Kivuko cha MV Magogoni chapoteza mwelekeo, abiria wajitosa majini

Wakifa watu ndo tutajua kweli ni suala serious tutalitatua, vinginevyo ni porojo za watu tu.
Kivuko tumeleta kipyaaa
Nahodha mpyaaaa
Maboya mapyaaa
Jaman watanzania wenzang, wapuuzeni hawa watu.
Hapa kazi tu
 
Kivuko ndio kilikua kinaondoka kigamboni, kivuko kikubwa kilikuwa kibovu hivyo kilibakia kile kidogo tu na muda huo wa asubuhi watu ni wengi sana.
kilichotokea kivuko kidogo kilivyofika watu wakaanza kuingia kwenye kivuko, dereva wa pantoni alivyoona kivuko kimejaa na watu wanaendelea kuingia, akaamua kuondoa kivuko bila ya kutoa taadhali yoyote aidha kupiga honi au kutoa matangazo. wakati ametoa ule mlango aliuinua juu, sasa lilivyosogea na watu wengi bado wapo mlangoni ulizidiwa mlango ukashuka watu ndio wakaingia majini, vilio vikatawala na taharuki kubwa ikatokea! Cha ajabu yeye aliendelea na safari watu ikabidi wasukumane kuelekea ndani kujinusuru na ndio ikawa salama kwao.
pamoja na vivuko vibovu lakini dereva wa leo alifanya kosa kubwa sana la kucheza na maisha ya watu. wahusika wamchulie hatua kali
Na angawaachia mjazane hadi kivuko kuzidiwa na kuzama mngeleta lawama. ifike mahali watz wajali uhai wao sio watu wana behave kama wanyama,mnajua kabisa kivuko kidogo mnataka muende wote kwa wakati mmoja,mmezoea hivyo kwenye daladala na mabasi ya mikoani likipata ajali mnamlaumu dereva kwa kuwajaza kama mahindi kwenye gunia, hamjitambui??!!
 
Hapo siku zote ndio utagundua.

Kwenye ajali wengi wanaoumia au kupoteza maisha, mara nyingi ni wale wanaohamaki.

Chombo kimepoteza muelekeo, wengine hata kuogelea hawajawahi/hawawezi wanajitosa.

Sasa hapo unategemea nini?
 
tatizo watu wanasogeaga mbele kikikaribia kufika so uzito na COE vinahama na engine hazina nguvu wakati mwingine iko moja so lazma kipoteze mwelekeo,,wakati mwingine mwendeshaji anawalowesha makusudi kuwasogeza nyuma
so,so,so ndio nini sasa hiki ,kwani ukitumia Kiswahili hutaeleweka
 
nakumbuka jamaa yangu aliniambia kujenga kigamboni ni sawa na kujenga kwenye hifadhi ya barabara,na sasa naona kigamboni ni eneo hatarishi kuliko hata jangwani
unapajua kigamboni lakini, nikusaidie tu, kwa d'salaam hiyo ni "one of the best place to reside ever
 
Mida mingine paniki ndip inaua watu, sasa hapo kulikuwa na haja gani ya kupaniki, mbona kipo ktk gati kabisa?
 
Ila mbona sijaona jitihada za watu walio juu wakijiokoa?mfano kufungua hayo maboya yaliyo hapo juu.au kuvaa life jackets kama zipo??
 
Kivuko cha MV Magogoni kupata hitirafu, kumepoteza mwelekeo na kuacha njia yake hali ilozua taharuki kwa abiria.

Vilio na kelele zilisikika pale maji yalipoanza kupanda ndani ya kivuko.

Hali hiyo ilisababisha abiria waanze kujitosa ndani ya maji kwa wale wanaojua kuogelea. Hakika watu wa Kigamboni wanatembea roho mkononi.

Poleni kwa wote Mliofikwa na mkasa huu
View attachment 322468 View attachment 322469 View attachment 322470
Serikali Iwasaidie watu wa Kigamboni, hii si mara ya kwanza, mara nyingi huwa wanasaidiwa na Wanajeshi(Jeshi la majini la pale Kigamboni.

Serikali ilinunua Kivuko cha Kwenda Bagamoyo wakati hapa Dar tu tabu.

Natumia nafasi hii Kuwaomba wanajeshi wetu waende pale kigamboni kutoa msaada kwani leo abiria ni wengi na wengine hawajui watavuka saa ngapi.
View attachment 322475 View attachment 322476

==================

Updates;

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile, alishamwandikia barua, Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu hili titizo. Haya hapa chini ni Maelezo yake ambayo ameyaweka kwenye hii thread.

Bonyeza hapa
Mpaka watu wazame kwenye maji na kufa huyo Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ndio atachukuwa hatuwa. yaani hiyo nchi yetu inaongozwa na Viongozi wasanii kweli ni hatari sana mtu kuishi Kigamboni unahatarisha usalama wako poleni sana Mliopatwa na mkasa wa kutaka kivuko kizame.
 
Back
Top Bottom