Kivuko cha mto Kilombero na ahadi za serikali

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
wana JF jana nimepata bahati ya kutembelea mjini ifakara, nikaona nisiishie hapo nikafika hadi mtoni kilombero ambapo ni mpaka wa kilombero na ulanga, ila kwa kweli hali ya kivuko sio nzuri sana, ukiangalia hiki kivuko Mv Kilombero II hata kama hakina mtu kinaonyesha dalili ya kuzama, nimewaletea picha hizo hapo wadau mjionee

5905d1252610759-ujenzi-wa-daraja-mto-kilombero-kuanza-oktoba-mv-kilombero.jpg

5906d1252610759-ujenzi-wa-daraja-mto-kilombero-kuanza-oktoba-mv-kilombero_1.jpg
 
Attachments

  • Mv Kilombero.jpg
    Mv Kilombero.jpg
    19.9 KB · Views: 156
  • Mv Kilombero_1.jpg
    Mv Kilombero_1.jpg
    38.4 KB · Views: 139
Loh! kinafanya kazi kweli? Mbona picha ya pili naona kama kimekua dumped.? Hivi nauli ya kuvuka kwa kivuko hiki siku hizi bei gani?
 
Asante kwa kutuonyesha hali halisi. Kawambwa jamani, tena Mechanical Engineer unakubali kuweka rehani maisha ya watu namna hiyo?? Hicho ndo kivuko tuliambiwa kimegharimu milioni 600? Hapo lazima kuna rushwa tu?? mbona huo mto daraja linaweza kujengwa? tena kwa pesa zetu wenyewe? Serilaki ya CCM humna priorities? au mnadhani nchi inaendelea kwa nyinyi mawaziri na wabunge kuwa na magari ya kifahari?
 
Kikwete akimnadi Selina Kombani 2005 ilikuwa ni moja za ahadi kujenga daraja pale, na hata kwenye ziara ya 2008 JK alisema kuwa uhakiki na upembuzi yakinifu wa kujenga daraja kwenye mto Kilombero unaounganika Wilaya ya Kilombero na Ulanga umeishafanyika. Naona 2010 iko ukingoni sijui atakuja na hadithi gani tena Muungwana na CCM, usanii tu Big tyme!
 
nilisoma Kwiro, nilipata kuwa abiria kwenye vivuko vya mto huo, ukweli ni kua moja ya agenda muhimu ya wakazi hasa wa Ulanga mashariki au magharibi tangu enzi za marehemu Itatiro, ni kuwekwa daraja katika mto huo......miaka ya tisini kulikua na agenda ya umeme, wakadanya sana watu, sasa ahadi ni ujenzi wa daraja, bahati mbaya wakazi wengi wa wilaya ya ulanga wanadanganyika kirahisi, atawapa kura watawala wa hovyo ambao hawatimizi ahadi zao.
Asante kwa picha hizo....kifupi ni kielelezo cha watawala wasiojali.
 
Asante kwa kutuonyesha hali halisi. Kawambwa jamani, tena Mechanical Engineer unakubali kuweka rehani maisha ya watu namna hiyo?? Hicho ndo kivuko tuliambiwa kimegharimu milioni 600? Hapo lazima kuna rushwa tu?? mbona huo mto daraja linaweza kujengwa? tena kwa pesa zetu wenyewe? Serilaki ya CCM humna priorities? au mnadhani nchi inaendelea kwa nyinyi mawaziri na wabunge kuwa na magari ya kifahari?

tena JK alisema katika ilani ya CCM ni kujenga daraja mto kilombero..we are almost 17 months to go kufikia uchaguzi na sijui kama hilo litawezekana.Lakini mwenyewe kasema juzi kuwa ahadi zote zitatekelezeka...
 
Subira haina neno ila tusubiri hadi lini? Nilifanya biashara ya rubi kule maeneo ya Epanko hadi Lukandi. Hali ni ya ovyo ovyo tu!
 
Kuna mambo ambayo kuyachezea ni kucheza na uhai wa watu.Mahali hapa yaani mto Kilombero wamekufa watu wengi kwa ajili ya pantoon hii.Mtakumbuka mwaka 2000 Fredirick Sumaye akiwa Waziri Mkuu alienda pale kuzindua pantoni baada ya iliyokuwepo kuuwa watu wengi tu,Alisema ufumbuzi wa wa pale ni daraja.Akaja JK AKATUAMBIA UPEMBUZI YAKINIFU UMEKWISHA FANYA ni michoro na kupata wafadhili.Najua awamu hii ikipita basi ajaye atakuja na vimbwanga vyake pia.Safari hii atasema tutaweka helicopta ya kuwavusha wananchi.Poleni watu wa Kilombero na Mahenge.Kwani,Itatiro alipewa kazi ikamshinda,akaja Ngasongwa naye akababaishia ,Walau Celina Kombani amejitahidi kulisukuma hili lakini ndo hivyo tena halisogeiiii CCM kura watachukua daraja wala kivuko itabakia kuwa ndoto ya alasiri tu.
 
Tuweke CCM HQ Ifakara na wafanyakazi wao wote waishi upande wa Ulanga ndipo utakapoona kwamba Daraja la pale ni so cheap, na ujenzi wake utaenda chap chap!
 
Ujenzi wa daraja Mto Kilombero kuanza Oktoba
Na Samuel Msuya,Morogoro

UJENZI wa daraja la Mto Kilombero linalounganisha Wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, utaanza mara baada ya kampuni inayofanya usanifu, kukamilisha kazi yake Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Morogoro,Charles Madinda alisema kazi za usanifu wa daraja hilo, inafanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Nimeta ya Dar es Salaam na Kampuni ya Howard Humphrey ya Kenya.

Kwa mujibu wa Madinda kazi hiyo iko katika hatua ya mwisho na inatarajiwa kuwa ifikapo Oktoba, itakuwa imekamilika .

Alisema ya kusanifu daraja hiyo, itagharimu kiasi cha Sh300 milioni na kwamba kazi hiyo ndiyo itakayobainisha gharama za mradi huo.

Meneja huyo alisema pamoja na kuweka nguvu katika ujenzi wa daraja hilo, serikali pia mbioni kufungua barabara inayounganisha Mkoa wa Morogoro na Ruvuma, kupitia Lupilo,Malinyi hadi kijiji cha Kitunda, wilayani Namtumbo.

Meneja huyo alisema tayari Tanroads imeshakamilisha ujenzi wa daraja la Mto Fuluwa wakati ikiendelea na ujenzi wa daraja la Mto Mwatisi, ikiwa ni sehemu ya mkakati huo.

Alisema hatua pia zimechukuliwa kusafisha barabara kutoka Kilosa kwa Mpepo hadi Londo mpakani mwa Morogoro na Ruvuma.

Kukamilika kwa daraja la Mto Kilombero kwa kiasi kikubwa, kutawaondolea adha ya usafiri wananchi wa Wilaya ya Kilombero na Ulanga, ambao kwa miaka mingi sasa, wamekuwa wakitumia vivuko visivyokuwa vya uhakika kuvuka katika mto huo.

Source: Mwananchi.

Kampeni ama wako serious? Kuna kipindi kazi hii walisema imekwisha fanyika na gharama za daraja zilikadiliwa kuwa ni Sh Billion moja, leo milioni 300 ama mwandishi kakosea?
 
Na Samuel Msuya,Morogoro

UJENZI wa daraja la Mto Kilombero linalounganisha Wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, utaanza mara baada ya kampuni inayofanya usanifu, kukamilisha kazi yake Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Morogoro,Charles Madinda alisema kazi za usanifu wa daraja hilo, inafanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Nimeta ya Dar es Salaam na Kampuni ya Howard Humphrey ya Kenya.

Kwa mujibu wa Madinda kazi hiyo iko katika hatua ya mwisho na inatarajiwa kuwa ifikapo Oktoba, itakuwa imekamilika .

Alisema ya kusanifu daraja hiyo, itagharimu kiasi cha Sh300 milioni na kwamba kazi hiyo ndiyo itakayobainisha gharama za mradi huo.

Meneja huyo alisema pamoja na kuweka nguvu katika ujenzi wa daraja hilo, serikali pia mbioni kufungua barabara inayounganisha Mkoa wa Morogoro na Ruvuma, kupitia Lupilo,Malinyi hadi kijiji cha Kitunda, wilayani Namtumbo.

Meneja huyo alisema tayari Tanroads imeshakamilisha ujenzi wa daraja la Mto Fuluwa wakati ikiendelea na ujenzi wa daraja la Mto Mwatisi, ikiwa ni sehemu ya mkakati huo.

Alisema hatua pia zimechukuliwa kusafisha barabara kutoka Kilosa kwa Mpepo hadi Londo mpakani mwa Morogoro na Ruvuma.

Kukamilika kwa daraja la Mto Kilombero kwa kiasi kikubwa, kutawaondolea adha ya usafiri wananchi wa Wilaya ya Kilombero na Ulanga, ambao kwa miaka mingi sasa, wamekuwa wakitumia vivuko visivyokuwa vya uhakika kuvuka katika mto huo.

Source: Mwananchi.
 
Afadhali maana ukipanda kile kivuko unakosa amani kabisa,ukifika ng'ambo unahema,unamshukuru Mungu.

Tuombe Mungu hayo maneno yawe na ukweli ktk utekelezaji wake.
 
Oktoba 2010 inakakaribia kila kitu kilichosahaulika kitakumbishwa, tutaambiwa, tutaamini, tutasuburi hakuna kitakachoendelea come 2015 hadithi ni ile ile, siku zinaenda. Soma signature hapo chini
 
PAMOJA KUA NI SIASA au ni sehemu ya kampeni hapana wacha wajenge hili daraja, maana mimi nilisoma Kwiro , aisee mtu asikwambie ,kutokuwepo kwa daraja hilo ni chanzo cha umasikini wa Wilaya ya ulanga, maana kutoka kivukoni hadi mahenge ni kilometa 70, mwaka 1997 nauli ilikua ni shilingi 2500, kwenye vi Canter au landlover 109.

Wakati huo mwaka 1997 nauli kutoka Moro hadi Dar ilikua Tsh 1500, kwa umbali wa km 180.

Unaweza kupima hali ikoje UMEME ULIFIKA MWAKA 1995 HUKO MAHENGE.

MAANA UKIVUKA PALE SALAMA UNAJIPONGEZA NA NGALANGE.
 
Sio kwamba wasijenge, actually hawatajenga, hii ni danganya toto tu, hebu jiulize kwa nini hawajenga daraja siku zote hizo. Ulanga ni potentially kiuchumi kwa nini wasijenge daraja siku zote hizo mpaka waone uchaguzi unakaribia ndo ahadi zinaanza.

Kumbuka daraja la kigamboni toka walivyoanza kusema limejengwa mpaka leo???? Kumbuka barabara ya kigoma mjini wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.
 
OOH NI KWELI NGAMBO.

......maana uchaguzi wa mwaka 1995 ulipokua unakaribia wakati wakazi wa mahenge wakiwa wamemchoka mzee G. Itatiro, serikali ya CCM iliwapelekea wapogoro Umeme, kwa mara ya kwanza uliwaka pale Bomani ilikua mwezi June mwaka 1995, kufikia October Mahenge mjini kote kulikua na Umeme.

Uenda wakatimiza hili kwa ajili ya pressure ya kumuokoa Ngasongwa na mwenzie simkumbuki jina.
 
kujenga madaraja sehemu ambazo kuna vivuko ni ndoto kwanza serikali inategemea mapato kutokana na hicho kivuko, ushauli wangu au maoni yangupeza zinazopatikana kutokana na hivyo vivuko zisaidie maendeleo katika maeneo husika kama hapo kilombero pesa ziende kusaidia watu wa ulanga na wenzao wa jirani kilombero
 
Na Samuel Msuya,Morogoro
UJENZI wa daraja la Mto Kilombero linalounganisha Wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, utaanza mara baada ya kampuni inayofanya usanifu, kukamilisha kazi yake Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Morogoro,Charles Madinda alisema kazi za usanifu wa daraja hilo, inafanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Nimeta ya Dar es Salaam na Kampuni ya Howard Humphrey ya Kenya.

Kwa mujibu wa Madinda kazi hiyo iko katika hatua ya mwisho na inatarajiwa kuwa ifikapo Oktoba, itakuwa imekamilika .

.

Mwananchi wa kawaida akisikia na au kusoma anapagawa kabisa, hajui tofauti ya ujenzi na usanifu kwake vyote ni sawa ni kama kaliona daraja. Usisahau kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 2009 ambao wenzetu wameushupalia kwelikweli,huu ni mtaji kwao.
 
Back
Top Bottom