Kituo cha polisi kutegwa bomu

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Kitendo cha watu kuingia makao makao makuu ya polisi na kutega bomu inasikitisha lakini kikubwa ni inatia mashaka juu ya uwezo wa jeshi la polisi na vyombo vya usalama kwa ujumla, hii inatutisha wananchi kama vyombo vya usalama vimeshindwa kujilinda je vitaweza kulinda wananchi na taifa kwa ujumla?

wapi tunaelekea?
 
Kama waliweza kuligundua hilo bomu kabla halijalipuka, basi wanastahili pongezi, ila wasibweteke waongeze ulinzi ili watega mabomu wakamatwe kabla hata hawafika maeneo ya watu wengi.
 
bongo suala la usalama bado kabisaaaaaa tuko nyuma! eti makao ya polisi hata kamera za CCTV hawana! Unategemea nini? Lazima tukubali kutumia tekinolojia katika ulinzi....kutumia 'mashushushu' peke yake haitoshi!
 
Kama waliweza kuligundua hilo bomu kabla halijalipuka, basi wanastahili pongezi, ila wasibweteke waongeze ulinzi ili watega mabomu wakamatwe kabla hata hawafika maeneo ya watu wengi.

Mimi ni mtanzania najua wabongo tulivyo wasani. Siamini kwamba hilo bomu lilitegwa na mtu kutoka nje ni usanii tuu wa kutafuta umaarufu na zawadi kama ipo kwa ajili ya kuligundua bomu hakuna lolote hii ndio Bongo.
 
mimi ni mtanzania najua wabongo tulivyo wasani. Siamini kwamba hilo bomu lilitegwa na mtu kutoka nje ni usanii tuu wa kutafuta umaarufu na zawadi kama ipo kwa ajili ya kuligundua bomu hakuna lolote hii ndio bongo.

hilo nalo neno...
Mtegaji angefaidika nini kwa kulipua makao makuu ya polisi?
 
Hili ni tusi- makao makuu ya police imetegwa bomu ina maana hakuna ulinzi? Hebu tuwe serious kidogo wawajibishwe viongozi wa kituo hicho na waliokuwa lindoni9 siku hiyo. Wawajibishwe na isiishie tu katika kusema tumefanikiwa kulitegua what if lisingegunduliwa? NI UZEMBE MKUBWA

Wao wakiwa hawawezi kujilinda wenyewe sisi raia tutapataje imani kuwa tuna walinzi thabit? Mi cjapenda
 
Mimi ni mtanzania najua wabongo tulivyo wasani. Siamini kwamba hilo bomu lilitegwa na mtu kutoka nje ni usanii tuu wa kutafuta umaarufu na zawadi kama ipo kwa ajili ya kuligundua bomu hakuna lolote hii ndio Bongo.

Alarmists na wapenda publicity what would be the motive?????????
 
watZ wengi tupo kwa lengo la kulaumu tu bila kijua madhara yake, badala ya kulipongeza jeshi kwa kazi nzuri ya kutegua hilo bomu watu tunaanza kulaumu kuwa bongo hakuna ulinzi, ni sawa lakini vitu kama hivyo hata huko kwenye ulinzi na technolojia ya kila aina ndio kunaongoza kwa matukio ya kutisha, tujifunze kujali na kuthamini majeshi yetu ili nayo yatujali na kutulinda kwa moyo mmoja
 
Kutegwa bomu. Sijui kama kweli, labda waliangusha wenyewe. Lakini kuhusu umakini wa ulinzi Polisi sidhani kama wako makini kiasi hicho. Bomu hili limetegwa nje ya kituo cha Polisi laki pale Msimbazi Polisi jamaa aliingia akavunja sefu ya pesa akaiba mishahara na hawajawahi kumkamata mpaka leo.
 
vyombo vya usalama ni wazembe mno, labda kuna police kachukua pesa ili jamaa aweke bomu
 
naona ni wakati wa kubinafsisha polisi au kubadili utawala mzima,
ni hatari kila kukicha tukio jipya la kutegwa bomu juzi na msasani pia je usalama na polisi wako wapi?
 
Back
Top Bottom