Alipokuwa anajiuzulu alisema ameonewa. Kama ndivyo je mbona habishi linapokuja swala la kulipa fidia kwa hao hao aliowakataa kipindi kile?
ukifuatilia kauli zake nyingi za karibuni utagundua kuwa yupo kwenye mashaka fulani na kuna kitu anategeategea kwa kujaribu kupata mass support
Ww vipi? Si kama alionewa aseme wasilpwe maana ilishamdhuru? Huoni mambo yanavyukuaga ? Huwezi kudangaya for ever.Unataka aseme nini!!
Bongo ni nchi ya dili za wizi.
Ukiwa katikati ya dili chunga ulimi wako.
Goood vision, though difficult to implement! Time will tell.
Huku Sumaye akigusia kwa kifupi, kambi hiyo ndogo ya upinzani imetoa tamko katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana, ambalo Katibu wake David Kafulila, alisema kitendo cha Serikali kutaka kuilipa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa bungeni ni sawa na kuchezea moto.
Chimbuko la Dowans liliangusha Serikali madarakani, hivyo Serikali inatakiwa kutoa nafasi kwa sakata hili kwenda bungeni ili ieleze iweje kampuni batili ilipwe kiasi hiki cha fedha, alifafanua Kafulila, hatua ambayo itaiweka Serikali ya CCM katika ncha ya kisu.
Katibu huyo wa kambi hiyo ndogo, alifafanua kwamba ndani ya Serikali kila kiongozi ana mtazamo wake kuhusu malipo ya Dowans na kusisitiza, suala hilo linatakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.
Sakata la Dowans Tanzania ni sawa na Goldenberg scandal iliyoangusha utawala wa chama cha Kanu nchini Kenya, kashfa hii ilianza mwaka 1993 na kumalizika 2002, Richmond na Dowans ilidumu tangu 2006 hadi sasa hakuna majibu,alisema Kafulila Kafulila ambaye amewasilisha kusudio lake la kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhoji sababu zinazoifanya Serikali isiwajibike kwa kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwenye sekta ya nishati, alisema Serikali ikipuuza suala la Dowans itapunguza uhalali wake wa kisiasa.
Pamoja na kuwa kambi hii si rasmi, lakini hatuwezi kukaa kimya katika mambo ya msingi, Dowans ni suala ambalo haliwezi kuzimwa hivi hivi tu wakati ukweli haujajulikana, na kwambia CCM itangoka madarakani sababu ya Dowans kama ikifanya mchezo, historia ya Kanu itawahukumu, alisema Kafulila. Aliongeza kwamba, kama CCM hakitang'oka madarakani basi kuna uwezekano nchi ikakumbwa na machafuko.
Dowans isilipwe mpaka sakata hili lifike bungeni na kupitishwa katika mkaa wa moto wa wabunge, wakilipuuza hili la malipo ya Sh94 bilioni basi wanaweza kupuuza hata malipo feki ya Sh100 bilioni, alisema Kafulila.
Alifafanua, Dowans ikilipwa kabla ya kujadiliwa bungeni maana yake ni kwamba suala hilo litapanuka na kuongeza kuwa ikiwa hivyo, atawaomba wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na Serikali.
Hivi hii nguvu na mbio kubwa za kuilipa Dowans zimetoka wapi, mbona malipo ya wastaafu wa EAC na walimu hayapewi kipaumbele, mimi hoja yangu imelenga zaidi hukumu ya ICC kuhusu kulipa Dowans kiasi hiki cha fedha,alisisitiza Kafulila.
Alipoulizwa kwamba haoni kurudisha sakata la Dowans bungeni linaweza kuibua mengine kuhusu sakata la Richmond ambalo lilisababisha mawaziri kujiuzulu, Kafulila alisema; ...ninachokwenda kuhoji bungeni ni suala la hukumu ya ICC kuilipa Dowans, nataka maelezo katika hilo, najua kuna ambayo hayakusemwa katika ripoti ya Richmond iliyotolewa bungeni na ile kamati ya akina Mwakyembe, inawezekana yakaamka tena, hilo sijui, lakini likiwa hivyo atakayevuliwa nguo chafu na kuvalishwa safi ataonekana.
Source: Mwananchi
a) wakati hukumu ya mahakama ya kimataifa ya biashara imeelezwa kusajiliwa kwenye mahakama ya biashara, uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hukumu hiyo haihjasajiliwa katika Registry ya mahaklama ya Biashara ya Tanzania. Badala yake Annexes chacheche ndizo zilizosajiliwa katika "normal Registry" ya High Court. Hii tafsiri yake nini na nani ana ghilibiwa. Ni kwanini mahakama imepokea tu annexes badala ya hukumu yenyewe kama inavyotakiwa na sheria?