Kitine: Kuna waziri ameiba fedha za nchi huko nje ametia mfukoni mwake kutafutia urais

Ndio ni Membe, basi iyo ya Mtwara itakua ya pili. Lindi mjini kuna Hotel haina zaidi ya miaka 2 tangu iishe kujengwa inaitwa Lindi Oceanic View inasemekana ni ya kwake pia.

Pili hii pesa ya Comoro si ndio ile ambayo mnadhimu mkuu wa JWTZ Maj.Gen.Shimbo nae aliambiwa ameila. Inawezekana wali gawana wengi? Invisible kuna information aliitia kapuni kipindi news ya Shimbo ikijivinjali hapa JF-kwa hili anaweza kutusaidia zaidi.


Mkuu unaongelea hii?
1.1268393520.oceanic-hotel.jpg
 
Bila shaka anamsema Membe!

Hofu yangu isije ikawa ni kulipiza visasi...lakini kama anasukumwa na uzalendo, then well and good!!

Kwanini nasema isije ikawa visasi?
Nakumbuka ni Waziri Membe ndie ambae aliibua kashfa ya Hans Kitine kutumia mamilioni ya shilingi huko Washngton isivyo halali. Kama sikosei, suala lenyewe lilikuwa linahusiana na matibabu. Enzi hizo ni watu wachache sana walikuwa wanamfahamu Bernad Membe, kwani alikuwa ni mbunge tu kupitia jimbo la Mtama.
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ni kashfa hiyo ndiyo ilisababisha Hans Kitine kujiuzuru uwaziri!
Mkuu uko sahihi.
 
Siku hizi ex gamba akizungumzia uadilifu anaambiwa ana wivu,kweli Sophia Simba aliposema hakuna msafi ndani ya ccm,alimaanisha,kimsingi mfumo wa magamba ni corrupt,hata Pinda aliyejiita mtoto wa mkulima kageuka mtoto wa bepari!
 
Mkuu,

Kwa uelewa wangu, majungu ni maneno yanayozuka mtaani yakisemwa chini chini na ni ngumu ku-trace source yake. Dr. Kitine aliyasema hayo kwenye TV, sasa hapo jungu liko wapi?

Kama ni majungu, mhusika aende mahakamani kufungua kesi ya kuchafuliwa jina. Hii ni habari kubwa na yenye uchafu mwingi sana katika safari ya kuelekea Magogoni, so, kama mhusika anaona kwamba Dr. Kitine ni mzushi, afungue kesi ya kujisafisha au kusafisha jina lake.
Mkuu nani akashitaki na akamshtaki nani? Tumeambiwa Hassy Kitine hajataja jina hivyo huwezi kushitaki.
 
Asante kwa maelezo mazuri. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa tehn Kitine hakuwa waziri full. Alikuwa Naibu Waziri (I stand 2 b corrected). Je tuhuma hizo zilitosha kuondoa moral authority yake kuzungumzia masuala ya kuijenga nchi kwa kuweka sawa uongozi huu. Ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa kiongozi wa sekta nyeti na muhimu (tena wakati huo kumbuka ilivyokuwa nyeti kweli).

Lakini suala muhimu hapa, kwa hiyo ni sawa kusema kuwa Membe (kama ni yeye aliyemaanishwa katika kauli hiyo) na Kitine hawana tofauti. Maana ukiziweka vyema sentesi zako katika inferences unapata conclusion hiyo kuwa Membe (kama ni yeye waziri mhusika) na Kitine hawana tofauti, hivyo unakubali kuwa waziri aliyezungumzwa kweli siyo mwadilifu eeh?

Siwezi nikasema ndio moja kwa moja kwa kuwa hakuna ushahidi,nimepta ujasiri wa kuona na kusema mzee kitine anatapa tapa katika kutaka kulipa kisasi kile kwa kuwa suala lake linao ushahidi ambao uliwasilishwa bungeni na kumlazimisha aachie ngazi uwaziri kamili na sio udeputy na kumbuka hakuachia ngazi kirahisi alijaribu kufanya hila ili abaki kwa kuwatumia baadhi wa wabunge wasio waaminifu kwa taifa lakini watiifu kwake akiwemo mbunge wa muda mrefu wa sumve bwana Mganga Ndasa na wenzake ambao walijaribu kumtetea kwa kuleta ushahidi wa uongo, lakini wabunge wa wakati ule wakawa wakali kina Ndasa wakapigwa ban pia kwa kujaribu kulidanganya bunge.

Pia ikumbukwe kabla ya kashfa hiyo ya ufisadi wa kitoto KITINE alionekana ni waziri mmoja muadilifu ambae aliaminiwa na wengi akiwemo BIG BEN mwenyewe ambae inasemekana alikua ni mmoja kati ya aliowaanda kumrithi kwenye urais.

Kashfa ile iliyoshughulikiwa na Membe kiufanisi ndio iliyosababisha kifo cha ndoto za urais za mzee KITINE na pia kifo chake kisiasa. Hivyo anayoyalopoka lazima tuyatizame kwa tahadhari sana, tusikurupuke na kupaza sauti.

Kitine huyuhuyu kwa nyongeza aliwahi kulitumbikiza baharini benzi lake la kifahari ambalo alilipata kifisadi ili kuukwepa mkono wa mzalendo, true son of this country, EDWARD MORINGE SOKOINE.
 
Mkuu Sniper kuna siku moja nilikuwa nakunywa kahawa huku nikiangalia mpira kwenye hotel hii nikasikia majungu kwamba hii hotel inamilikiwa na familia ya Makame Rashidi

Sidhani,"General" namjua vizuri,ana hali mbaya sana kimaisha,mzee mkapa alimpeleka akawe balozi malawi angalua kumsitiri tu baada ya kuombwa na kina mzee mwinyi.
 
Frankly speeking huyu anaetajwa ni Benard Membe. Hotel anayojenga ipo Mtwara pembezoni mwa Bahari. Niliiona mwezi uliopita nilipokuwa Mtwara.

TUMBIRI wa JF
niliiona kama miezi minne iliyopita ipo pembezoni mwa bahari jamaa atatumia pesa ya kutosha kutengeneza beach(pwani) maana kuna mawe ya kutosha
 
Sidhani,"General" namjua vizuri,ana hali mbaya sana kimaisha,mzee mkapa alimpeleka akawe balozi malawi angalua kumsitiri tu baada ya kuombwa na kina mzee mwinyi.

Mkuu si unajua nchi hii wanasiasa wetu hawaweki vitu vyao hadharani basi inabaki kuwa speculations tu. Siku hizi kuna mtu anamilikishwa kila jengo kubwa linalojengwa hapa nchini ispokuwa ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF
 
Mkuu KIM KARDASH naona wamesahau kumpa shavu kwenye Tume ya Katiba hivyo anawakumbusha kuwa yupo.

Hilo nalo neno,hivi hajapewa shirika huyu mzee?

Halafu mimi nina tatizo moja,watu wa nyerere na wote waliotokea TANU YOUTH LEAGUE siwakubali kabisa kushiriki katika uongozi,hawana jipya,wakipata nafasi wanakuwa na pupa ya kukwiba tu,unajua jamaa nyerere na sokoine waliwabana sana sasa wakipata nafasi zama hizi hawafanyi kazi wanafanya wizi tu,kizazi kile tuepukane nacho sasa,wabaki washauri tu kama mzee warioba na mzee msuya.
 
siasa ni usanii....siasa ni unafiki. Huyu waziri wakati ule alikuwa akifanya kazi chini ya mtandao kitine alikuwa mojawapo ya tageti zao kwasababu naye aliutaka urais. Haya yote yanayotokea kwenye medani ya siasa ndani ya ccm na hata upinzani ni kwasababu ya vita vya makundi na tamaa ya madaraka/mali. Sasa Kitine katumwa na nani? Wanasiasa wazelendo waliondoka na Kambarage....hivi kwanini mtu atuhumiwe pale tu anapotaka au anapomsaidia mwingine kupata madaraka?
 
Katika kila lisemwalo ni vizuri kulifanyi uchunguzi. Binafsi sioni kama mtu alishika uwaziri kwa zaidi ya miaka 15 ashindwe kujenga Hotel kama hiyo isemwayo, kama fedha siyo ya wizi kuna ubaya gani?

Let us not jump to conclusion, tuwaachie wahusika wachunguze kwani tips wamepata.
 
Uko sahihi kabisa naona mzee kitine hapa hasukumwi na uzalendo bali ni kulipa kisasi kutokana na membe kuongoza safu ya mashambulizi dhidi yake kipindi kile alipokuwa waziri tena wa utawala bora,alitumia nafasi yake kufanya ufisadi kwa kutumia fedha za umma kumpeleka mkewe akatibiwe ng'ambo lakini kina membe na kina mohammed abdul aziz nafikiri kwenye kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi wake wakagundua makubwa ikiwa ni pamoja na kugundua hospitali ambayo mzee kitine na mkewe waliwasilisha stakabadhi kuhalalisha malipo hewa ya matibabu ilikua ni hospitali ya mmbwa na si binadamu,membe akauweka hadharani bungeni ushahidi huo kwani alisafiri mpaka huko ughaibuni kufuatilia hiyo kashfa iliyomhusu bosi wake huyo wa zamani wakiwa TISS na inasemekana uhasama ulianzia huko TISS.

Hapa hakuna kumtetea Membe wala Mzee Kitine. Kama mzee amezungumza mambo ya kweli basi nampongeza na sitojali kama alishawahi kumess before na kuripotiwa na Membe kama mtu mmoja alivyosema humu jamvini. Mwizi wa zamani kama kamrudia Mungu kuna tatizo? Akae kimya kisa nini? Muosha huoshwa. Binafsi nawamini Kitine kuliko Membe.
 
Hapa hakuna kumtetea Membe wala Mzee Kitine. Kama mzee amezungumza mambo ya kweli basi nampongeza na sitojali kama alishawahi kumess before na kuripotiwa na Membe kama mtu mmoja alivyosema humu jamvini. Mwizi wa zamani kama kamrudia Mungu kuna tatizo? Akae kimya kisa nini? Muosha huoshwa. Binafsi nawamini Kitine kuliko Membe.

sawa lakini tofauti mwenzake alileta ushahidi uliomfanya yeye asiwe na pa kutokea licha ya kuwa na mbinu nyingi kama shushushu mzoefu mwenye mafunzo ya hali ya juu,sasa na yeye asitapetape kwenye tvs alete ushahidi tu,hatuna tatizo,lakini majungu hapana,yeye kama alipewa nafasi akaiabuse kwa kudanganywa na mkewe hilo ni tatizo lake.
 
Back
Top Bottom