Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

Kweli jamaa ana guts za aina yake hayo aliyoyafanya yanatisha maana alikuwa anachwzea jela tangu siku ya kwanza sasa kama amemudu kwa siku 3 basi anastahili sifa
 
mbona habari haionyeshi wamejuaje kama huyo jamaa ni Dr feki? mwanakijiji fafanua kidogo habari hiyo.

walianza kumshitukiya alipo ingia chumba chaupasuwaji walipo pigasim makao maku ikaonekana hakuna mtu aliye tumwa najina analolitumia hawana lekodi nalo
 
Kama asingeingia chumba cha upasuaji ina maana asingeshtukiwa? mi nadhani pale tu alipoamrisha kufungwa kwa kituo cha afya bila kujali uhai wa wagonjwa ilibidi mawasiliano yafanyike wizarani mara moja.

Tatizo lilitokea alipoingia chumba cha upasuaji. Unajua kuna taratibu zake kuanzia jinsi ya kuvaa, kunawa mikono n.k. Hata mfanyakazi wa kawaida hospitalini ambaye hajawahi kufanya kazi 'theatre' akiingia tu utagundua. Sasa huyu bwana ukichanganya na ukwelikuwa si daktari hali ilikuwa mbaya sana. Kwanza kulikuwa na kushangaa shangaa sana.
Vinginevyo angeendelea kumtafuna bata kwa sana tu.
 
Aidha mtaalamu huyo'feki' alikaa kwenye halmashauri hiyo kwa siku tatu huku akigharamiwa kila kitu kama kiongozi kutoka wizarani, na kupewa ulinzi wa jeshi la polisi ambalo hivi karibuni limejikuta likikumbwa na kashfa ya kutumia nguvu zaidi . "Ameitia halmashauri yetu hasara kubwa nimeishamuagiza mkurugenzi ahakikishe gharama zote zilizotumika kwa ajili yake zinarudishwa,alikuwa na msafara mkubwa wa magari wakati akizungukia vituo vya afya"alieleza mwenyekiti huo

Hivi kama ni mtumishi wa serikali toka wizarani inakuwaje agharamiwe na Halimashauri wakati tayari anakuwa amepewa masurufu toka alikotumwa, naona kuna kuwa na ulipwaji mara mbili na matumizi manaya ya fedha ya serikali, kwa maana hiyo waliolipa na aliyelipwa wote ni wahalifu
 
Mgeni huyo katika wilaya ya Ngara alikifunga kituo cha afya Bukililo kwa madai kuwa hakuridhika na kiwango cha huduma zilizokuwa zinatolewa,na mwenyekiti kudai kuwa halmashauri iliingia gharama kubwa kuwahamisha wagonjwa kwenda vituo vingine. Pia John Shimilimana aliiambia Fikrapevu kuwa baada ya kuagiza kufungwa kwa kituo hicho walimbembeleza kuwa wagonjwa wangeweza kupoteza maisha kwa uamuzi huo wa ghafla,jambo alilodai angelifikilia baadaye baada ya kuwa wametekeleza agizo lake.


Labda anaweza kuwa kama yule wa tukio la nape pale St. Peters
 
Shimilimana,Hivi majina haya ndo alina Uwingilimana,Habyarimana,Ndendakumana n.k.Anyway,kwanza mipaka yenyewe iliwekwa na wakoloni,Afrika ni moja.​
breakingnews.jpg


Kama vile mlolongo wa vituko na kashfa havijaisha serikalini huko Ngara mtu aliyejitambulisha kuwa ni daktari wa magonjwa ya binadamu na afisa kutoka Wizara ya Afya ameivuruga wilaya ya Ngara mkoani Kagera na kuitia hasara baada ya kufunga kituo cha afya Bukililo na kushuhudia kazi ya upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya misheni Rulenge. Yote yakigharimiwa na kufanyika chini ya halmashauri ya Ngara inayoongozwa na CCM.

Mtaalamu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Dr. Illongo Mlawa kabla ya kugundulika kuwa ni tapeli aliongozana na msafara wa watendaji wa halmashauri akiwa na ulinzi wa polisi kwa kile alichodai ni kukagua shughuli zilizoko chini ya wizara hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Shimilimana aliyekuwa pia katika msafara huo,alijitambulisha kuwa ni Naibu Katibu mkuu idara ya Utumishi.


Aidha mtaalamu huyo'feki' alikaa kwenye halmashauri hiyo kwa siku tatu huku akigharamiwa kila kitu kama kiongozi kutoka wizarani, na kupewa ulinzi wa jeshi la polisi ambalo hivi karibuni limejikuta likikumbwa na kashfa ya kutumia nguvu zaidi . "Ameitia halmashauri yetu hasara kubwa nimeishamuagiza mkurugenzi ahakikishe gharama zote zilizotumika kwa ajili yake zinarudishwa,alikuwa na msafara mkubwa wa magari wakati akizungukia vituo vya afya"alieleza mwenyekiti huo.


Aidha mwenyekiti huyo alilalamika kuwa alilazimika kuwaita madiwani siku ya Jumamosi ili wakutane na kiongozi huyo,ambaye alitoa maelekezo ya kutaka watumishi wa idara ya afya kulipwa stahili zao haraka baada ya kupokea malalamiko ya kutolipwa kila alipopita.


Mgeni huyo katika wilaya ya Ngara alikifunga kituo cha afya Bukililo kwa madai kuwa hakuridhika na kiwango cha huduma zilizokuwa zinatolewa,na mwenyekiti kudai kuwa halmashauri iliingia gharama kubwa kuwahamisha wagonjwa kwenda vituo vingine. Pia John Shimilimana aliiambia Fikrapevu kuwa baada ya kuagiza kufungwa kwa kituo hicho walimbembeleza kuwa wagonjwa wangeweza kupoteza maisha kwa uamuzi huo wa ghafla,jambo alilodai angelifikilia baadaye baada ya kuwa wametekeleza agizo lake.


"Kama mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara nilimbembeleza asikifunge kituo cha Bukililo kwani wagonjwa wengi wangeteseka na kupoteza maisha,tuliwahamishia katika vituo vingine"alisema Shimilimana.


Pia kutokana na wadhifa wake na kujitambulisha kuwa ana taaluma ya udaktari na ni kiongozi wizarani aliruhusiwa kuingia katika chumba cha upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya Misheni Rulenge na kushuhudia madaktari walivyokuwa wakiendelea na majukumu yao. Hata hivyo mwenyekiti huyo alidai kiongozi huyo alianza kushtukiwa baada ya kuingia na kutoka katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Rulenge ambapo pamoja na kuvaa mavazi yanayotumiwa na madaktari tayari kwa upasuaji hakuweza kuhoji wala kuuliza suala lolote linalohusiana na taaluma hiyo.


Mwenyekiti huyo amedai baada ya halmashauri kufanya mawasiliano na wizara iligunduika kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyetumwa huko na hakuna rekodi zozote za jina linalohusiana na mtu huyo. Kwa mujibu wa Shimilimana Dk Ilongo Mlawa baadaye alikamatwa juzi na kuwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Salewi alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo aliomba apewe muda kwa maelezo kuwa alikuwa anaendesha kikao.



SOMA KITUKO HIKI CHA AINA YAKE NA VINGINE HAPA

 
Duhh kweli hii ndiyo bongo, lolote lawezekana.

Hata mkurugenzi wa halmashauri hajui utaratibu,sheria hivi hawa watu watafundishwa mpaka lini yani wewe unapokea mgeni bila hata barua wala taarifa. Wazee wa intelegensia nao!!!!

Aaaahhh karagabao. MMJ inafurahisha lakini ni hatari sana.
Kwani ziara za kushtukiza huwa zinatanguliwa na barua?Hapa hakuna sababu ya kumlaumu mkurugenzi,labda mganga mkuu wa wilaya maana yeye ndiye alitakiwa kumbaini mapema.
 
Amefikisha ujumbe kuwa kwa hivi sasa watumishi wengi ni waoga hasa wakisikia MTU ametoka wizarani,hivyo basi hawawezi kuhoji kuhusu utaratibu,maana wanafanya kazi kwa mapokeo badala ya kiyakinifu.
 
Faida ya ziara za kushitukiza ndiyo hizo,maana hamuwezi kuhoji kuhusu utaratibu,zaidi ya kuona nani atatumbuliwa.Na hata hapa sijuwi kama hatatumbuliwa MTU.
 
Haya ni matokeo ya kufanya kazi kwa hofu na kutaka kumridhisha mkuu. Kwa nini mawasiliano na wizara husika hayakufanyika mapema? Hofu ya kuonekana hawajui majukumu yao? hofu ya kutumbuliwa? Kimsingi ninachoona viongozi hawa wamekosa uhuru wa kufanya kazi. Wanatambua kuhoji ni sumu kali sana inaweza kuwapotezea kibarua.

Ina maana huyu jamaa asingeingia kwenye chumba cha upasuaji,labda kwa sasa angekuwa anatembea Halmashauri nyingine. Ujinga ungekuwa uleule tu maana ni lazima watu wangepeana taarifaa kuwa mkuu anakuja, wekeni mambo sawa. Huo muda wa kutafuta uhalali wake ungetoka wapi.

Hali ya kutohoji kwa sasa ni tatizo kubwa mno kwenye taasisi za serikali. Ikiwa utahoji mambo halali kwa mtu halali, una hatari kubwa sana ya kukosa kazi. Tukio hili, hapa naona ingekuwa halali kabisa kwa Mkurugenzi kujiuzulu na ingekuwa halali kabisa kwa Raiskumwajibisha Mkurugenzi.
 
OP alibandika hili miaka sita (6) iliyopita sasa hayo mambo ya kusema waliogopa kuhoji wangetumbuliwa na style ya ziara za kushtukiza ni irrelevant.
 
Kama mnashinda kutukana humu mnadhani mtaangalia barua. Kwani Chadema haina wafanyakazi Serikalini. Utapeli hauna chama. Nenda Chadema uliza uchaguzi wa Mwenyekiti Mara ya kwanza na ya mwisho ulifanyika lini.
 
Back
Top Bottom