kizibo..

Bellino

Member
Jan 29, 2012
65
10
kizibo akutana na maza mjamzito njiani. mazungumzo"
kizibo.."shikamoo
maza.."marahabaa
kizibo.. "mbona tumbo kubwa?
maza.. "huku kuna mtoto
kizibo.."mzuri ee
maza.. "mzuri kama wewe
kizibo.. "sasa mbona umemmeza?
 
Kizibo: Halooo (akipiga simu kwa mwalimu wake)
Mwalimu: Haloo
Kizibo: Namwombea ruhusa Kizibo hawezi kufika shuleni leo
Mwalimu: Naongea na nani?
Kizibo: Unaongea na baba'angu!
 
Baba Kizibo: Asantee mwanangu lakini mbona umeniletea magazeti mawili?
Kizibo: Nimekosa gazeti la tarehe 10 nikaona nikuletee mawili ya tarehe 5!
Baba Kizibo: Ayaah weeeeh ameshajumlisha! Dah!
 
Mama Kizibo: Gari ikifika Chalinze ndipo ule hayo maandazi yako.
Kizibo: Sawa mama.......(muda ukapita baada ya kuondoka Dar.......)
Kizibo: Konda; konda; hapa tumefika wapi?
Konda: Morogoro
Kizibo: Mi sitaki mi sitaki nilikwambia ukifika Chalinze uniambie nirudishe Chalinze!
Abira kwenye basi: Kweli jama mrudisheni Kizibo Chalinze huyo ni mtoto na alisema toka mwanzo wa safari!
Konda: haya ngoja tukurudishe.....muda ukapita..
Konda: Haya hapa ndiyo Chalinze njoo ushuke fanya haraka..
Kizibo: Aka mi sishuki mama aliniambia nikifika Chalinze ndiyo nile maandazi yangu.
Abira: ahaaaah.....
 
Kizibo: Halooo (akipiga simu kwa mwalimu wake)
Mwalimu: Haloo
Kizibo: Namwombea ruhusa Kizibo hawezi kufika shuleni leo
Mwalimu: Naongea na nani?
Kizibo: Unaongea na (baba yake!)

Hapo kwenye mabano alisema 'unaongea na baba'angu'
 
Kizibo: Halooo (akipiga simu kwa mwalimu wake)
Mwalimu: Haloo
Kizibo: Namwombea ruhusa Kizibo hawezi kufika shuleni leo
Mwalimu: Naongea na nani?
Kizibo: Unaongea na baba yake!


Hapa naona ingenichekesha kama alivyoulizwa naongea na nani? angejibu unaongea na: natania tu mwalimu, KIZIBO naongea.
 
Back
Top Bottom