Kizungumkuti cha ndoa!

Kama na mimi nina mali ambazo zinatosheleza familia, nitamwacha mali zake aamue yeye mwenyewe ili mradi anazitumia vizuri lakini kama matumizi hayatakuwa mazuri lazima niingilie bila kujali alizipata kabla ya ndoa au baada ya ndoa.

Kama angekua na matumizi mabaya usingemkuta na mali!
 
mhuuuuuuuuuuuuu!!!! haya bwana, kwa hapa jf wapole sana, tena fantastic answers ndo zimetawala, sijui kuhusu actions!
 
Kama angekua na matumizi mabaya usingemkuta na mali!
Anaweza kuamua kuanza kutumia vibaya baada ya kujua sasa yuko na mwenza na mambo yote kuhusu familia ni juu ya mwenza wake, lakini kama matumizi ni mazuri kwa nini nimpangie na mali ni zake?
 
Anaweza kuamua kuanza kutumia vibaya baada ya kujua sasa yuko na mwenza na mambo yote kuhusu familia ni juu ya mwenza wake, lakini kama matumizi ni mazuri kwa nini nimpangie na mali ni zake?

Kama ni hivyo kwanini umpangie mali si zake?Hata kama ataziharibu si zake?
 
BADILI TABIA,hakuna maamuzi ya pamoja,hakuna mahali popote pasipokua na mtu mwenye kauli ya mwisho,kwenye ndoa nako hakuna tofauti,kama unakataa mwanaume asiwe na kauli ya mwisho basi uwe wewe,lakini hujategua hicho kizungungumkuti hapo!Hebu sema utamruhusu awe na kauli ya mwisho kwenye mali yako?

Eiyer,
kawaida kwenye mahusiano mwanamke hata akiwa na kipato kikubwa huwa hana shida kujishusha na kumsikiliza mumewe,lakini kiukweli mwanamke huyo huwa rahisi zaidi kujishusha kutokana na vile mwanaume anavyojichukulia,

mwanaume anapojiamini, anapoketi na mkewe kupanga mikakati ya maisha, anapomsikiliza mkewe mawazo yake, na hii ikiwa katika kujenga maisha yako na kutafuta mafanikio zaidi kwa nini mwanamke akatae kuwa na kauli kwenye mali? na hasa ukizingatia mwanamke hutafuta "security" kwa maisha ya baadae na familia?

kwa nini akatae asiwe na kauli wakati wamezungumza na kupanga pamoja?
kwa nini akatae wakati anajua mali hii (lets say nyumba, ya mwanamke ipangishwe maana mwanamke baada ya kuolewa anahamia kwa mume; na kodi ya nyumba hiyo mwanaume anaiweka kwenye mradi fulani ambao utazalisha na kuongeza kipato cha kuwezesha kufanyia jambo fulani/ amhitaji/ada nk?) hapo mwanamke atakataa?

mwanamke anaweza kukataa kama hujamshirikisha, Kichwa cha familia kimeamka asubuhi anampa taarifa nyumba ya tabata nimepangisha hela nimeweka kwenye mradi fulani. Au mwanmke anaweza kukataa atakapohisi hela imetapanywa kwa njia fulani. au la kama mwanamke mwenyewe ana asili ya choyo na tamaa huweza kukataa,

narudia tena nyumba yenye kujadiliana na kupanga pamoja huwa na mafanikio.
 
Mali mali.....!! Mali kitu gani bna kaeni nazo...............ziwe waume zenu ziwapempe na ziwazalishe watoto! ARRRRRRRRRRGHHH!
Punguza hasira mkuu,
Unajua haya mambo kila mtu ana uelewa wake kulingana pia na malezi,
Alafu kuna baadhi ya mambo ambayo wanawake tunatakiwa kuyakubali(japo wenzangu wengi hawapendi) tu na sikubishana,
Hata ikiwaje hatuwezi kuwa sawa na MWANAUME,tunachofanya ni kubishana tu na kujibebesha majukumu ambayo si ya kwetu na mara nyingi huwa tunachemka!
Km upendo,ushirikiano na heshima ndani ya nyumba ipo basi wadhifa wa baba na ubaki kuwa pale pale usiingiliwe na chochote!
 
Majadaliano ndilo jambo la msingi zaidi lakini hii haiondoi lile hitaji la nani atakuwa na last say katika familia,hakuna penye watu wawili pakose kiongozi.
 
Kama ni hivyo kwanini umpangie mali si zake?Hata kama ataziharibu si zake?
Kama anaenda na njia iliyosahihi hapo sitamwambia chochote lakini kama ataenda na njia sahihi lazima niingilie na naposema kuingilia simaanishi kumzuia abadan anachotaka kufanya nimtashauri kwamba hii njia unayopita sio fuata hii utafika uendako na kama hatasikiliza ushauri wangu atapita njia anayotaka yeye na nitamwacha apite. Kumbuka nimesema na mimi nina mali zinazotosheleza familia.
 
Canta wanawake wa aina yako ni wachache sana now days!I wish ningepata wa mtazamo wa aina hii!
 
Hii nimeipenda sana, mara nyingi mwanaume huwa ni kichwa cha familia. Siamini kwenye dini illa huwa nachukulia bible na quran kuwa ni life principle books au life experience books. Kwanza kwa mwanamke anayependa usawa kwa vitendo huwa wanaachika sana hakai na mwanamme mmoja hata siku moja. uzuri ni kwamba wengi wao huwa ni maneno tu ukimkuta kwake yuko chini kabisaaaaa, nina mifano mingi tu mimi ni mtu mzima. Anayelalama kutaka usawa ujue kwake mpole sana tu. Anataka mifano ya kumpa mumewe

tatizo wanaume wengi hawajui usawa upi ambao unazungumziwa na wanawake wengi,....ipo hivi Usawa unaozungumzwa ni kujadiliana na mke wako kwa chochote unachotaka kufanya,kuwa mateso na manyanyaso kwa wanawake iwe mwiko sababu ni binadamu kama mwanaume...chochote anachoweza mwanamume mwanamke pia anaweza hapa naongelea dharau kwa wanaume kwa wanawake...mahitaji muhimu anayohitaji mwanamume na mwanamke anayahitaji hayo hayo....so hapana kunyanyasana kisa wewe ni Kichwa wakati kichwa hakiwezi kufanya shughuli zote bila ya moyo...so hapa usawa ni kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.....hakuna cha mwanaume wala mwanamke hapo
 
Kama anaenda na njia iliyosahihi hapo sitamwambia chochote lakini kama ataenda na njia sahihi lazima niingilie na naposema kuingilia simaanishi kumzuia abadan anachotaka kufanya nimtashauri kwamba hii njia unayopita sio fuata hii utafika uendako na kama hatasikiliza ushauri wangu atapita njia anayotaka yeye na nitamwacha apite. Kumbuka nimesema na mimi nina mali zinazotosheleza familia.

So what are u trying to say hapa ni kuwa umuhimu wa kumsimamia mwanamke na malizake ni mpaka uwe huna mali?
 
tatizo wanaume wengi hawajui usawa upi ambao unazungumziwa na wanawake wengi,....ipo hivi Usawa unaozungumzwa ni kujadiliana na mke wako kwa chochote unachotaka kufanya,kuwa mateso na manyanyaso kwa wanawake iwe mwiko sababu ni binadamu kama mwanaume...chochote anachoweza mwanamume mwanamke pia anaweza hapa naongelea dharau kwa wanaume kwa wanawake...mahitaji muhimu anayohitaji mwanamume na mwanamke anayahitaji hayo hayo....so hapana kunyanyasana kisa wewe ni Kichwa wakati kichwa hakiwezi kufanya shughuli zote bila ya moyo...so hapa usawa ni kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.....hakuna cha mwanaume wala mwanamke hapo

Ndugu una uhakika na haya maneno yako au ni assumption?
 
Back
Top Bottom