Kituo cha mabasi Mwenge kimekuwa gulio

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,843
8,232
Ndugu zanguni bado hali ya kuachia mambo yaende hovyo inazidi kushamiri hapa TZ kwa sasa kituo cha daladala pale Mwenge kimegeuka gulio kwani sasa daladala zinabanwa na hata abiria nao hukosa nafasi za kupita kwani gulio limeziba hata sehemu za kupandia abiria,kwa mpango huu si ajabu hata Ikulu kukageuzwa gulio
 
Sheria za nchi zitaanza kutumika tena baada ya uchanguzi mwezi wa kumi
Lakini huo sio utendaji na uwajibikaji jamani! hilo analolisema mtoa mada ni kweli mwenge hapafai hujui kama upo sokoni au kituo cha basi,uchafu umejaa achilia vibaka,inasikitisha sana! mi nashindwa kujua kazi ya viongozi wa manispaa nini?au ni kuvaa suti? ningelikuwa ni mimi kwa hali ile hata hiyo suti ni singe vaa,ni aibu kwa viongozi wasomi kushindwa kuwajibika tena aibu sana,au mnataka na hili aje raisi wetu ndo awaelekeze nini cha kufanya?
 
Wao (viongozi) hawakanyagi kabisa ardhi ya pale mwenge stendi, huwa wanapita wakiwa kwenye magari ya viyoyozi. Hii kwao ni breaking nyuz! Raelly Mwenge hapafai kabisa, kwa mtu mgeni ataingia majaribuni! Ni sawasawa kabisa na Ubungo kipande cha tokea mataa hadi darajani kuelekea Riverside..full kero, hasa nyakati za jioni!
 
Ujasiriamali... Hakuna mtu anayeenda karume inabidi wafate abiria huko waliko....

Sio kwamba wahusika hawakioni hili, wanalijua na wanachukua kodi...
 
Back
Top Bottom