwa kupewa bure ubunge na sasa ni mbunge wa kuchaguliwa, ni vitu viwili tofauti na ni very important kwenye ku-determine msimamo wa mbunge bungeni, the point hapa ni kwamba tufike mahali bongo katiba ibadilishwe tusiwe na wabunge wa bure tena!

2. Mama ni former mwalimu wa Kisutu Sekondari, accountant ATC, Senior Accountant Gulf Air, Successful Business Woman on her own rights, na sasa mbunge wa Same East, makamu wa mwenyekiti kamati ya bunge Miundo Mbinu, mwenyekiti kamati ya bunge ya Ethics kwa viongozi wa taifa, ameweza on her own kufungua maduka makubwa ya nguo between Dodoma, Darsalama na Same, na vifaa vya ujenzi kwa kuleta bidhaa hizo kutoka USA na Europe, lakini hana nadharia ya sayansi, uchumi na mahusiano ya jamii? Pleeeeease jamani ma-professor wa JF damn!

3. Urais wa Tanzania? hivi kuna mahali popote kwenye interview ambapo amesema kuwa anahitaji ana mpango wa kugombea urais wa Tanzania? Ina maana all this nasty comments ni kwa sababu kuna wanaodhani kuwa atagaombea urais au? Kuacha Mwalimu ni nani mwingine aliwahi kuwa na hizo qualification za urais kama zinavyotakiwa hapa JF?

Ninaomba ksuema hivi, Mama Kilango anahitaji some adjustments touch ups hapa na pale kwenye view zake on important ishus za taifa, lakini sioni anything serious ambacho akiamua kugombea urais kinaweza kumzuia, kwanza ni haki yake kama Mtanzania, na kama anatimiza the most important qualification yetu CCM ya kuwa na angalau First Degree that is all what counts watakaoamua ni wananchi, na record lakini sisi wananchi wa Tanzania ndio tutakaoamua kulingana na safu ya wagombea na records zao period, personal problems za watu hazita-count kwenye taifa kama zinavyo lazimishwa hapa JF, hapana!

Mimi ninamtakia mafanikiio mema na safari njema ambayo ninajua kuwa itakuwa ni ndefu sana, maana kwa maoni mengi ninyoyaona hapa ni kwamba tayari amerithi maadui na marafiki, ninaamini kuwa anlijua hilo kwa karibu sana!

Ahsante Wakuu!

Kama nimekuelewa vizuri unatuma ujumbe kuwa inawezekana hayuko tayari sasa hivi lakini anaweza kujiandaa na kuwa tayari hapo baadae.

Kama nimekuelewa vizuri basi nakubaliana na wewe na kukuunga mkono.
 
Back
Top Bottom