Kifulambute
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 2,539
- 755
Polisi tena ??? JK asipoangalia nchi itamporomokea mikononi mwake.
iporomoke mara ngapi?
Polisi tena ??? JK asipoangalia nchi itamporomokea mikononi mwake.
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli
Taarifa zilizotufikia punde zinasema kuwa wananchi wenye hasira wakiwa na silaha za jadi, wamevamia kituo cha polisi mjini Mugumu wakishinikiza kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji!kweli hawa makurya hawana imani na polisi. Mh Vuai ameligusia hili kupitia taarifa ya habari ya ITV. Je wananchi kujichukulia sheria mikononi ni matokeo ya wananchi kutokuwa na imani na CCM
Source: Mdau -Mugumu
NAONA MHALIFU AMEVAA T-SHIRT LIMEANDIKWA CUF, MAMBO YA NGANGALI NINI HAYA
Jamani kwa hili kweli wananchi walichokifanya si cha busara.Mimi nilikuwa safarini wilayani Serengeti nilifika eneo la tukio kituoni kulikuwa na askari wachache pia gari la polisi halikuwepo kituoni walikuwa kwenye msafara wa NW wa TAMISEMI Agrrey Mwanli.Ilibidi gari la polisi likatishe safari kwenye msafara wa NW lirudi kituoni kuja kuongeza nguvu kuwasambaratisha hao wananchi waliokuwa wamekivamia kituo. Hakika kwa jinsi wananchi walivyokuwa na jazba gari la polisi lingechelewa kwa dk kama kumi uharibifu mkubwa ungetokea
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli
Kwanza: hakuna kabila linaloitwa MAKURYA kama ulivyoandika hapo juu. Wilaya ya Serengeti kuna watu wa makabila mbalimbali wakiwemo wachaga, wajita, wajaluo, wangoreme, wahehe, wamakonde, wanata, wasukuma, wanyamwezi na makabila mengine mengi tu. Hivyo ni makosa kuwajumuisha watu wote wa Mugumu kuwa ni MAKURYA. Ni vyema ungetumia neno WANANCHI au WAKAZI wa MUGUMU. Kwa ufupi sikutarajia matumizi ya ukabila wa kiwango hiki kwa "Great Thinker" kama wewe.
Pili: suala la wananchi kutokuwa na imani na jeshi la polisi ni la kitaifa na halina uhusiano na watu wa kabila moja peke yake. Hata hapa Dar es salaam, penye watu wa makabila yote ya Tanzania, vibaka wanachomwa moto kwa sababu ya wananchi kutokuwa na imani na mfumo mzima wa kutoa haki wakiwemo jeshi la polisi, idara ya mahakama, ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, ofisi ya mwanasheria wa serikali na jeshi la magereza magereza.
Tatu: suala wananchi kujichukulia sheria mkononi lina sura nyingi. Kubwa ni kutokuwa na imani na mfumo wa kisheria wa nchi. Ni kwa kiasi gani hawana imani na CCM siyo rahisi kujua kwa sasa hasa ukizingatia kuwa CCM ni chama tawala na kimeshinda uchaguzi mkuu muda siyo mrefu uliopita. Na kama sikosei wilaya ya Serengeti ni moja ya wilaya ambazo CCM ilishinda kwa kishindo.
Kwa mtazamo wangu wananchi wengi bado hawajaweza kuhusianisha ubovu wa mfumo wa sheria za nchi na uwepo wa CCM madarakani kama chama tawala.
sasa mbona unamkosoa mwenzako wakati na we unakosea,SHUKLE ndo nini?MANALAUMU ndo nini?wanasihasa ndo nini?attation ndo nini? hivi si muwe mnaandikia tu kiswahili?? shukle za kata hizi zimeleta mambo sana khaaaa..halafu manalaumu oooh mitihani ya NECTA migumu mtafaulu vipi kama hiki ndo kiingereza chenu...
Wanasihasa ndio kina nani tena? Kesi inanunulika kweli?
Teh teh teh teh
Hizo mishale zinanikumbusha kipindi cha dulilo na kotoreja pia kutemya.
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli
NAONA MHALIFU AMEVAA T-SHIRT LIMEANDIKWA CUF, MAMBO YA NGANGALI NINI HAYA
Kiukweli taarifa hii imenisikitisha,wakati watu wanapambana na jeshi la polic iwe inatenda haki kwa raia na pia nguvu zitumike kuwaelimisha wananchi wasichukue sheria mkono,kama picha inavyojieleza wapo karibia wananchi 30 na mikuki,mapanga na marungu,kituo kiujumla kinaweza kuwa na askari wapatao kumi na kuendelea,wanapokuja na virungu kuwadai watuhumiwa badala ya kushinikiza wapelekwe mahakani kwenye haki,unategemea kutatokea nn kama askar aliyefunzwa vizuri na mkononi ana smg yenye lisasi 30?kwa matukio kama haya kulaumu jeshi la police naona kama hatulitendei haki,wakirusha mikuki kuzuri jeshi lenye silaha ya moto wasijibu mapigo?na nn maana ya kujihami?tuwaelimishe wananchi kutochukua sheria mkono na upande wa pili tulielimishe jeshi letu litende haki,kwani haki ndio msingi wa kila kitu