Kiwanja kinauzwa Kwembe - Kinondoni

KASRI

Member
May 2, 2009
93
22
Wana JF,
Nimetembelea eneo la Kwembe Kati wilayani Kinondoni Dar es Salaam kuonyeshwa kiwanja kinachouzwa ili nikinunue. Nimeonyeshwa eneo ambalo serikali imelipima na eneo walilohamishwa baadhi ya waliokuwa wamiliki. Eneo husika lipo nje ya mpango huo hivyo mmiliki wake ni halali (kwa mujibu wa mwenyeji wangu).

Ndugu zangu naomba endapo kuna mwenye taarifa zitakazonisaidia nisinunue "bomu" nitashukuru maana pesa zenyewe za mkopo.

Nawasilisha
 
Nenda Kwa mwenyekiti au katibu wa serikali za mitaa kufanya uhakiki wa kiwanja hicho, na ukitaka kuwa na uhakika zaidi nenda idara ya mipango miji utapata jibu lenye uhakika zaidi. Jirani au mwuzaji ni wafanyabiashara usije tumbukiza pesa zako chooni bure ukaja jutia kulikoni.
 
Toa taarifa zaidi ni karibu na wapi? point of reference muhimu hapa kwani ni kweli kuna vilivyopimwa na Serikali na kuna sehemu nyingine haijapimwa. Pia kuna eneo la Chuo kikuu Muhimbili hivyo mambo yote haya yanalifanya eneo hilo kukimbiliwa na wengi na pia matapeli kuliza watu. Usikubali hawa wajumbe wengi ni wa kuchonga.

Hivyo wewe nenda hapo peke yako halafu fanya utafiti mwenyewe bila huyo dalali / muuzaji na watu watakushauri. Waweza ni PM kwani nakaa huko na ni mmoja wa watu waliopo kwenye viwanja vilivyopimwa. Nimeshuhudia watu wakiuziwa maeneo yaliyolipwa tayari kwa kutofanya utafiti na baadaye kujilaumu. Hakikisha unauliza watu wenye nyumba pale wanaokaa na wala si vijana wanaolinda site kwani wanarubuniwa kirahisi
 
unasema Kwembe - Kigamboni ----- Then unasema Kwembe ipo Kinondoni. Mzee vipi? hebu eleza vizuri.
 
Lule navyojua mimi kiwanja cha 25 by 30 watakupiga- Tshs 12, - 15m. ukizubaa 20m kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom