KJ Leo: MwanaHalisi Sasa Wajiandaa

Sumaku

Member
Feb 17, 2009
53
1
MwanaHalisi wajiandaa

19 May 2009 4 views No Comment

Kubenea; “ Tutaiomba Mahakama itupilie mbali hukumu’

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Mahakama Kuu ya Tanzania ikiwa imeamuru gazeti la MwanaHalisi, kumlipa fidia ya Sh bilioni 3, Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, kutokana na kuandika habari za kumkashifu zikimhusisha na kampuni ya Richmond, imefahamika kuwa uongozi wa gazeti hilo umechukua hatua za kukabili hukumu hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi, inayochapisha gazeti hilo, Bw. Saed Kubenea, kati ya hatua walizokwishachukua kukabili hukumu hiyo ni pamoja na kuwasilisha ombi Mahakama Kuu kulalamika kuwa hukumu hiyo ilitolewa bila wao kupewa nafasi ya kusilikizwa.
“Tayari tumewasilisha ombi letu Mahakama Kuu kueleza kwamba hukumu imetolewa bila sisi kutendewa haki kwa kusikilizwa, lakini pia tunataraji kuiomba Mahakama ya Rufaa itupilie mbali hukumu ya awali ya Mahakama Kuu,” alisema Kubenea katika mazungumzo yake na gazeti hili la Kwanza Jamii.
Alisema wataiomba Mahakama ya Rufaa kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo kupitia kwa mawakili wa kampuni hiyo.
Jopo la mawakili wa gazeti la MwanaHalisi linaongozwa na wakili maarufu nchini, Mabere Marando, ambaye aliwahi kuwa Mbunge kupitia Chama Cha NCCR-Mageuzi, na pia kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, kilichokuwa na nguvu kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.
Hukumu hiyo iliyotolewa Jumanne wiki iliyopita, dhidi ya MwanaHalisi kutaka Rostam alipwe Sh bilioni tatu kutokana na kukashifiwa ilitolewa bila kusikilizwa walalamikiwa kutokana na MwanaHalisi kuchelewa kuwasilisha utetezi wake kwa wakati na hivyo kutoa nafasi kwa kesi hiyo kusikilizwa upande mmoja.
Nakala ya hukumu hiyo inaelekeza kuwa Bw. Rostam Aziz alipwe fedha hizo kama fidia ya kukashifiwa katika habari zilizoandikwa na MwanaHalisi.
Habari iliyoleta kasheshe hilo ni ile iliyoandikwa na kupewa kichwa cha habari; “Richmond ya Rostam.

Chanzo: http://www.kwanzajamii.com
 
Back
Top Bottom