Kituko masaki: Familia nyingine bana (hakikisheni kuna maji na TP)

Purity1

Member
Jul 4, 2011
15
5
jamani hiki ni kituko cha kweli,
jana nimetoka na mwenzi wangu tukaenda kusalimia ndugu fulani ambao waliondokewa/walifiwa na ndugu yao. kwa ufupi familia hii ina uwezo mkubwa tu na wanaishi masaki. tukafika tukawakuta na kuwapa pole. wakati tupo hapo nikajisikia nataka kwenda long call (haja kubwa) nikaelekezwa wash room ilipo. Basi mimi niikaenda nikafanya mambo yangu. kumaliza nikataka kujifuta, salaleee mtume hakuna, toilet paper (TP), nikasema ngoja nitumie maji.. toba!! mungu wangu maji hakuna.. na huwezi amini na maji ya ku-flash hakuna!! nikasema ama kweli leo nimepatikana.. bahati nzuri nilikuwa nina simu yangu mfukoni, ikabidi nimpigie MWENZI wangu aje aokoe jahazi. ikabidi afanye mpangilio niweze kupata maji na toilet paper.

my take:
  1. jamani katika familia tujitahidi kuhakikisha kuna maji na toilet paper (haina maana kuwa na nyumba yenye swimming pool halafu chooni hali ni tete)
  2. tembea na toilet paper kwenye mfuko!!
  3. simu yaweza kukuokoa katika maeneo tatatishi
 
4 fanya risk analysis kabla ya kujiachia! hujasoma mazingira ww unaendelea tu,sio ustaarabu!kama nakuona na pozi la kufungua mlango kupokea vitendea kazi!

5 jifanyie bowel training. mtu mzima kuenda haja kubwa kwa watu sio tabia nzuri. ukiamka asubuhi seat in a toilet, take ur time na haja itakuja tu. baada ya hapo unaoga unawekelea pamba na uturi kidogo unaondoka!
 
Nadhani mwanzo ulisema umekwenda kwenye msiba sio kwenye party, sasa ukosaji wa maji au TP sioni kama ni jambo la ajabu kwenye nyumba hata kama ina Sauna na Jaccuzi watu wako busy na kuomboleza na kazi hiyo ilikua ufanye wewe ulokwenda ulize kama kuna chochote chakusaidia,so kwenda kuwajazia choo, ingekua siku za kawaida umepita tuu hapo sawaa ningekuelewa,au ww ungekua huo msiba unakugusa kama ungekua na time ya ubishoo kuangalia yote hayo? ebu kua Mungwana ulienda kutoa pole hukuwenda kutafuta mapungufu ya watu.
 
mgeni unakwenda nyumba za watu
haipiti mda,unataka kwenda toilet kuacha ugali wako??????

muwe mnajisaidia makwenu kwanza,

inawezekana wamekufanyia kusudi ili ujifunze

watu wengine ustaarabu wa matumizi ya toilet ni mdogo,
akitoka yeye,toilet haitamaniki
 
samahani sikueleweka.. msiba ulikuwa umeshatokea long time.. like more than a month ago!!
 
Siku ingine ukienda kuwatembelea hakikisha unavaa "adult diapers". Unaachia mavituz hapo hapo mnapoongea, nani anajuwa? siri yako!
 
Haa sasa hao wana uwezo kama unavyotaka kutuamini..??mi naona hawana ustaarabu, kwani busara zinaanzia sehemu kama hizo maliwatoni.
 
sipati picha kama umeachia vitu hapo na ushungi ulivyojikausha lol

Khee, kwani mie ndio nlioalikwa nyumba isiyo na maji? kwanza hiyo mikaratasi sie wengine tunajikaushia tu, mwanamke maji babu tena sharti ya mawardi na maasumini.
 
hahaha,lol! kwa kweli umenichekesha kwa curiosity hii,lmao!
QUOTE=The Boss;2269239]sipati picha kama umeachia vitu hapo na ushungi ulivyojikausha lol[/QUOTE]
 
jamani hiki ni kituko cha kweli,jana nimetoka na mwenzi wangu tukaenda kusalimia ndugu fulani ambao waliondokewa/walifiwa na ndugu yao. kwa ufupi familia hii ina uwezo mkubwa tu na wanaishi masaki. tukafika tukawakuta na kuwapa pole. wakati tupo hapo nikajisikia nataka kwenda long call (haja kubwa) nikaelekezwa wash room ilipo. Basi mimi niikaenda nikafanya mambo yangu. kumaliza nikataka kujifuta, salaleee mtume hakuna, toilet paper (TP), nikasema ngoja nitumie maji.. toba!! mungu wangu maji hakuna.. na huwezi amini na maji ya ku-flash hakuna!! nikasema ama kweli leo nimepatikana.. bahati nzuri nilikuwa nina simu yangu mfukoni, ikabidi nimpigie MWENZI wangu aje aokoe jahazi. ikabidi afanye mpangilio niweze kupata maji na toilet paper.my take:
  1. jamani katika familia tujitahidi kuhakikisha kuna maji na toilet paper (haina maana kuwa na nyumba yenye swimming pool halafu chooni hali ni tete)
  2. tembea na toilet paper kwenye mfuko!!
  3. simu yaweza kukuokoa katika maeneo tatatishi
Mytake ni kwamba kubwa na ndogo umalize kwako usiwajazie bili za dawasco wenzio. Pole sana inaelekea wenyewe wanajua jinsi ya kucheza na hyo ishu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom