Kiwango cha kufaulu kushuka 2013

Jul 29, 2012
52
4
Jamani nina hisi wanafunzi wengi watafeli sana mwakani. Kwa kuanzia kudodosoa nianze na hawa wa kidato cha pili wengi hawana sifa za kuwepo katika kidato hicho kwasababu zifuatazo, wengi hawana uwezo wa kusoma au kuelewa lugha ya kiingereza. Wengi wao hawawezi kuumba herufi yani hata neno likaeleweka. Pia Mihula ya mwaka huu Imetawaliwa na likizo za hapa na pale, shughuli za sensa kupelekea walimu wengi kutomaliza sylabus kwa muda muafaka. Kwa asilimia kubwa wanafunzi hawaja pewa elimu ya kutosha kujibu mitihan yao kutokana na Mgomo wa walimu ulioanza toka kipindi chini kwa chini. Kunamapungufu nimeyaona katika baadhi ya shule, utayar wa waalimu kutoa material kwa wanafunzi umekuwa dhaifu kutokana na haliduni ya hawa walimu wetu kutothaminiwa na utayari wa wanafunzi wenyewe katika usomaji ambapo wengi wamebweteka sana na kukata tamaa. Serikali inabidi itazame upya suala la kuboresha vitendea kazi mashuleni. Kuna wakati serikali itakosa wasomi wenye sifa kwa kufumbia macho mkanganyiko huu. Naishahuri serikali ifanye mtazamio upya wa Tanzania yetu kwa miaka ya sasa hadi mingineyo kwa kipindi cha miaka 50 baadae, kwamba walifanyalo sasa kwa manufaa ya wakati ujao kwa ajili ya kumkomboa mwalimu na kuikomboa nchi katika misingi ya elimu kama nyenzo kuu ya taifa. Na ikilitafakari hili jambo kisiasa kwa miaka mitano mitano ya uongozi hakutakuwa na maendeleo katika suala la elimu maana itabaki ni MADESA tu, bali kutakuwa na uozo ndani ya taifa kwa watu wasioelewa kuchambua na kupembua mikataba, ufisadi wa fedha za walipa kodi na uchukuaji wa rushwa na kuchakachua baadhi ya masuala. Na kupata msiba na majanga ya kuhujumu uchumi na mengineyo. Tujipange jamani!
 
Back
Top Bottom