Kiwanja Kigamboni Tuangoma

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
15,286
10,836
Wakuu,
Kuna mtu ameniletea dili la kiwanja kinauzwa huko Tuangoma Kigamboni. Kwa ninavyofahamu kigamboni inaleta mashaka sana hasa pale ambapo kiwanja hakijapimwa kwa kuwa mipango miji mingi inaelekea kule japo si maeneo yote yako katika mpango wa kupimwa. Kabla sijapoteza muda wangu kumchukua mtu wa manispaa Temeke apate coordinates za pale eneo (wanalipwa japo nauli) ninaomba kupata ushauri kama huu mji mpya wa Kigamboni unaishia wapi? Then kama haugusi Tuangoma then itanipa haja ya kuwaona sasa wataalam ili kupata uhakika wa matumizi ya eneo husika. Karibu kwa maoni. Asante.
 
Tuangoma ipo Kata ya Tuangoma, Mji mpya Unaishia Kata ya Mjimwema...Kwahiyo Haupo kabisa katika habari za Mji mpya.
Kwa maelezo zaidi nenda serekali ya Mtaa wa tuangoma utapata ufafanuzi wote. Karibu Kigamboni.
 
Asante sana mkuu kwa taarifa njema. Ngoja nitafute muda nimpeleke mtu wa ardhi manispaa anipe matumizi ya pale. Ni sehemu nzuri nimeipenda na eneo kubwa pia. Shukrani.
 
Kaka hata mimi nipo Tuangoma na karibu nahamia huko. Kibanda changu kimeshafikia mahala pazuri. Uzuri wa kule serikali za mitaa kidogo zinafanya kazi nzuri kwani mitaa iliyokuwepo huwa inapishwa grader kila mara na hivyo kufanya kuwa ngumu kwa mtu kuvamia sehemu ya njia. Binasfi sikwenda hata Halmashauri kufanya uhakiki ingawa natambua kuwa si sahihi so kama uko na muda wakutosha na uko na mtu ni bora ukafanya hivyo. Kutokana na mwenendo huu mzuri wa Serikali za Mitaa, tunaamini kuwa hata upimaji utakapokuja wataturasimishia tu eneo letu kwakutupatia hati kwani kazi ya serikali siyo kufukuza hata pale watu walipojenga kistaraabu na majengo yakileo bali ni kuwafikishia huduma zakijamii na maeneo hayo wameshapatiwa. Yapo hata maeneo ya wazi yanayotambulika na serikali za mitaa kule bwana. Tatizo kubwa ambalo mimi baada ya kupata eneo kule Tuangoma nimelipata ni kuwa wenyeji wa kule wameshatambua kuwa eneo lao ni Hot Cake (na hii inatokana na uzuri wa nyumba zinazojengwa kule kwani nymba nyingi zinazonjengwa kule katika maeneo yasiyopimwa ni design ya Mbezi Beach, Masaki, Mikocheni etc maana hakuna uchafu kule) so wapo mataperi wengi ambao huuza kiwanja kimoja zaidi ya mara moja kwa kutumia wenyeviti wa serikali za mitaa tofauti. Imetokea kwa jirani yangu mimi harafu imetokea pia kwa jamaa mmoja ambaye aliuziwa open space. Ukiongea vizuri na hao wenyeviti wa serikali za mitaa wanajuwa mengi sana kwani hata ramani wanazo. Jihadhari na hilo tu. Karibu sana Tuangoma. Otherwise, kama ulivyoshauriwa na Doltyne hapo juu, ukienda pale pale Mtaa wa Tuangona au hata pale Mtaa wa Malela utapewa maelezo yakuridhisha kabisa na unaweza usitamani hata kwenda Halmashauri. Wale jamaa siyo waswahili kama wa Mwananyamala.
 
Asante mno mkuu kwa maelezo fasaha kabisa. Ngoja nichangamkie tenda hii maana anayeniuzia ni mtu namfahamu ila pia nitaongea na hawa serikali za mtaa wanipe taarifa zaidi kama hakina mgogoro. Maana binadamu siku hizi hata unayemwamini anaweza kukugeuka tu.
 
njoo mi nikupe vilivyopimwa kabisa. nakupa hadi stage ya offer. then ww unamalizia kupata hati miliki mwenyewe.
 
Kaka vya kwako viko wapi wewe, ukubwa ? na bei gani? naomba details zaidi kaka.
 
njoo mi nikupe vilivyopimwa kabisa. nakupa hadi stage ya offer. then ww unamalizia kupata hati miliki mwenyewe.

Naomba utujuze hivo viwanja vipo maeneo gani,ukubwa gani na bei gani kama alivouliza mwenzangu hapojuu.
 
dooo! kazi kweli kweli mwaka jana nilikuwa juu ya mawe nikatangaza kuuza moja ya kiwanja changu huko twangoma majibu niliyopata yalikuwa balaaaa! mwingine anauliza ndo wapi huko? hivi huo ni mji lakini leo tunashukuru tunapata wenzetu walio tayari kununua hata visivyo pimwa karibuni sana!
 
Nalo ni wazo jema, asante sana. Sema bei, ukubwa na ili nikamilishe hati ninatakiwa kulipa kiasi gani cha fedha. Sina uzoefu na vya offer bali vya hati ambavyo unatakiwa kulipa kodi za manispaa/tranfer fees etc. Leta habari zaidi kimatangazo fasaha ya biashara.
 
dooo! kazi kweli kweli mwaka jana nilikuwa juu ya mawe nikatangaza kuuza moja ya kiwanja changu huko twangoma majibu niliyopata yalikuwa balaaaa! mwingine anauliza ndo wapi huko? hivi huo ni mji lakini leo tunashukuru tunapata wenzetu walio tayari kununua hata visivyo pimwa karibuni sana!

Mkuu mtu mwnye nia ya kununua ardhi ili mradi ipo sehemu nzuri hatakiwi kuuliza sana. Mimi hata kama eneo halijapimwa lakini naangalia mambo mengi, kama huduma, accessibility, hakuna uswahili n.k. Mdau hapo juu amesifia serikali ya mtaa Tuangoma wamepanga sana mitaa yao japo hakujapimwa kwa hiyo siyo tabu sana. Upimaji nitagharamia mwenyewe nikishapata master plan ya pale tu maana najua kwa kigamboni ipo. Mambo ya kusubiri kukanyagana maboya ya viwanja vya hongo vya manispaa ni bora ununue eneo lako upime ni uhakika zaidi.
 
Naomba utujuze hivo viwanja vipo maeneo gani,ukubwa gani na bei gani kama alivouliza mwenzangu hapojuu.

Viko huko MWANZO MGUMU . bei negotiable ila kuanzia 8m ukubwa kuanzia 550sqm- 650sqm zaidi ya hizo sqm tunauziana kwa Tsh 8000@sqm
 
Asante mkuu kwa taarifa. Wengi nami nikiwemo hatujui sana maeneo ya Kigamboni. Je unaweza kuelezea vizuri Mwango Mgumu interms of umbali toka Feri, huduma za jamii hasa umeme maana maji nina shaka kama yapo labda uchimbe kisima, inapakana na nini kwa maeneo maarufu kigamboni say Mji Mwema, Tuangoma, Gezaulole etc. Na pia kama ni vile vya kupimwa na serikali au ni mtu amepima eneo lake kwa kibali cha manispaa ect. Hii itasaidia kupata picha.
 
Mwanzo Mgumu ni baada ya Gezaulole unaacha njia ya Tuangoma kwenda huko ni rami then unaacha rami barabara zipo zimechongwa. ni maeneo ya mtu yamepimwa sio vya manispaa. known area karibu na kwa Sofia simba area. SIMANGIRA AREA
 
Ok. tumekupata asante.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom