Kiwanda cha Kutengeneza Maji

wimbi la mbele

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
647
266
Forum nzuri hiii.

Nauliza, mfano nataka nifungue kiwanda cha maji, yaani kufunga mashine mpya, madumu ya maji etc, bora ni ninunue mashine wapi? Mpya za China au used za ulaya?

Je, kuna websites naweza kutembelea kuona kama naweza kupata mashine hizi?

Je chupa itakuwaje?
 
Duuuu set nzima itakugharimu kama sh 100m hivi. Investment yake imesimama kidogo....hapo badp space na nyumba ya uzalishaji....machine zipo china ndio bei rahisi...machine 5 zinatakiwa ili uwe fit zaidi......

Nakushauri kama unataka urahisi zaidi nenda kwa kiwanda cha A1 kinatengeneza maji ya MO Dewji..utapata nembo yako na utatengenezewa maji yako uyapelekee...sokoni
 
TZS 250m bado kiasi kidogo kama unataka kuanzisha kiwanda cha maji kwa ajili ya biashara.

Kuanzisha kiwanda cha maji unahitaji kuwa na aina nne za machine ambazo ni mashine ya kusafishia maji, mashine ya kutengenezea chupa za maji, mashine ya kuwekea maji kwenye chupa na mashine ya kuwekea label. Gharama ya mashine (complete set and / with accessories) ex China au India au Taiwan hadi Dar-es-salaam pamoja na kodi ni kiasi cha TZS 355m.

Mashine ya kusafishia maji (water purifying mashine) = 50m
Mashine ya kutengenezea chupa za maji (bottle manufacturing machine) = 70m
Mashine ya kuwekea maji kwenye chupa (purified water bottling machine) = 50m
Mashine ya kuwekea label (labelling machine) = 7m
Usafiri na bima (freight & insurance) = 35m
Kodi (tax 67%) = 142m

Hapo bado hujajumlisha gharama za kununulia au kukodisha eneo la kuweka kiwanda, malighafi, wafanyakazi / vibarua, gharama za kuendesha mitambo, gharama za maji na umeme, gharama za kujitangaza, usafiri na kadhalika.

Start up cost ni kama TZS 500m, kwa kubana sana.
 
wasikutishe mpendwa. ukitoa gharama za banda na van, kama utaanza na chupa ndogondogo itabidi uwe na angalau dola 40,000 za kuanzia kwa mshine pekee, lakini kama ni chupa kubwa, hata dola 15,000 utapata mashine za kuanzia. na unaweza kuendelea kuexpand kidogokidogo hadi kufikia scale unayotaka. kwa kuwa umesema una 200m+ unaweza kuanza na chupa za ujazo mbalimbali. kuna mtu tumeishamsaidia na sasa kiwanda kinafanya kazi tayari, so we have practical experience. mashine tulinunua china. za ulaya hazikuwa na advantage, kuna mambo mengi oinabidi ufanye kama kupima aina ya maji kutoka kwenye chanzo chako (water analysis) na uwe na laboratory report ambayo itakuongoza kujua mitambo yako iwe ya technolojia gani nk pia ni vizuri mambo ya tbs na tfda uyazingatie. kuna mengi hapo ndugu. best wishez
 
Wakuu, nimefanya intensive research kuhusu kiwanda ya kutengeneza maji ya kopo na kusindika Juice. Nimeshaandika business proposal na nimeshafanya simulation kwenye mambo ya finance.

Sasa nataka kujua guideline (muongozo) wa kupata vibali vyote muhimu. Kama kuna mtu anafahamu muongozo huo tafadhali nitumie msg.

Kama kuna mtu anataka kujua gharama za kuanzisha kiwanda, nini kinaitajika uliza tuu.
 
Natamani kujua mkuu! 7bu tukiwa na Viwanda vingi vyakucndika hasa Matunda itasaidia kumuinua hata MKULIMA mdogo! so cmbaya kumwaga taarifa hapa Kiongozi
 
Mtanganyika

This is a very good idea

My advice is, ungetengeneza full package ya jinsi ya kuanzisha hii biashara including a bankable business plan, pre project procedures, plant and machinery sourcing (processing & packaging), business finance opportunities and a sound brand name halafu ukawa unauza business rights za package yote (sort of franchise), hivyo basi wale wote watakaokua wanataka kuanzisha wanatafuta strategic specific market locations .... kila atakaeanzisha awe na market area yake in terms of zones all over Tanzania ... hakutakuwa na muingiliano wa masoko kijiografia na brand ni ile ile

I hope this can workout
 
Last edited by a moderator:
Kwanini Lady Jaydee alizimwa biashara hyo? Ebu wasiliana naye Facebook akupe chanzo ili uweze kujua maana hawa TFDA washawekwa mifukoni..
 
Kwanini Lady Jaydee alizimwa biashara hyo? Ebu wasiliana naye Facebook akupe chanzo ili uweze kujua maana hawa TFDA washawekwa mifukoni..
Maji na Juice hauwezi kupata kibali kwa urahisi hasa kama soko lako unaanzia Dar,TFDA tbs etc watahakikisha vigezo vyote na vya ziada unatekeleza.kuna Azam,Dasani,Sayona watahakikisha soko la Dar haliongezewi ushindani,na soko la Dar ndio soko kubwa na muhimu ktk biashara hiyo
 
Kwanini Lady Jaydee alizimwa biashara hyo? Ebu wasiliana naye Facebook akupe chanzo ili uweze kujua maana hawa TFDA washawekwa mifukoni..

lady jaydee hakuwa na kiwanda cha maji bali kuna kampun ilikuwa inatumia jina la lady jaydee kwenye maji na walimlipa kutumia jina lake
 
Hongera sana viwanda vidogo ndio ukombozi I think unahitaji kwanza kuregister kampuni brela , pata leseni pale wizara ya viwanda , tin Tra , register mradi wako pale tanzania investment centre ( naamini ni zaidi ya dola 100,000) ungeweza share na sisi cost na nini kimehitajika ingekuwa elimu nzuri ila mwisho Kabisa unatakiwa uonane na tfda na tbs lazima wanahusika wengine wataongezea
 
Wakuu, nimefanya intensive research kuhusu kiwanda ya kutengeneza maji ya kopo na kusindika Juice. Nimeshaandika business proposal na nimeshafanya simulation kwenye mambo ya finance.

Sasa nataka kujua guideline (muongozo) wa kupata vibali vyote muhimu. Kama kuna mtu anafahamu muongozo huo tafadhali nitumie msg.

Kama kuna mtu anataka kujua gharama za kuanzisha kiwanda, nini kinaitajika uliza tuu.
Hongera mkuu, hata na idea hiyo. Niko kwenye kufanya utafiti na kuandaa business plan.tunaweza share some issues.kuhusu vibali nenda TFDA watakupa guidelines yao inauzwa elfu tano na map ya kiwanda watakupa na fomu pia.kisha ukienda TBS omba kuingia libary wakuprintie document ya juice kwa matunda unayotaka na catalogy ya maji.pia kingine ni Brela ukasajili jina na kampuni na TRA for TIN.
 
Wakuu, nimefanya intensive research kuhusu kiwanda ya kutengeneza maji ya kopo na kusindika Juice. Nimeshaandika business proposal na nimeshafanya simulation kwenye mambo ya finance.

Sasa nataka kujua guideline (muongozo) wa kupata vibali vyote muhimu. Kama kuna mtu anafahamu muongozo huo tafadhali nitumie msg.

Kama kuna mtu anataka kujua gharama za kuanzisha kiwanda, nini kinaitajika uliza tuu.

Mkuu heshima mbele,

mi mwenyewe nimekuwa nadream sana hii biashara ya maji,tafadhali naomba kujua gharama yake kwa ujumla,au kama una proposal please share,we can exchange ideas on how to start.
 
Maji na Juice hauwezi kupata kibali kwa urahisi hasa kama soko lako unaanzia Dar,TFDA tbs etc watahakikisha vigezo vyote na vya ziada unatekeleza.kuna Azam,Dasani,Sayona watahakikisha soko la Dar haliongezewi ushindani,na soko la Dar ndio soko kubwa na muhimu ktk biashara hiyo

that dude id dead, right?

never heard it in the market nowadays!!
 
Back
Top Bottom