Kizazi cha JKT kimeharibu nchi

Kuna mtu kama wewe aliwahi fanya research ya watu waliokuwa wanaendesha magari kisha yakapata ajali. Aliwauliza kama walipata breakfast au la. Conclusion yake ikawa wengi wa waliopata ajali walikuwa wamekula mikate. Akarecommend kuwa ili kupunguza ajali, watu wale viazi badala ya mikate.
Conclusion yako haina tofauti na mtafiti wa ajali na mikate!
mjukuu wangu jitahidi sana kuweka ujumbe wako katika hali ya kueleweka na uzee huu napata tabu kukuelewa.
 
Siamini kama JKT iinawajibika kusimamia tabia ya mtu baada kutoka kambini na kwenda ku-lead maisha yake mwenyewe.Kule unafundishwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu hasa kwa wanaokuzidi vyeo.So siku na wewe ukipata cheo hutarajii wa chini yako kuanza kuhoji unayoyafanya.Hiko ndicho kitokeacho sasa.Hakuna anyefikiri kuwa apaswa kuhojiwa kwa kuwa wote walifundishwa 'nidhamu ya hali ya juu'
ndio maana tunawasema vibaya vijana wetu,et ooh hawana adabu kisa wanahoji mambo hadharani bila kuogopa
 
kama kweli JKT ilifundisha ujasiri iweje leo hii watu kama kina rostam et al wanayumbisha nchi?naamini vijana wa leo ni majasiri kwani wanaweza kuipinga serikali waziwazi,wanaweza kuandamana pamoja na vitisho vya polisi nin.a uhakika huko tunapoelekea wataanza kujitoa muhanga.wanaotuangusha ni hawa wa wazee wenzangu wa JKT ambao wanakosa ujasiri wa kusema kodi ya madini iwe 50%

Kama wataweza kujitoa muhanga itakuwa ni kizazi chenye faida.Wazo lako siyo baya.
Kama mkuu mmoja amesema jkt ilisadia sana kuleta nidhamu.
Mfano mdogo kwenye daladala wazee wamesimama vijana wamekaa kwenye viti.
zamani hiyo huwezi ona,
 
Tupe list ya Upinzani ambao hawakupitia JKT.
..Nyie ambao hamkwenda JKT ndio hata kupiga kura hamtaki neno Uzalendo kwenu ni utamaduni ulopitwa na wakati.
Mkuu, angalia vizuri, watakwambia nyie ndo mnaipigia kura ccm kwasababu ndio kitu pekee mnachojua.
Wakati wenu ilikuwa kupigia kura CCM au kivuli.........you have got used to it!!

Uzalendo wa hawa ndugu waliokwenda JKT upo wapi?.........Walijenga taifa hili la kifisadi, walishindwa kusimamia mashirika ya uma, hata mashamba tu walishindwa............sasa uzalendo huu uzalendo gani??
 
Kama wataweza kujitoa muhanga itakuwa ni kizazi chenye faida.Wazo lako siyo baya.
Kama mkuu mmoja amesema jkt ilisadia sana kuleta nidhamu.
Mfano mdogo kwenye daladala wazee wamesimama vijana wamekaa kwenye viti.
zamani hiyo huwezi ona,
Nidhamu? Mkuu acha utani bana..........nidhamu ya mfano wako haikuwa instilled JKT, hiyo ilikuwa kazi ya society wakati huo.
Nidhamu tunayoitaka sisi ni nidhamu ya kutimiza wajibu..........ukipewa ukurugenzi wa SUKITA unakuwa mchapa kazi, mkweli, mwenye nidhamu ya hali ya juu na unayeipeleka SUKITA inapotakiwa...........Sio kumpisha mbabu kiti kwenye daladala!!!
 
Mi sijapitia JKT. Ingawa I wish ningekuwa nimepitia. Ila namshangaa huyo aliyepata conclusion ya utafiti wake kuwa ni vijana kutopitia JKT..! Kweli anafanana na mtafiti wa ajali na mikate.
 
Mkuu, angalia vizuri, watakwambia nyie ndo mnaipigia kura ccm kwasababu ndio kitu pekee mnachojua.
Wakati wenu ilikuwa kupigia kura CCM au kivuli.........you have got used to it!!

Uzalendo wa hawa ndugu waliokwenda JKT upo wapi?.........Walijenga taifa hili la kifisadi, walishindwa kusimamia mashirika ya uma, hata mashamba tu walishindwa............sasa uzalendo huu uzalendo gani??
Haaa haaa haa! chaguzi mbili zilizopita imeonyesha wazi Vijana wengi kati ya umri wa miaka 18 hadi 30 ndio hawakupiga kura.. Hawa wa miaka 30 walikuwa na umri wa miaka 7 wakati Nyerere anaondoka madarakani yaani darasa la kwanza, hivyo kama kuna walakin basi tuanzie huko.

Na kama ni swala la Viongozi wetu na wananchi wasiokuwa na Uzalendo nadhani kisayansi itakuwa bora zaidi kutazama hulka ya mwanadamu anapokuwa amefungiwa kwa muda mrefu ktk Ujamaa kama mnyama alofungwa kamba akila kwa urefu wa kamba yake. Siku akifunguliwa huwa na tabia gani?..Hivyo yawezekana kabisa ukweli umejikita katika itikadi ya UJAMAA na KUJITEGEMEA kuwalazimisha watu kuishi ktk mazingira fulani maanake hata watoto waliolelewa ktk gate kali siku wakipata Uhuru wa kufanya walitakalo bila usimamizi matokeo yake huharibikiwa zaidi. Hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba Ubepari umekuwa sababu ya watu kukosa Uzalendo kwani Money, Power and Fame ndio yamekuwa malengo ya kila Mdanganyika.

Na kama unabisha ebu tembelea EastAfricantube.com kwenye search andika - Mambo ya kumwaga radhi, kisha zitazame hizo video za hiki kizazi kipya - Majibu utayapata...
 
Baadhi ya waliopitia jkt: ra, riz1, ngeleja, makamba jr, masha, jeetu patel, lowasa jr, nape, nyalandu, mwigulu mchemba. Mnasemaje uzalendo wao?
 
JKT ilitumiwa kujenga nidhamu ya woga na kudhalilisha kina wakina mama na sio kujenga taifa kama wenye nidhamu ya woga wangependa tuamini
 
maudhi yanayoendelea hapa nchini kwa kiasi kikubwa yanafanywa au yamefanywa na wazee wetu ambao walipitia JKT.inashangaza kuona hawa wazee wenzangu wakilaumu vijana ati hawajapita jkt.walioko madarakani,watendaji serikalini na wapiga kura wazee ni mifano ya kizazi cha jkt.

kabla hatujaenda JKT kizazi chetu tayari kilikwishaharibika..........................JKT ni kusingizia tu na lengo ni kuficha ukweli....................kizazi chetu ni kiovu na hii ni laana kwa vizazi vijavyo labda mshtuke na mumtafute Muumba awaokoe lakini huko mwendako yaani jehanamu nafuu...........
 
Jkt haikuleta nidhamu, ila zama zenyewe ndizo zilizoruhusu hali ya kuwa na nidhamu.

Siku hizi hata watoto wakizaliwa na kukulia kambini bado nidhamu itakuwa chini kwakuwa zama haziruhusu.
 
Mkubwa jkt inafundisha uoga na utii wa lolote linaloamuriwa we angalia majeshi yote jinsi askari wetu walivyo na maisha duni huku viöngozi wao wakineemeka, wanaishi kwenye mabanda ya mbwa na wakilambishwa kama mshahara dun. Kwa kweli jkt ilikuwa inafundisha nidhamu ya woga we angalia jinsi wazee wanavyolalama ooh! Vijana hawana uzalendo kisa hawataki kuambiwa ukweli wanatamani waendelee kuiba, kutunyonya na watoto wao waishi vema. WATU WASIO NA SHUKRANI KWA TAIFA HILI WAUAJI WAKUBWA ETI VIJANA WAMEKOSA UZALENDO.... PTUU!!
Naamini kama kungekuwa na jkt mpaka leo,tungeweza kukomboa nchi yetu.
Jkt ilikuwa inafundisha ujasiri,na vijana wa leo hawana ujasiri.
iIli tuweze kuwa na mabaliko lazima tuende front,vijana wataweza?
ukiwaambie tuingie front watasema "hiyo ni kazi kubwa man au nita chafuka man.
Itawzekana vipi uingie front na suruali inaninginia kwenye magoti?
 
JKT ni jeshi la kujenga taifa sasa jiulize taifa letu limejengeka au ndio linaelekea kubomoka?

Mkuu, kwa hiyo kwa ufahamu wako, JKT ilikuwa inafunza ufisadi na moyo usio wa kizalendo? Crap!!! Jamani kama uwezo wenu wa kufikiri una kasoro, nyamazeni badala ya ku-generalize mambo. JKT was the a precious thing we have to regret loosing as a nation. Great nations like Nigeria, Israel etc,. still have it
 
Yaani kama kuna watu wameiharibu hii nchi ni wazee wa jkt ,walikosa ukakamavu wa akili.
 
Baadhi ya waliopitia jkt: ra, riz1, ngeleja, makamba jr, masha, jeetu patel, lowasa jr, nape, nyalandu, mwigulu mchemba. Mnasemaje uzalendo wao?

Nadhani aliyepita JKT hapo juu ni Ngeleja pengine na Nyalandu. Hao wengine sidhani. Nikiwa miongoni mwa waliopita JKT tunapaswa kukiri wazi kwamba wenzetu wengi wameiangusha nchi yetu. Wamekosa uzalendo na nidhamu ya kulinda mali ya umma.
 
Mkuu, kwa hiyo kwa ufahamu wako, JKT ilikuwa inafunza ufisadi na moyo usio wa kizalendo? Crap!!! Jamani kama uwezo wenu wa kufikiri una kasoro, nyamazeni badala ya ku-generalize mambo. JKT was the a precious thing we have to regret loosing as a nation. Great nations like Nigeria, Israel etc,. still have it
kwa akili yangu ya kizee naona JKT ilifunza ufisadi,uoga na unafiki na ndio maana leo hii viongozi wetu au tuseme sisi wazee tunahusishwa na ufisadi,uzembe,ulegelege,ushirikina,uoga na unafiki.leo hii tumerudi kule kule kwamba hakuna jambo zuri tunaweza kulifanya bila msaada wa wawekezaji ninavyoona kuna wakati utafika tutahitaji wawekezaji wa kutuzalishia wake zetu.kama kweli JKT iliundwa kwa kustawisha taifa nionyeshe matunda yake leo hii.inawezekana 'JKT' ya nigeria na israel zilifanikiwa katika malengo yake sidhani kama JKT yetu imetusaidia!sana sana imejenga mijitu mikorofi isiyojali binadamu wenzao.
 
Back
Top Bottom