Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

Safi sana Dr Ilongo!

Kama JK anazunguka nchi zima na kutoa ahadi hewa, basi, ni heri huyu ambaye alifika na kuamuru kufunga kituo cha afya ambacho hakikidhi haja.. Halafu na kuagiza watumishi walipwe stahiki zao haraka!

Miaka michache iliyopita, huko Dodoma, kuna msichana aliajiriwa kama Daktari kwa muda wa miezi kadhaa, na baadaye ilikuja kugundulika kuwa hata Darasa la saba alishindwa masomo!
 
Kinachonishangaza Tanzania ni jinsi usalama unavyoratibiwa. Ukisema hakuna usalama sikubaliani na hili kwani viongozi na watu maarufu usalama wao haujawahi kuwa wa mashaka kabisa.........

Mkuu viongozi na watu maarufu hata wao usalama wao uko hataranini.

Watu wa usalama prority zao ziko kwenye
phyical security. Ndio maana Hata Rais wetu alidondoka. Wao wakimvisha Bullet poof wanajua wamemaliza. Kwenye chakula may be wanacheki poison badala ya sugar, fat etc content.... Ile issue ya kiongozi kuanguka kulitakiwa kuwa na uwajibishaji..........

Nadhani umeelewa. Priority za securty wanazofanya bado ni za mwaka 1970.

Huyo Jamaaa ningekuwa mimi Ningeshauri TISS wampe kazi. kama sio TISS basi CAG. Inaonekana anajua mambo na loopholes nyingi how halamashauris wanavyofanya kazi na mapungufu kibao ya communication

 
siku tatu jamaa anakula bata tu na akaondoka na point tatu muhimu? Hii ni hatari, hivi hawa wanaojifanya sijui intelijensia pindi tu kunapokuwa na mkusanyiko wa cdm wapo wapi? Binafsi na mpongeza huyu jama! Huyu na mfananisha na michael scoff au matt damon!! Ningependa ajitokeze tu hata kupitia jf atujuze namna alivyo waingiza shule hao wanyarwanda wa tz na vilaza wao usalama wa ccm.


napata shaka na intelijensia ya ccm maana lazima nao walitoa support kwenye msafara wa dr huyo wa ukweli, i ril appreciate the guy, kwn ni jinsi gani anaonesha udhaifu uliopo katika serikali hii.
 
Kama asingeingia chumba cha upasuaji ina maana asingeshtukiwa? mi nadhani pale tu alipoamrisha kufungwa kwa kituo cha afya bila kujali uhai wa wagonjwa ilibidi mawasiliano yafanyike wizarani mara moja.
 
Mwanakijiji usishangae sana kama tunakuwa na rais mwizi unategemea huko chini watafanya nini kama sio kuendeleza umburukenge.

Mafisadi wanalindwa, walikuja na ngonjera mpya ya magamba sasa sijui wataleta mpya ipi? Ngoja kwanza wajilipe na hii Dowans mpya inayokuja kwa njia za kiubabaishaji.
Wacha nakubaliana nawe, nakubaliana nawe katika hilo, nchi hii ni nchi ya watu wa kitu kidogo, fikra rojo na mtizamo takataka... hakuna anaeogopa kufanya uhalifu kwakua toka juu mpaka chini mfumo umeoza kabisa.
 
Huyu jamaa nadhani hatakiwi kushitakiwa kwa kukagua huduma za afya. Viongozi wa serikali wao wameshindwa kufanya hiyo kazi, ngoja sasa wapewe msaada na raia.
 
Ila.. huyo nadhani kaamua kwenda mbele zaidi tu ya wengine; maana wapo wengi mijini wanaojipitisha kama "Msaidizi wa rais".. nimesoma habari moja (iliripotiwa hapa) jamaa aliyejifanya ni Askofu Malasusa akijaribu kumtapeli Meya wa Ilala sijui! Nadhani watu wameshajua namna ya kutapeli kwa kutumia madaraka maana wanajua watu wanaogopa wenye mamlaka. Ndio maana miye mwenzenu nawapuuzia sana watu wenye kujiona wana madaraka fulani! Kwamba wanafikiri kwa sababu yamadaraka yao wanaweza kukufanya uinamishe kichwa ukainama, ubong'oe na ukabong'oa.
 
yaaani hao viongozi wa halmashauri ndio vihiyo kweli,unataka kuniambia wao hawajui hata viongozi wakuu wa wizara husika? wanafanyaje kazi sasa kama hata viongozi wakuu wanashindwa kuwa na majina yao halisi?
kikawaida kunapo kuwa na msafara wa viongozi wakuu kama hao huwa kuna ujumbe ambao unatumwa kabla ya mda wa safari ili viongozi watakao mpokea mgeni waweze kujiandaa,sasa ilikuwaje hawa jamaa kumpokea huyo jamaa feki pasipo kuwa na taarifa yeyote ile kutoka wizara husika

hayo ni matatizo ya kunyenyekea viongozi pasipo hata kuwa na tabia ya kuwahoji ki undani zaidi

Umakini wa kazi haupo apo
 
Hapo kuna tatizo katika Halmashauri yote kwa ujumla, mtu anajitambulisha kwa mdomo kisha wanampokea na kufanya kazi kubwa hivyo tena siku 3! No kukagua kitambulisho, no mawasiliano anakotoka!!!!! agrrrrrrrrrrrrrrrr, ni aibu hata kuisoma hii aise
 
Sipati picha alikuwa na msafara wa magari je plate namba zilisomekaje?madereva wa hayo magari wamekamatwa?hakuambatana na VIONGOZI wengine toka huko WIZARANI?
 
Ila.. huyo nadhani kaamua kwenda mbele zaidi tu ya wengine; maana wapo wengi mijini wanaojipitisha kama "Msaidizi wa rais".. nimesoma habari moja (iliripotiwa hapa) jamaa aliyejifanya ni Askofu Malasusa akijaribu kumtapeli Meya wa Ilala sijui! Nadhani watu wameshajua namna ya kutapeli kwa kutumia madaraka maana wanajua watu wanaogopa wenye mamlaka. Ndio maana miye mwenzenu nawapuuzia sana watu wenye kujiona wana madaraka fulani! Kwamba wanafikiri kwa sababu yamadaraka yao wanaweza kukufanya uinamishe kichwa ukainama, ubong'oe na ukabong'oa.

And actually is a sign of fear trying to cover his/her incompetence and lack of confidence in whatever he is trying to show is capable of doing or has authority in it! Mtu mwenye kujitambua kuwa ana madaraka na kujua nguvu hiyo katika utendaji wake hawezi kujitutumua kuwa ana madaraka hayo kwa kuogopesha wengine ili bidi watu watambue hilo kabla ya kuambiwa kwa jinsi unavyolandana na hayo madaraka katika utendaji wako na siyo katika kuvictimize wengine kwasababu tu kuna external force inayoku back katika hilo and alone huna hiyo authority inside as an intrisic value ila tu ni imparted kutokana na taratibu.

Huhitaji kumwambia mkeo kuwa wewe ni mume wake kama kweli una exercise uume wako katika all areas of dominion, ukiona hivyo basi ujue una hitaji kujiangalia kweli kama wewe ni mume kwa huyo mke ama ni mlezi/provider of material things kama kumzalisha watoto na kumpa jina la kuwa ameolewa ambayo kila mtu aitwaye mwanaume anauwezo wa kufanya hivyo.

Kwakweli dharau yangu ni kubwa kwa watu hao whatsoever authoritative they are na pia wale wote wanaowahonga wenzao kwa pesa ama inferior things nakujimulika kwenye TV kama vile wanayoyafanya niyakuheshimiwa sana wakati ni udhalili mkubwa; only kwasababu hao wametokea kuwa deprived of their basic needs na kusahu kuwa heshima haiji kwa kununua bali kuacha foot print kwenye mioyo ya watu...maana wakila pesa, khanga ama Tshirt yako ikiisha wanasahau kama uliwahi kuwahonga...
 
Hapo kuna tatizo katika Halmashauri yote kwa ujumla, mtu anajitambulisha kwa mdomo kisha wanampokea na kufanya kazi kubwa hivyo tena siku 3! No kukagua kitambulisho, no mawasiliano anakotoka!!!!! agrrrrrrrrrrrrrrrr, ni aibu hata kuisoma hii aise

Unaweza muuliza boss wako kitambulisho Tanzania? Kuna siku police walikuja nyumbani kwangu kukamata mtuhumiwa na pia kukagua kutokana na jirani kwenda kumshitaki huyo kijana polisi. Later on ikaja gundulika jirani alikuwa na ugomvi na kijana wa kazi bila mm kujua. So ikatokea kwamba huyo jirani akaenda police kuripoti kuwa ana hisi kijana jirani hapo ameingia ndani kwao bila kujua akaenda mpaka chumbani kwake na kuiba vitu kadhaa. Then ma polisi wakaja asubuhi na mapema kupekua eti wakaongea na house girl wangu na kuanza process ya kumkamata huyo kijana na kumpiga piga sehemu sehemu then mimi nikasikia makelele na kutoka nje. Nikawauliza nyie kina nani wakaniambia sisi polisi nikauliza vitambulisho na barua ya kuja kufanya hivyo kwenye premise yangu iko wapi? Wakaniambia si waoni walivyo vaa ama nataka na mimi wanijumuishe kwenye hiyo kesi ya wizi...Ukweli hizo sheria hata sizifahamu vizuri nikawauliza so partly nikawa siwezi kujitetea vizuri lakini nikawa na uliza logical questions tu. Mfano je jambazi hawezi kuja kwa style yenu and we had argument ambazo mm nikaona kama vile tunaongea kwenye level ya tofauti. Nikaamua kupiga simu mwenyewe makao makuu kisha ndipo wakaniambia ni kweli hiyo issue ipo kwao na niwaache wamchukue huyo kijana na mchana watakuja na formal letter kwaajili ya inspection. I realy was confused eti waje mchana what if mimi nikaenda kuondoa hivyo vitu vya wizi na kuharibu evidence inakuaje...Any way kwasababu hata mm sikuwa najua hizo sheria nikaamua kukubali kwaajili ya ujinga wangu. Lakini kwakutumia tu logic is this what things need to be done? Je wote tusomee sheria kweli ili kujilinda badala ya kulindwa na serikali yetu?
 
Huyu Jamaa ametuonyesha jinsi gani serikali yetu ambavyo haipo makini na ilivyojaa viongozi wasiojua lolote hasa katika ngazi za wilaya. Nadhani Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya pia walipaswa kukamatwa kwa uzembe maana hapo hata ile kamati ya Ulinzi na Ulasama ya wilaya ni zembe pia.
 

mwenyekiti huyo amedai baada ya halmashauri kufanya mawasiliano na wizara iligunduika kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyetumwa huko na hakuna rekodi zozote za jina linalohusiana na mtu huyo. Kwa mujibu wa shimilimana dk ilongo mlawa baadaye alikamatwa juzi na kuwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kamanda wa polisi mkoa wa kagera henry salewi alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo aliomba apewe muda kwa maelezo kuwa alikuwa anaendesha kikao.​



kazi kweli kweli wamekutana matapeli wote
 
imekaa kama vile alikuwa anafanya rehearsal ya sinema, tapeli anafanya ziara?
 
ndio maana idara ya ulinzi na usalama ya nchi ilikuwa kimya wakati mapesa ya epa yanaporwa sembuse kwa hawa wasanii wa mjini ambao wananjiita askari kanzu na usalama wa tiafa wanaonyanyasa watu hapa mjini.......noma. nilkutana na mmoja maeneo ya cocobich nimepumzika akasema sio sehemu zpte zinazoruhusiwa akaniambia ni usalama wa taifa nikamdanganya na mm kuwa ni mtoto wa mwanajeshi naishi makongo akaniacha fasta............hao wapo wengi sana
 
hii ni aibu kubwa kwa taifa letu mpaka leo hii bado tuna watu wajinga sana kiasi kama hiki?hili ndio tatizo hasa hizi kazi zakupeana kishikaji na undugu JK kafanye semina hata mikoani, wilayani, tarafani, katani, vijijini na pengine hata vitongoji ndio utasalimika lakani kwa mtaji huu unaviongozi wajinga sana sijaona polisi au hata hao mkuu wawilaya na safu yake yote. Dr. mkuu wa wilaya, na hospitali husika wanasitahili kufukuzwa maana huwezi niambia leo hii mtu amekuja anfanya ukanguzi bila hata vielelezo vyovyote na we unamruhusu afanye. hii ni kuonyesha hatujui mipaka ya majukumu yetu na nini cha kufanya niaibu.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom