Kizungumkuti Dowans

I am not sure if this is misplaced but I intended to send it at the lawyer section "Jukwaa la Sheria"
 
Yani upumbavu wa watu 5,utugharimu mil 40! haiwezekani na hatutakubali.Kama mbuai mbuai!!!.
Mmetufanya tulipe hilo deni sisi walalahoi kwa kuongeza bei ya umeme,mnataka mlipetena cash!!!
Dhambi hiyo itatutafuna sisi na nyie pia,asidhani mtu atapona.Tutakutafuteni kokote mliko mpaka tutakapowanyonya macho,hamtatushinda nawahakikishia.kama ni taabu tumezizoea,bora iwe taabu kamili.Naongea kwa uchungu jamani,roho inataka kuacha mwili napoona adha nitakayopata mwezi huu kulipia umeme,na itakayofuata mara baada ya kupanda bei ya vyakula,mavazi na kodi za nyumba ili wafidie pengo sababishwa na upandaji wa umeme.
Nyie hamtaguswa na adha hizi kutokana na ukwasi mlojilimbikizia pasi na kujali wenzenu kule vijijini.Kwanini mateso haya yatufike sisi tusio na hatia? Kwanini mjilimbikizie mali kwa gharama ya damu za watz kule kijijini wasio na kosa wala kujua nini kinaendelea.
Mmekosa hata huruma kwa maskini,mioyo yenu kwanini haioni aibu? mmeumbwaje?
Watu wanapata mlo mmoja tena kwa kubahitisha,nyie mnasisitiza kuwalipa wahuni,watoto wanakaa chini shuleni,hospitali hakuna madawa,maskini wanapinda migongo kwa kilimo msimu mzima wanavuna debe mbili za mazao coz mvua hakuna,ikinyesha mfuriko yanasomba na viwavi wanavamia,hamumfikirii mama anayejifungulia ktk mkokoteni akipelekwa kwa mkunga wa jadi,hao walimu mnaowalipa 90000 eti wajikimu na familia zao kwa mwezi mzima,watoto wanaoombaomba mitaani hamuwaoni? au ndo tuseme mmelaaniwa.Anaulizwa!,eti hajui umaskini wetu unatokana na nini.Tunashindwa kumtofautisha huyu mtu na yule mama mwenye tongotongo nzi wakimng'ong'a na watoto wake 7 wamemzunguka wakilia 'mama njaa' ni haki ya huyu mama kutojua chanzo cha umaskini wake. Sasa hujui umaskini watokana na nini,afu unalipa 94bil kwa wahuni tu.Wenzio watakucheka.
Tukiandamana mnatuchapa risasi,mnataka tuishi mtakavyo.Kwa hili hatutakubali,tuko tayari kwa lolote.MWENYE MASIKIO NA ASIKIE MANENO HAYA.
 
Mimi nashindwa kuamini hawa uvccm kama wanaelewa maana ya hii vita, hawa vijana wamelewa mvinyo ya damu za watanzania na hawajui kitu gani wanapigania, na nani wanampigania na adui ni yupi, anaefaidika ni nani! waziri kijana mwenzao (ngeleja) alitaja wamiliki hadharani,nakutuhakikishia kuwa atalipa pesa, sitta na mwakyembe wakasema haiwezekani kampuni hewa kulipwa pesa za watanzania kwa kampuni hii ya kisanii, ccm vijana nao wanatoa tamko lao kuwa hawaoni sababu ya bosi wao kulipa, huu ni ushaidi tosha ukijumlisha na ambao tumekuwa tukiupata tangu na kabla Lowassa kujiuzuru, kuwa NCHI INAENDESHWA NA WAKORA skendo hizi haziwezi kuisha bila rais kuwajibishwa ni dhahiri kuwa JK na wenzake wamedhamiria kutekeleza haya malipo. Chama chao kimetupa uhakika kila mara tena hadharani kuwa, nchi hii inaliwaje tena na nani, kama hilo halitoshi wadhalimu hawa wanajitahidi kututoa kwenye hoja asilia na kutupeleka kwenye propaganda za udini.

MAONI YANGU, huu ni wakati taifa(mwananchi) tunapaswa kumuwajibisha raisi na wasidizi wake, sababu hakuna kitengo au wizara ktk serikali hii waweza kukuta wizi, uporaji, unyang'anyi, udhalimu ambao hauitaji kuumiza kichwa kwa kufikiri kujua source ni Rais kikwete. wanao uliza kauli ya rais, tamko ama kuakaa kwake kimya! mnataka aseme nini wakati mnajua kabisa kwa uwezo manunuzi na ridhaa aliyopewa awamu ya kwanza,ambayo (naamini pia udhalimu ulifanyika kushinda) akapanga mikakati ya kuiba tena ili ashinde kwa udhalimu huu huu. Any way alijimilikisha urais, tena bila haya ya uso mbele ya watu wake na mataifa. Huyu mtu mnamuomba atoe tamko kwa nani, na la nini, aseme kitu gani! kwamba dowans si kampuni? ama siijui? sihusiki nayo, sijawahi isikia... au najua ninacho kifanya mniache, msiniingilie mamlaka yangu, lazima nilipe pesa za mshikaji, au watanzania walio wengi wako tayari kula nyasi lazima dowans ilipwe, nchi inaheshimu sheria za kimataifa sana nimekuwa waziri/mambo ya nje muda mrefu tunaaminika kwa kutii, au tuvumiliane tu nimalizie dili zangu niwaachie nchi yenu.

Mnataka hasa majibu gani kutoka kwa JK ambayo bado hamjayapata,hamyajui au hamjapewa........this dude is a criminal! he knows that, he is very familiar for his violation of laws and constutution, to which he claim to protect. huwezi kusema unaipenda sheria ya kimataifa kuliko sheria ya watu wako ambayo wewe mwenyewe umeikanyaga na kuidharau. ANGALIZO, Dont expect someone to respect you if you dont respect yourself. wananchi tumeshindwa kujieshimu tumewaruhusu politicians kutununua, kwa fedha,chakula, ulaghai, vyeo, madaraka, ajira, dhuluma, matokeo yake unapo kubali kuuza utu wako kwa hayo, hivyo si kazi yako tena kumpangia mnunuzi akufanyeje au akutumieje? thats non of your business............!!! for him you are a slave and he is the master! usitegemee kushirikishwa, kuombwa ushauri, kushiriki maamuzi, kuhoji,kufuata sheria, kulalamika, kugoma, kukataa,kufurahi, kuwahuru, uhakika wa maisha au kuishi siku nyingi kwa raha, laa! sifa na haki zako zote uliuza kwa kujua ama kutokujua thamani yake. kwako wewe haki yako ni rehema za bwana wako, na wala si uhodari wa kumsihi au kumuomba kutoa tamko kuhusu hali yako kwamba umechoka kiasi gani ama uko hoi kiasi gani,umezalisha kiasi gani na atumie kiasi gani. Lugha hiyo fisadi haijui wala hana shida ya kujifunza, kumbuka alivyokupata...........

NINI CHA KUFANYA, Mtumwa anapochoka NA MAANISHA yule aliyochoka kweli na ana dhamira ya kweli ya kuitaka haki yake aliyo uza au poteza si kwa kumuomba ama kum-please mnunuzi kwa sababu hatakurudishia kwa style hiyo na utangoja sana..... Tanzania, utangoja sana.
kuna wale walio pata rehema za mnunuzi na wanahisi hawaitaji kuitisha haki yao tena, wao wameridhika ingawa nao ni watumwa hata kama tunalingana hali ya machungu na makali ya utumwa. wao ni watiifu na hawako tayari kumsaliti bwana wao, tujitahidi kuwaelewesha kwamba tumechoka:frusty: tukovitani. vita hii sio ya RA ma JK tu kwani tunajua kuna kikundi ambacho kinampa nguvu ya kuchochea ushabiki wa ubadhirifu hao pia ni adui zetu. JF let we have the same aim and same objective, to find who ever against our war...... hawa ndio wanao turudisha nyuma. pili kumshinikiza na kumtaka JK kutoka madarakani... HOW.. BY ANY MEANS NECESSARY.
 
Kama dowans watalipwa na mimi silipi mkopo walionipa kwa ajili ya elimu ya juu...Eeh nimegoma kwa staili hiyo. Mahakamani siendi, kujitia mafuta sijitii. Ila silipi.

Kama na wewe unadaiwa ungana na mimi kutolipa, kama kweli sote tuna machungu na nchi.
 
Mkama, na wewe huafiki DOWANS kulipwa mkuu? Unadhani nini kifanyike kuhakikisha hawalipwi hawa jamaa? Nani anaweza kuhakikisha move ya kuzuia malipo yao inafanyika?

BTW, heri ya mwaka mpya mkuu
 
Mkama, na wewe huafiki DOWANS kulipwa mkuu? Unadhani nini kifanyike kuhakikisha hawalipwi hawa jamaa? Nani anaweza kuhakikisha move ya kuzuia malipo yao inafanyika?

BTW, heri ya mwaka mpya mkuu

Kamati kuu ya CCM imeshapitisha uamuzi wa kuilipa Dowans unafikiri nini kitazuia malipo zaidi ya maandamao ya watanzania wenye uchungu na nchi yao Tanzania nzima,kwa kasi wanayokwenda nayo hata bunge halitaweza kuwazuia.
 
Mkama, na wewe huafiki DOWANS kulipwa mkuu? Unadhani nini kifanyike kuhakikisha hawalipwi hawa jamaa? Nani anaweza kuhakikisha move ya kuzuia malipo yao inafanyika?

BTW, heri ya mwaka mpya mkuu

Melo, kudhibiti hawa jamaa ni kazi rahisi sana, sema tatizo linalotuangusha na hawa watu tunaojiita wasomi ktk nchi hii. Hapo problematic ndo inaanzia.

Kama serikali wanawalipa DOWANS, hai-make sense mie kulipa mkopo. Soln ipo na ni rahisi sana kama wasomi wataamua mapinduzi mapya.
 
Zaidi ya Utaratibu wa Mahakama hakuna jinsi nyingine kwa sasa kuzuia tendo hilo.
Utashi wa kisiasa kwa maana ya chama tawala umebariki jambo hili kwa mbwembwe na kibri!
Juhudi za mtu mmojammoja kama anavyoshauri bwana MkamaP ni peanuts, na grand effect yake ni negligible kama siyo negative!
 
Kamati kuu ya CCM imeshapitisha uamuzi wa kuilipa Dowans unafikiri nini kitazuia malipo zaidi ya maandamao ya watanzania wenye uchungu na nchi yao Tanzania nzima,kwa kasi wanayokwenda nayo hata bunge halitaweza kuwazuia.
.

Maandamano mtahatarisha maisha ya watu bure na kuwapa sababu za kukupiga risasi.Kama kweli wewe huogopi kifo cha RISASI kwanini uogope kifo cha NJAA. Watu wote wagome kufanya kazi, simple. Inatulia ndani kwako ama unajiendea shamba lako kwa ajili ya chakula cha hapa na pale. Ni week moja tu ama mbili wote wana resign.
 
Zaidi ya Utaratibu wa Mahakama hakuna jinsi nyingine kwa sasa kuzuia tendo hilo.
Utashi wa kisiasa kwa maana ya chama tawala umebariki jambo hili kwa mbwembwe na kibri!
Juhudi za mtu mmojammoja kama anavyoshauri bwana MkamaP ni peanuts, na grand effect yake ni negligible kama siyo negative!

Mkuu, hapa na maana watu wagome kufanya kazi week mbili wote wakae ndani, wale makapuni binafsi na serikali. Watatoa wapi fedha za kulipa dowans?
 
Kama dowans watalipwa na mimi silipi mkopo walionipa kwa ajili ya elimu ya juu...Eeh nimegoma kwa staili hiyo. Mahakamani siendi, kujitia mafuta sijitii. Ila silipi.

Kama na wewe unadaiwa ungana na mimi kutolipa, kama kweli sote tuna machungu na nchi.

We usilipe kwanza ukione kilichomtoa kanga manyoya mgongoni.
 
Kamati kuu ya CCM imeshapitisha uamuzi wa kuilipa Dowans unafikiri nini kitazuia malipo zaidi ya maandamao ya watanzania wenye uchungu na nchi yao Tanzania nzima,kwa kasi wanayokwenda nayo hata bunge halitaweza kuwazuia.

Zaidi ya Utaratibu wa Mahakama hakuna jinsi nyingine kwa sasa kuzuia tendo hilo.
Utashi wa kisiasa kwa maana ya chama tawala umebariki jambo hili kwa mbwembwe na kibri!
Juhudi za mtu mmojammoja kama anavyoshauri bwana MkamaP ni peanuts, na grand effect yake ni negligible kama siyo negative!
Wanasiasa wanafurahia sana wananchi mnapoonekana mme-give up na kukiri HAMNA LA KUFANYA.

Lakini tukumbuke sisi ndiyo wenye nchi, wengine tumewapa dhamana ya kuendesha, sisi ndio tunaweza kuwaondosha. Ni maamuzi tu.
 
Mkama, na wewe huafiki DOWANS kulipwa mkuu? Unadhani nini kifanyike kuhakikisha hawalipwi hawa jamaa? Nani anaweza kuhakikisha move ya kuzuia malipo yao inafanyika?

BTW, heri ya mwaka mpya mkuu

Daa!! Mzee Melo kumbe na wewe mara moja moja huchanja mbuga humu ndani? Ndio mara yangu ya kwanza kugongana na wewe kitaa.
 
Mi nathani nitham ya woga ndio inagarimu watu kutokupata haki yao na ndio maana wakubwa wengi wanatumia nafasi hii kuchukua hata kile tunachozani tunacho n kujinufahisha.....
PAMOJA TUTAIJENGA NCHI YETU
 
UKO WAPI UZALENDO?: Tsh 94,000,000,000. Hiki ndicho kiasi (kwa makadirio yaliyo karibu) cha mabilioni ambacho Mtanzania anashawishiwa kuwa hakikwepeki kuwalipa Dowans-Richmond. Mbona umeme bado wa mgao? Enyi mnaodai kuwa malipo haya hayakwepeki, waonesheni Watanzania katika Televisheni mambo yafuatayo:-Anuani & Mahali/Eneo hapa Tanzania zilipo Ofisi za Dowans- Richmond, Majina ya Wamiliki wa Dowans-Richmond,Majina ya Bodi ya Wakurugenzi ya Dowans-Richmond, Jina la Mkurugenzi Mtendaji wa Dowans-Richmond, Majina & Cheo cha kila Mfanyakazi wa Dowans-Richmond na Sifa zao za Kitaaluma (CV). Pia uiteni Uongozi wa juu wa Dowans-Richmond uje uongee na Watanzania katika Televisheni ya Taifa TBC 1, waonekane waziwazi, waulizwe maswali, wajibu kwa ufasaha, kinagaubaga na bara-bara hadi Watanzania wote Waridhike. Enyi mnaodai malipo haya hayakwepeki, Jiulizeni kuwa kwa kiasi hiki cha Fedha (Tsh 94 bln), tungejenga nyumba ngapi za walimu Watanzania?au tungejenga maabara ngapi na kununua vifaa vingapi vya maabara kwa shule za sekondari za kata za Watanzania?au tungenunua vitabu vingapi,madawati mangapi kwa shule za awali na msingi kwa wanafunzi watoto Watanzania? au tungenunua matrekta mangapi yenye uwezo wa kulima,kumwagilia na kufua umeme kwa wakulima Watanzania? Enyi mnaodai malipo ya Dowans-Richmond hayakwepeki, ONESHENI MOYO WA UZALENDO NA HURUMA KWA WATANZANIA KWANI FEDHA HIZI NI JASHO LA WAZALENDO WATANZANIA.
 
Tusihangaishe akili zetu.Pesa za kampeni 2000 na 2005 zilichotwa BOT.Na ndo maana yule mdudu KAGODA amesiginwa kwa kisigino kwenye jiwe ambalo ni very rough,can you imagine that mdudu will exist! Aah wapi! Tumeshasahau,sasa uchaguzi tuliandaliwa mezani tukingoja kula tusichokijua lakini kumbuka mwanzo kuna Nnyama Richmund ambaye alijeruhi watu kadhaa na almanusura angua.Mnyama Dowans ni ndama wa Richmund aliyetokomea kusikojulikana,sasa ndama amekua mkubwa kuliko mamayake.Swali ni je,ataua au atajeruhi? Hivi zile bilion50 zilipatikana kwa wapenzi kuchangia kwa kupitia vilongalonga? La hasha hazikutosha ilibidi zingine ziazimwe somewhere. Je, baadaye zirudishweje? Ah!zizini kuna yule mnyama si yuko zizini kwetu?Tuwaambie kusanyiko la waandishi Mnyama anatakiwa bilion 185.Oh! Kusanyiko la watu wote limegoma basi tupunguze maana tutaifilisi hazina na tutaonekana siwazalendo_OK! Basi tuseme bilioni94.Lakini hatutapata faida kubwa,we! Nani kasema? Miaka mitano akaunti zetu za mashariki na magharibi zitakua na pesa nyingi tu,watakula watoto na wajukuu na vitukuu na vilembwe na vilembwe vyao. Ah! Wengine? Hao watakula nyasi. Jamani Dowans ni deni lazima tulipe hata wakiandamana.Wana JF Mnyama huyu anachinjika? Maana ni mpango wa muda mrefu,kama ndio basi tumsake Kagoda na tumchinje pia.Ngoja niwaambi jamani,hii issue ya Dowans itapotea siku si nyingi kwa kutafutiwa issue nyingine sensitive yakutupoteza na kama hamuamini ukifika wakati nitawakumbusha Mungu akipenda.
 
Mi nathani nitham ya woga ndio inagarimu watu kutokupata haki yao na ndio maana wakubwa wengi wanatumia nafasi hii kuchukua hata kile tunachozani tunacho n kujinufahisha.....
PAMOJA TUTAIJENGA NCHI YETU

It is difficult to free fools from the chains they revere.
 
Ndugu nenetwa hawa hawawezi kuyafanya hayo uliyosema kwakua haiwezekani wao kufanya hivyo kwakua dowans +richmond ni kampuni hewa na ni utapeli unaofanywa mchana kweupee,dawa ni kuwa kama tunisia mpaka kieleweke,tupinge kulipwa hawa matapeli kama itawezekana.
 
Back
Top Bottom