Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Kuna haja ya kuwatafuta na kuwatwanga lisasi popote wanapoonekana?
aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha jamii (ccj) - almanusura niandike ccm! - richard kiyabo, leo "amerejea" na kukabidhiwa kadi rasmi na katibu mkuu, yusuf makamba.

Habari zilizotangazwa sasa hivi na taarifa ya habari kwa ufupi ya saa 10 jioni ya tbc1 zimetangaza.

Taarifa zitaendelea kuwafikia.
 
Hii ni conclusion tosha kwamba sio kila chama cha upizani ni cha upinzani kiukweli ukweli! Vingine ni mapandikizi kwa ajili ya kuharibu au kubadilisha hali ya hewa. Hakuna mtu anayeweza kuwa na utaahira kiasi hicho.... come on! Hii ni mbinu ya 'wale jamaa' wanajua wanachokifanya. Kiyabo? Infact hakuna chama kingine chochote kingeweza kumpokea.... amekwenda kuliko kwake (I mean that's where he belongs).
 
Kama una baba wa aina hii, ni vema kumuita mama yako faragha na kumuuliza "hivi kweli huyu ndio baba yangu?"
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) - almanusura niandike CCM! - Richard Kiyabo, leo "amerejea" na kukabidhiwa kadi rasmi na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Habari zilizotangazwa sasa hivi na Taarifa ya Habari kwa Ufupi ya saa 10 jioni ya TBC1 zimetangaza.

Taarifa zitaendelea kuwafikia.

Wanavyojitahidi kuwanunua, sijui ndio demokrasia gani hii
inakera sana, i hate CCM
 
Niliwahi kusema CCJ naikalia mbali kwani ilikuwa imenikalia vibaya na sikuwa naimani nayo sasa ona. mwenyekiti mwenyewe wa chama alikuwa mamluki sasa amerudi kundini. MMwanakijiji upo!!!
 
Duuh, hatimaye nimeamini kila shetani na mbuyu wake.Huku alikokwenda ndiko moyo wake ulipokuwa siku zote. Imagine mtu ungefanya papara kuamini kuwa kale kachama nacho kako serious....chama gani hicho ambacho kinategema kuondoka kwa vigogo wa CCM tu?? Wasipoondoka nacho kinakufa hapo hapo.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) - almanusura niandike CCM! - Richard Kiyabo, leo "amerejea" na kukabidhiwa kadi rasmi na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Habari zilizotangazwa sasa hivi na Taarifa ya Habari kwa Ufupi ya saa 10 jioni ya TBC1 zimetangaza.

Taarifa zitaendelea kuwafikia.

Jamaa anaitwa nani?
 
Na sisi JF hatunazo wakati mwingine. Kiongozi akitoka CCM tunashangilia, akirudi tunamponda. Wakati huo huo tukidai kujengwa demokrasia, sasa tunajengaje demokrasia bila kuheshimu haki za kidemokrasia? Nilizani utamu wa pilipili ni ukali wake?
 
Kisha mkuu wangu Mwanakijiji alikuja waamini watu hawa!....Na yuko wapi..

Mimi toka mwanzo niliamini kabisa kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa kuivunja nguvu Chadema kabla ya kampeni. Kuondoa hoja kubwa ya Ufisadi ambayo ndio ilitawala magazeti yote nchini na kwa kufanya hivyo walifanikiwa sana.
Huyu Richard Kiyabo kamaliza kazi yake na anarudi kambini. Hakuwa ametoka CCM hata siku moja na wajinga wengi waliamini kuwa CCJ ni chama kipya chenye mwelekeo.

Lakini pamoja na yote haya mimi na mashaka sana na Uwezo wa kufikiri wa Watanzania. Ni jana tu asilimia kubwa walikuwa wakilaani CCM na kutoa matusi yote ya mapungufu ya JK, leo hii wameshasahau au kusamehe, hao hao ndio wanaunga mkono chama hicho tena kwa nguvu zote...Kesho kilio tena!
Sijui ndio asili ya athari za Utumwa au Miafrika ndivyo Tulivyo!
 
Ukisikia mtu kuwa taahira na ZUZU, huu hapa uthibitisho!
Bora hata utaahira na uzuzu una unafuu. Hili lijamaa ni likichaa kabisa. Wala halijui linafanya nini? Mijitu kama hii ingekuwa nchi za wenzetu bila shaka ingepigwa risasi kabisa.
 
Nadhani alikosa nafasi ya jikoni CHADEMA ambapo walishamstukia na kumweka benchi.
Hongera zake kwa kudhihirisha UCHU wake hadharani


Huyo alutumwa kudhoofisha upinzani kwa kugawa wanachama ikiwemo chadema.Mpango huo aliotumwa na CCM wenyewe umeshindikana kwa hiyo amona hela za kampeni hazimfikii na kivyo arudi jikoni kabla kampeni hazijaisha.Na kweli jamaa amekonda hilo koti mhh...
 
Mimi toka mwanzo niliamini kabisa kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa kuivunja nguvu Chadema kabla ya kampeni.

Nikusahihishe mkuu; (lakini husiniombe data). CCJ ni chama kilichoanzishwa na mapapa wa ufisadi (EL, RA, V-g-sumni, & co) wakihofia matokeo ya kamati ya Mwinyi ambayo yangewavua uanachama. CCM wakagundua kwamba CCJ ingeisambaratisha CCM na hivyo wakayatupilia mbali matokeo ya kamati ya Mwinyi. Wafisadi walipoona wako salama ndani ya CCM wakavunja CCJ, na hivyo kumfanya mwanzilishi wa CCJ kubaki mdomo wazi mana hakujuwa alitumiwa kisiasa....sasa kaona kumbe if you can't beat them you may as well join join them.
 
MALAYA wa kisiasa huwa hatulii chama kimoja.
Naongelea wote ambao wanahamahama vyama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom