Jumamosi wiki iliyopita nilikuwa bored kukaa nyumbani nikaona nitembee kwenye countryside, nikaishia kwenye shamba la miwa la Dizungu ambalo sina wasiwasi wowote kwamba ni shamba la Rais wa awamu ya nne aliyestahafu Benjamin William Mkapa.Shamba hili baada ya kuuliza wenyeji wangu, waliniambia kwamba Mkapa alilinunua kwa Mhindi moja ambaye jina nimelisahau.Nadhani hii ni moja ya biashara zake alizofanya akiwa Ikulu!Shamba hili nimeambiwa lina takriban hekta 900.Ni shamba linalotunzwa vizuri.Katia maongezi yetu na jirani zangu, nilitaka kujua mambo mengi.Hata hivyo jambo lililonigusa sana, ni pale mmoja wa wenyeji wangu ambaye ni mfanyakazi wa shamba la Dizungu ambalo ni shamba la Mkapa,alipolalamika kwamba wananchi wa Tanzania tunaibiwa sana.Nilipomuuliza kwa vipi,aliniambia kwamba shamba la Mtibwa ni mali ya Mkapa!Nilipomuambia anipe ushahidi wa kuthibitisha usemi wake,alisema ushahidi upo,nao ni kwamba mishahara yote inatoka Mtibwa,na hata Meneja wa shamba la Dizungu yupo Mtibwa.Alisema kila siku ya malipo,iwe katikati ya mwezi au mwishoni,bwana fedha anatoka Mtibwa kuja kuwalipa.Aliendelea kuniambia kwamba Shamba la Dizungu lina Headman tu, ambaye yuko chini ya Meneja wa Mtibwa.Ushahidi huu ulikuwa so convincing to me,hasa nikizingatia kwamba kumekuwa na minong'ono mingi kuhusu nani hasa analimiliki shamba la Mtibwa.My conclusion is,kama shamba la Mtibwa sio la Mkapa, basi upo uhusiano usiofaa kati yake na kampuni ya Mtibwa.Jee,huu ni ufisadi mwingine?