Kivazi na miguu!!

Ras

Senior Member
Mar 16, 2007
126
6
Wanajamii habari! Nina jamaa yangu mmoja, tumekuwa washikaji kwa muda mrefu sana toka enzi za Sekondari Jite. Jamaa kaoa na bado ndoa yao changa tu kwani ina miezi mitano sasa, jamaa kaniomba ushauri kuhusu tatizo fulani, anasema mke wake anapendelea sana kuvaa pedo na sketi fupi fupi shida ni kuwa mkewe huyu ana miguu mnyembamba sana hali ambayo mshikaji hupendi awe anavaa hivo lakini anashindwa kumweleza aanzie wapi kwani mkewe pengine anaweza jisikia vibaya akiambiwa kuhusu hilo!! Mawazo yenu wana jamii, jamaa afanyaje?:A S 39:
 
Sasa alimwoa wa nini kama anaogopa kumweleza kitu kidogo kama hicho? Uwazi wake uko wapi kwa mwenzie wa ndoa? Mi nadhani amwambie tu. Kama anaona shida kuzungumzia wembamba wa miguu kama sababu ya kutopendelea nguo fupi, anaweza kutumia sababu nyingine, mf maadili: anaweza kumwambia kwamba kuvaa nguo fupi ni kujidhalilisha kwa watu. Au anaweza kutumia sababu ya 'kiwivu' kwamba akivaa nguo fupi anavutia macho ya wengi, na kwamba yeye (mume) hapendi kuona wanaume wengi wanamtazama; kumbe yafaa afunike miguu. Au anaweza kutumia sababu ya Unadhifu: kwamba yeye mwanaume anavutiwa zaidi amwonapo mkewe kavaa nguo ndefu kuliko nguo fupi, nk. nk. Sababu zipo nyingi tu.
 
ha ha ha ha ha........awe anamnunulia nguo zinazoficha miguu, mkewe ataelewa tu kwamba mume anapenda mavazi ya aina hiyo
 
wanawake bwana, hawaeleweki kabisa, unaweza kuongea nae vizuri. very polite language, lakini ugomvi utakaotoka hapo ukawa ni balaa.
 
Huyo rafikio kwani alikuwa hajui mkewe ana miguu myembamba kwani wakati wauchumba wo huyo dada (mkewe ) si alikuwa anavyaa wakitoka out na anamsifia kuwa amependeza?? sasa kesha mweka ndani ( amemwowa) ndio anaona miguu myembamba angemweleza tangu walipokuwa wachumba maana hayo mavazi inaelekea alikuwa anavaa tangu enzi za uchumba wao kama alikuwa hayafurahii angemweleza tu kuwa heri uva suruali kuliko hizo pedo na vimini mama angeelewa kuwa mume hapendi..
 
wanawake bwana, hawaeleweki kabisa, unaweza kuongea nae vizuri. very polite language, lakini ugomvi utakaotoka hapo ukawa ni balaa.

Hapo hapo Mkuu ndipo mshikaji anaogopa isijekuwa zogo
 
Kuna ule msemo unaosema " Samaki mkunje angali mbichi".... huyo rafikio angemueleza tangu alipopewa green card kuwa sipendi hiki na hiki na hiki na huwa napenda hivi hivi hivi... nk mambo yangekuwa mswano tu
 
Mwambie wife anafanya kitu ambacho yuko confortable nacho..akisubiri miguu inenepe hiyo siku haitafika.
Lakini pia kama jamaa anaona ni myembamba sana si amwambie hata kiutani utani
 
Mwambie wife anafanya kitu ambacho yuko confortable nacho..akisubiri miguu inenepe hiyo siku haitafika.
Lakini pia kama jamaa anaona ni myembamba sana si amwambie hata kiutani utani

Mmh! FirstLady, ni utani gani huo atakaoutumia? Nijuavyo mimi utani wa kweli huwa wauma!! halafu afadhari kwa mwanaume Mwanamke inakuwa kesi inayojitegemea hiyo!!:pound:
 
Mmh! FirstLady, ni utani gani huo atakaoutumia? Nijuavyo mimi utani wa kweli huwa wauma!! halafu afadhari kwa mwanaume Mwanamke inakuwa kesi inayojitegemea hiyo!!:pound:

hahahaha utasema aaah wife leo ungeondoka na ile skin jeans ungekuwa kisura kweli kweli..
Wife leo nimekununulia nguo hii ..naona itakufit kweli kweli...
Mama choice ya leo badilisha mie napenda hii hapa unatoa mfano ..mwisho wa siku atakupenda zaidi na kugundua unampenda na kuthamini uvaaji wake
 
Nashukuru ntamshauri mshikaji kijinsi hiyo ajaribu kuondoa hilo tatizo. hahah
 
hahahahha,miguu wengi hatuna ila tunavaa vimini,huyo mwanaume naye ana kasumba tu chaaa!
 
...Lol, na 'picture' mtu kama anatembelea mikono vile.

Anyway, sidhani kama mtu ulimpenda, ukamchumbia kisha kumuoa halafu leo hii ndio uanze kuchukizwa na miguu yake. Mapenzi hayasababishi upofu wa namna hiyo jamani, miguu? ingekuwa kaongezeka/kapungua matiti au makalio kweli...
 
Ah! tayari huyo mwanamke kesha mpenda kwa yote maana naamini kuwa alimfurahia kabla ya kumleta ndani na kukubali matokeo ya lolote lile liwalo kwa hiyo akae tu kimya na kumuacha aendelee na mavazi yake hayo. Au aliuziwa mbuzi ndani ya gunia? Ki ufupi ni kwamba aizoee miguu yake hiyo myembamba.
 
au amshauri aikate
 
Mwambie wife anafanya kitu ambacho yuko confortable nacho..akisubiri miguu inenepe hiyo siku haitafika.
Lakini pia kama jamaa anaona ni myembamba sana si amwambie hata kiutani utani
he!! si amwambie kuwa ukivaa hvyo hupendezi........hutoki chicha!!
 
Mwambie wife anafanya kitu ambacho yuko confortable nacho..akisubiri miguu inenepe hiyo siku haitafika.
Lakini pia kama jamaa anaona ni myembamba sana si amwambie hata kiutani utani
....Siku amwulize tu :
"Honey umepiga sarakasiya kusimamia mikono au....?"
Atamwelewa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom