Kitumbua

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,559
21,040
Funza naingia, ukumbini kuelezea
Utamu wa kitumbua, hakika mnaujua
Nikila nafurahia,na usingizi unijia
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Nenda kwa mama Maria, lazima utarudia
Jinsi anavyoumua, na sukari kukitia
Kinanoga kitumbua, kwa chai ukishushia
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Zilikuja Kalimati, lakini haziku chati
Zikaja na chapati, zenye nyingi hanjumati
Pia vikaja visheti, na kupitwa na wakati
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Upole watakinana, kitumbua kukichana
kile ukiwa wima hata kwa kuchutama
Kukosa utalalama, na moyo kukusosoma
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Ukikiona kimevimba, utapenda kukilamba
kwa mchele si pumba, namna ya kukiumba
ni kinene si chembamba, hakika kinabamba
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Vingine vinakilanga, ukila vina mchanga
Asili yake ni Tanga, sehemu za Kibaranga
Meno yatakubanga, ukivamia kijinga
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

(c) Funzadume (Soli ya Mbingu)
 
Mwanakijiji alikuja na Sambusa, naona mkuu umefunika na kitumbua.
Safi sana.
 
mwanakijijiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! uko wapi njoo tunakusubiri ujibu ya utamu wa kitumbua na sambusa
 
Kitumbua; Sambusa ndio ugonjwa wetu wote nyamaume ukiona rangi tofauti kigodo unapagawa. Shughuli kwelikweli
 
hehehe mmmh .....vitumbua na sambusa kwenye jukwaa la mapenzi! raha kweli kweli
 
Mimi ID yako tu MUKULU...... Lkn Kitumbua kilicholala, kinakuwa kigumu Funzadume!
 
Safi mashairi yametulia, wapi Mwanakijiji? Shida kitumbua kimeingia mchanga kinalika kweli?
 
mwenye mistari atupie kidogo nataka kupeleka ili shairi RTD
 
@Kaliganikwa ukiona hujaelewa juwa kitumbua hakikuhusu ww maana si mlaji wa vitumbua...!!!
 
Back
Top Bottom