kiuno kuuma kinasabishwa na nini?

ummu kulthum

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
2,785
1,317
ana miaka 25 sio mm ummu, lakini analia na kiuno hasa akifanya kazi za kuinama kama kufua au kupiga deki amepima U.T.I hakuna kitu kwa madai yake anasema amelogwa cause alitembea na bwana wa rafiki yake.ki taaalam hii iko vip jf members?
 
ummu kulthum Mwambie pole huyo Mwenye mika 25 na sio wewe, Kabla ya kukupa Ushauri wa kutumia Dawa itabidi uende au huyo rafiki yako aende Hospitali kubwa kwa hapo ulipo unapoishi akapige Picha ya X-RAY ili tupate kujuwa ana Matatizo gani ndipo hapo tuweze kutowa Dawa kamili. Na kuhusu swala la kurogwa lipo na linawezekana inategemea Huyo Rafiki yako yupo mji gani na kwanza amalize vipimo vya hospitali kisha tutatowa dawa ya kiuno.
 
Last edited by a moderator:
Nina tatizo kama hilo na nilichukulia ni maumivu ya kawaida, nikawa natumia dawa za kupunguza maumivu lakini hazikuwa na msaada niliamua kwenda hospital ambako nilipigwa X-RAY,bahati nzuri sikuwa na tatizo kubwa nikaandikiwa dawa aina mbili nazo ni ARCOXIA (etoricoxib,MSD) 90mg natumia kidonge kimoja katika masaa 24 na NORGESIC (450+35)mg kidonge kimoja kila baada ya masaa nane na kwa kweli nimepata nafuu sana kwa kuwa maumivu nilikuwa nayasikia mpaka miguuni..

Pili kuna mtu wangu wa karibu ana tatizo kama hili yeye kwa bahati mbaya X-RAY imeonyesha kuna mfupa umesogea kutoka mahala pake lakini alianza na dawa kama za kwangu lakini maumivu hayakumuondokea na aliporudi hospital ametakiwa afanyiwe tiba zaidi na ikishindikana itabidi afanyiwe upasuaji.

Ushauri wangu ni kama alivyo tanguliza MZIZI MKAVU mwambie muhusika aende hospital ndio uamuzi wa busara.
 
Umeolewa ummu? we sema kama ni wewe ili uweze kusaidiwa! pia mshauri huyo mtu zinaa ni deni na uchafu kwa hiyo ajiepushe nao.
 
fuata ushauri wa mzizimkavu maana naelewa bila uchunguzi sahihi tunaweza toa dawa zisiweze kukusaidia au hata kukuongezea matatizo zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom