Kizungumkuti Dowans

CC ya CCM sasa yabariki rasmi UDINI kuwa ni sera yake ya kitaifa baada ya wao kulikwepa kulikemea kama walivyofanya CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA.

Cha ajabu hata chombo chao binafsi cha UVCCM nacho kilikwepa kulikemea hii sera mpwa ya baba yao kutugawa kitaifa kwa misingi ya imani zetu na sisi tunasema; HUGAWANYIKI, HATUDANGANYIKI na Utaifa mbele kama tai tunapodai haki zetu!!!!
 
Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
 
Viongozi wa nchi, fanyeni hima kuinusuru hali hii, msiwalipe Dowans-Richmond, mtawadhulumu watanzania. Someni alama za nyakati kuinusuru nchi, wananchi wameanza kuchoka na ubabaishaji, ufisadi na kubebanabebana. Yanayoendelea sasa si lengo la watanzania. Rekebisheni makosa, simameni imara yasijetokea ya Tunisia na Ivory Coast. Viongozi wetu kumbukeni kuwa tabia/mielekeo na mienendo ya binadamu ni ileile pale wanapochoshwa na hali fulani.Tusisubiri hadi watanzania wachoke na hali ya mambo, inabidi kusimama imara kutetea haki za watanzania na kukemea waziwazi vitendo vyote vya dhuluma,ufisadi,ugandamizaji,unyanyasaji na unyamazishwaji, Mkiikataa hali ya dhuluma tunayotaka kufanyiwa na hawa Dowans-richmond, Mtakuwa mmeukataa Ukoloni mamboleo. Mkiikubali hali hii, basi mtakuwa mmeukubali ukoloni mamboleo, na Uhuru wetu utakuwa umeingia dosari. Wala msitetee kuendelea kuwalipa,KATAENI, Mkikataa na Watanzania watawaunga mkono, ila mkikubaliana na dhuluma hii, Watanzania wataweka shaka na pengine kuwakataa ninyi na hao Dowans-richmond. MSISUBIRI HADI WATANZANIA WAKATAE, ENYI VIONGOZI WETU KATAENI SASA kwani wakati ni huu.
 
Profesa Muya ashangazwa serikali kutaka kulipa Dowans
Friday, 21 January 2011 20:49

Zaina Malongo
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utawala bora, Maendeleo na Uchumi (CGG&ED), Profesa Maxi Muya, ameshangazwa na kauli ya serikali kutaka kulipa Kampuni ya Dowans.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Profesa Muya alisema haiwezekani kulipa kampuni ambayo mmiliki wake hajulikani kama inavyodaiwa kwa Dowans.

“Ninachokishangaa ni kauli inayotolewa na serikali kulipa deni kwa kampuni ambayo mmiliki wake hajulikani, halafu anatangaza na kung’ang’ania kulipwa,’’ alisema.

Profesa Muya alisema taasisi bandia haiwezi kutaka kulipwa, labda kuna mtu ambaye yupo nyuma yake ambaye hataki Watanzania wamtambue.

Alihoji iwapo kampuni inadai kulipwa, nani ambaye anakwenda kupokea malipo?
Profesa Muya alitumia nafasi hiyo kutaja mikakati ya miaka mitano (2011-2015), kwa taasisi yake katika kuelimisha wananchi juu ya kubaini mambo wanayotakiwa kufanyiwa na kiongozi wanapomchagua.

Alisema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wanachi kuwa, baadhi ya viongozi hawawatambui wanaowaongoza.

Profesa Muya alisema CGG&ED imejipanga kuondoa hali ya ubinafsi uliopo, baada ya kubaini uongozi ndio tatizo kwa watendaji.

“Tunachofanya sisi tumeandaa taratibu na mfumo wa kuboresha na kumdhibiti kiongozi anayeongoza kwa ridhaa yake, bila kujua anachotaka kuongoza,” alisema.

Kwa upande wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, alisema hivi sasa kuna mkanganyiko juu ya wananchi kudai kubadilishwa kwa katiba.

Tendwa alisema hivi sasa taasisi kama CGG&ED inatakiwa kukaa na kuelimisha wananchi kuhusu kilio ambacho wanalalamikia.
 
Alihoji iwapo kampuni inadai kulipwa, nani ambaye anakwenda kupokea malipo?
Profesa Muya alitumia nafasi hiyo kutaja mikakati ya miaka mitano (2011-2015), kwa taasisi yake katika kuelimisha wananchi juu ya kubaini mambo wanayotakiwa kufanyiwa na kiongozi wanapomchagua.

Usiulize majibu profesa ..........................Rostam Aziz ana "powers of Attorney" na hizo hela zinakwenda moja kwa moja kwenye personal account kwa fedha za kampuni.......................jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za nchi.................................Kampuni ambayo ipo nchini inakatazwa na sheria zetu kutoa "powers of Attorney"..........lakini kwa mafisadi kila kitu chawezekana tu....................................................sasa hivi wameanza kubuni uporaji mwingine......................................
 
Kulingana na hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya usuruhishi wa migogoro ya kibihashara,mh.Rostam Aziz ndiye aliyepewa dhamana na wamiliki wa kampuni hiyo kusimamia shughuli zote za Dowans hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuendesha akaunti ya kampuni hiyo iliyoko crdb bank ltd. Hivyo sioni kama suala la kujua wenye kampuni hiyo ni wakina nani, linapashwa kuwa na utata; kwa upande mmoja anaweza akaulizwa Rostam mwenyewe ili awabaini wale anaodai walimweka. Vile vile crdb bank nao wanaweza kuulizwa iliwaweze kudhibitisha ni nani wamiliki halali wa akaunti ambayo Rostam Aziz alipewa dhamana ya kuiendesha
 
Hii hoja inayoibuliwa na huyu bwana, inaweza kuwa na mantiki; kama kampuni imesajiriwa Tanzania, inawezaje ikampa mtu mwingine "power of attorney" kwaajili ya kusimamia shughuli zake hapa nchini? Hii inawezekana tu kwa "off shore" companies." Nakaribisha mchango juu ya suala hili.
 
Wengi wanaongelea kupinga malipo ya DOWANS lakini hawasemi nini kifanyike kuzuia serikali isilipe. Tunisia muuza mboga aliamua kijichoma baada ya polisi kumnyang'anya mboga zake na hapo ikawa ni maandamano mpaka raisi akatimka. Sasa hapa kwetu, gas juu, umeme juu, nauli juu, sukari juu, mkate juu, ada za shule juu wote kimya. Inawezekana watanzania wote tu wezi ndio maana tunamudu maisha pamoja na dosari zote hizo
 
Hii si mada ya kujadiliwa na great thinkers, ninaimani kuwa dowans ni ltd co, kama hivi ndivyo wamiliki hawana liability, pia kama ni issue ya nani ni mumiliki msajili wa makampuni analojibu hata hivyo kumjua mumiliki as an individual is useless.
 
Tumjue tusimjue haisadii kitu. Serkal yetu ni ckio la kufa na lazma itamlipa!, kelele za mlango zinamzuia mwenye nyumba kuingia? Cc tutaseka sana coz ccm ndo kila kitu. Hata wakisema wanakuua hawashindwi! Ndg yangu kama unaweza jiunge nasisi wanamapinduz tuendeleze harakati za kuikomboa nchi kutoka mikonooi mwa mafisadi
 
Suala si mmiliki ni nani. suala ni kwamba taratibu na sheria zimekiukwa toka kuanzishwa au/na kuasajiliwa kampuni hii nchini.pili walipata mkataba kihalali? if yes kwa nini ulivunjwa? na kavunja na atawajibishwa?
je tunahitaji kulipa kampuni feki? serikali ilichukua jitahada gani mpaka tukashindwa kesi?
sasa hela na kulipa zinatoka wapi?

Nani anawajibika kwa uzembe au uwizi huu?
 
Wengi wanaongelea kupinga malipo ya DOWANS lakini hawasemi nini kifanyike kuzuia serikali isilipe. Tunisia muuza mboga aliamua kijichoma baada ya polisi kumnyang'anya mboga zake na hapo ikawa ni maandamano mpaka raisi akatimka. Sasa hapa kwetu, gas juu, umeme juu, nauli juu, sukari juu, mkate juu, ada za shule juu wote kimya. Inawezekana watanzania wote tu wezi ndio maana tunamudu maisha pamoja na dosari zote hizo

Hapo katika alama nyekundu ndio hasa tulivyo watanzania wote!
 
Baada ya malipo ya DOWANS twaweza sikia mradi wa mabasi yaendayo kasi unaanza rasmi, tusubiri tuone
 
Alipokuwa anajiuzulu alisema ameonewa. Kama ndivyo je mbona habishi linapokuja swala la kulipa fidia kwa hao hao aliowakataa kipindi kile?
 
Pj huyo mkulu alilalamikia kupokwa uPM alipoambiwa asogee kando...kwa hiyo akaona anaonewa kuukosa uPM.
Lakini humu kwenye mshiko yupo saana tu hawezi comment kitu
 
Pj huyo mkulu alilalamikia kupokwa uPM alipoambiwa asogee kando...kwa hiyo akaona anaonewa kuukosa uPM.
Lakini humu kwenye mshiko yupo saana tu hawezi comment kitu

Kweli,kama unamuhusu unataka a-comment nini?? hana,ye atazungukia amani ni muhimu,mara tujifunze kwa wenzetu umuhimu wa amani lakini,msimamo wake hatosema.....ni riziki yake ile na akilazimika kusema atadanganya,bora akae kimya tu......:shut-mouth:
 
ukifuatilia kauli zake nyingi za karibuni utagundua kuwa yupo kwenye mashaka fulani na kuna kitu anategeategea kwa kujaribu kupata mass support
 
Hii hoja inayoibuliwa na huyu bwana, inaweza kuwa na mantiki; kama kampuni imesajiriwa Tanzania, inawezaje ikampa mtu mwingine "power of attorney" kwaajili ya kusimamia shughuli zake hapa nchini? Hii inawezekana tu kwa "off shore" companies." Nakaribisha mchango juu ya suala hili.

Wakuu nadhani huyu jamaa tunayesema ana "power of attoney" alikataa kuwa yeye si mmiliki wa Dowans. Sasa inakuwaje anapewa hizo power wakati amekana kuwa yeye si mmiliki? Wamiliki wa Dowans walitajwa na hakuna hata mmoja anayeitwa Rostam, kwanini tusikae kimya tu na tusilipe watu hewa?

Maswali haya yote yanatuambia kuwa Dowans ni ya kitapeli, na inawezekana wanaoshinikiza ilipwe wanashirikiana na matapeli.

So Richmond imebadilika jina imekuwa Dowans, ni bora kama itaodoka na Pinda tupate PM mwingine anayeweza kuishughulikia.
 
Back
Top Bottom