Kiwanda cha kuassemble magari Tanzania...kitarudi kweli?

sasa wewe bwabwa au punga kwa jina lingine, tatizo lako ninini hata ukashifu hivyo? nilitoa wazo, kama basi tulishindwa yale ya nyumbu, basi hata kufanya joint partnership Toyota au HOnda etc waje waweke plant yao hapa si haba, wewe ungetoa wazo la aina hiyo ili hata kama hatutakuwa na branch yetu baasi tuwe na kiwanda walau cha kuassemble magari kama wanavyofanya south africa na kwingine....utasemaje nakoroma kwa kisiasa wakati nia yangu kuongelea hili sikuwa na nia mbaya, wewe unakuja kuongea kama unatoka kutafunwa kipunga..vipi wewe? kila kitu kwako ni siasa? hata tigo yako unaweza kusema ni ya kisiasa...eheee.

Jamani mbona mna lugha kali hivi duh
 
Jamaniee, Mungu atupe nini sisi watz? Kule Liganga kuna chuma ambayo tutaweza kuchimba kwa miaka hata mia, kule mchuchuma na mbinga kuna makaa ya mawe tunayoweza kuchimba kwa muda wa miaka hamsini. tunayo bahari kuingizia mashine na vito vinginge tusivyonavyo. makaa ya mawe kutengeneza umeme mwingi. gesi kutengeneza umeme na matumizi ya ndani. mafuta nayo kuna uwezekano mkubwa kuwepo.

zamani tulikuwa na kiwanda cha kuassemble magari kule kibaha(NYUMBU), si mnakumbuka magari ya nyumbu jamani? kiwanda kile kilikufa kifo cha mende(mende akifa kimgongo asipolalia kifua anaweza akaozea hapohapo). what makes us tzs kutokuhimiza kiwanda kipya cha magari hapa jamani? wakati chuma tunayo ya kumwaga. uranium kama ni kutengeneza umeme etc tunayo ya kumwaga hapa(in mbinga and around lake nyasa). wakenya wana assemble magari tayari, na sisi tunang'a macho tu. wakenya wangekuwa na resources hizi, wangekuwa mbali sana.

kama kuna kiongozi aliyeshika rungu humu(mimi sijashika rungu ndo maana sauti au impact yangu haiwezi kuwa kubwa kama ile ya watu tuliowapa dhamana), huko china,uturuki,japan etc mnakopeleka wanafunzi, basi pelekeni wanafunzi kwenye mambo ya technologia, ili wakirudi tuanzishe vitu vyetu.

Kuna kijana mmoja kule kanda ya ziwa alisoma Japan, akafanya field kule kwenye kampuni ya kutengeneza boat, kwasasa amerudi hapa bongo, anatengeneza boti nzuri na za kisasa kule ziwa victoria sana. yaani very good ship builder aisee. nina uchungu sana na nchi yangu kwakweli.
Utaambiwa uranium tuliyonayo haifai kwa matumizi ya yoyote kwamaana kwaliti ni ndogo ( refer Machungwa ya Tanga). Chuma cha liganga hakifai kwa matumizi ya viwanda kwamaana kinateleza sana, makaa ya mawe ya mchuchuma hayafai kwa umeme kwamaana ni meusi sana( yataleta giza yakichomwa). Gesi ya songosongo haifai kwa matumizi ya nyumbani kwa maana inanuka sana.
 
Tuwe wakweli tutaweza kutengeneza gari ambayo inaweza kushindana na haya tunayoagiza kutoka nje?
Katika bei na katika ubora? Toyota inatumia Dolla milioni moja KWA SAA!!
Kwa ajili ya Research & Development, je serikali yetu hata ikitumia 10% ya hiyo hatutalalamika humu kuwa wanapoteza hela ambayo ingiweza kutumika vizuri zaidi?

Biashara ya kutengeneza magari ni ngumu sana, waangalie wamarekani kampuni karibia zote zilibidi ziokolewe na serikali la sivyo zingefilisika.
 
Gari zisizo weza pandisha mlima nani atanunua? jibu ni easy lazima kife
 
Back
Top Bottom