Njiku Julius
New Member
- Jan 22, 2016
- 1
- 0
Inabidi wizara husika na wenye mamlaka wawajibike kutatua tatizo hili kwa kweli
Mimi sikuwepo.nini kilitokea hasa? ina maana kivuko kilikuwa overloaded mpaka mlango ukataka kuzama au? ila mara nyingi nikiangalia tabia za abiria wa pantoni nashangaa sana.
nakumbuka jamaa yangu aliniambia kujenga kigamboni ni sawa na kujenga kwenye hifadhi ya barabara,na sasa naona kigamboni ni eneo hatarishi kuliko hata jangwani
Ok.............Mimi sikuwepo.
Lakini sijawahi kuona ferry imeanza kuondoka na watu mlangoni hivyo . Tunakagaaga masaa kusubiri watu wasukumane sukumane wengine waamue kushuka.
Naona leo captain aliamua awaonyeshe
Mkuu huyo alikuwa anamkashifu kikwetu kwa kujenga daraja lisilokuwa na maana yoyote na sio magufuliKuna jamaa humu JF alidai daraja la kigamboni halina. maana!hii nchi ni mabingwa wa kukosoa juhudi za serikali za JPM!
Ni hatari sana hii, ingekuwa katikati ya bahari si ni balaa.
Kivuko cha MV Magogoni kupata hitirafu, kumepoteza mwelekeo na kuacha njia yake hali ilozua taharuki kwa abiria.
Vilio na kelele zilisikika pale maji yalipoanza kupanda ndani ya kivuko.
Hali hiyo ilisababisha abiria waanze kujitosa ndani ya maji kwa wale wanaojua kuogelea. Hakika watu wa Kigamboni wanatembea roho mkononi.
Poleni kwa wote Mliofikwa na mkasa huu
View attachment 322468 View attachment 322469 View attachment 322470
Serikali Iwasaidie watu wa Kigamboni, hii si mara ya kwanza, mara nyingi huwa wanasaidiwa na Wanajeshi(Jeshi la majini la pale Kigamboni.
Serikali ilinunua Kivuko cha Kwenda Bagamoyo wakati hapa Dar tu tabu.
Natumia nafasi hii Kuwaomba wanajeshi wetu waende pale kigamboni kutoa msaada kwani leo abiria ni wengi na wengine hawajui watavuka saa ngapi.
View attachment 322475 View attachment 322476
==================
Updates;
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile, alishamwandikia barua, Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu hili titizo. Haya hapa chini ni Maelezo yake ambayo ameyaweka kwenye hii thread.
Bonyeza hapa
Hiko kivuko kilisumbua tangu asubuhi. Fundi alizamia akidai kuondoa uchafu hata hivyo engine ilisua sua sanaNikiwa ni mmoja kati ya watu walio shuhudia tukio hili la leo alhamisi asubui tarehe 11/02/2016 tukio lililo tokea kwa uzembe wa utawala na uongozi wa vivuko vya kigamboni.
Nikiwa mmoja wa mwathiliwa nimeshuhudia dhaili kuwa dereva akiforce kuondoa kivuko pasipo utalatibu wala ishara na kuwafanya watu nusura wazame katika maji,
tunaomba selikari iboreshe huduma za vivuko na kuwafukuza watumishi wasio waadilifu na wasio jari maisha ya watanzania wenzao na kukosa uelewa wa kuona nini hatima yake kwa mazoea haya ya kutokujari abiria wanapo panda vivuko hivyo ikiwemo wakina mama,watoto wa shule,wazee vijana na wengine ni walemavu.
sio busara kabisa watu waje kufa katika maji alafu ndio tusikie mnafanya jitiada za kuboresha vivuko huo utakuwa ni unafiki.huduma ni mbovu acheni siasa katika sehemu hatalishi zilizo zungukwa na maji yenye kina kilefu hizi ni roho za watu.
View attachment 322512 View attachment 322511 View attachment 322510
kabisa mamalile daraja liishe tu aisee