MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Anaenda wapi tena. shingo imepona?
Tangia watu wa Mbeya wampopoe mawe hakuna tena mambo ya Mh. Raisi kusimama bila ratiba, tena watu wenyewe wanaotaka awasikilize wana hasira!HEBU TUJULISHENI MLIOKO KIPAWA...mabomu ya machozi huko...ni aje wamemzuia mkuu wa nchi asipite?
Great,
Afadhali umetufahamisha walau kama hali imetulia. Ilikuwaje? Nani alikuwa anapiga mabomu hayo? Ili iweje? Kwanini wananchi watawanyishwe? Kwanini rais asiwasikilize kabla ya kuendelea na safari yake? Kipi muhimu kwake?
Friday, October 16, 2009 10:23 AM
ASKARI wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU), jana walilazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wakazi wa eneo la Kipawa, jijini Dar es Salaam waliokusanyika kando ya barabara ya Nyerere wakisubiri kumpokea Rais Jakaya Kikwete ili waweze kumweleza ma Wakazi hao walichukua hatua hiyo baada adha wanayoipata juu ya ulipwaji fidia wa nyumba zao kwa lengo la kupisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kutimuliwa kwa mabomu hayolilitokea jana majira ya saa 7 mchana na zoezi kuisha kwenye majira ya saa 9 na kupelekea barabara ya Nyerere kutopitika kwa muda.
Hali katika eneo hilo ilichafuka kwani ilitawaliwa na harufu ya moshi wa mabomu ya machozi na kusababisha wananchi, hasa watoto kukimbia hovyo kusaka maji ya kunawa uso kupoza makali ya moshi huo wa mabomu, yaliyokuwa yakivurumishwa na FFU.
Katika zoezi hilo kuna baadhi ya watu walijeruhiwa na mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Waziri, ameripotiwa kuwa ana hali mbaya baada ya kupigwa risasi na polisi wakati wakijaribu kuwatawanya wakazi hao.
Wakazi hao waliona ni bora wamsubiri JK ambaye alikuwa anatojkea Butiama katika maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Malimu Nyerere yaliyofanyika Butiama na kuona wamsubiria hapo mana wakati anapita kuelekea Ikulu lazima angewaona wananchi hao barabarani.
Wananchi hao walikusanyika huku wakiwa wameshika vitambaa vyeupe pamoja na mabango mbalimbali, likiwemo lililosomeka kuwa ‘Kipawa Hatudanganyiki kwa Vijisenti vya Zamani vya Mwaka 1967".
Wakazi hao waliweza kuwaambia waandishi kuwa walifikia hatua ya kukusanyika kwa lengo la kumweleza Rais Kikwete jinsi wanavyonyanyaswa juu ya ulipaji wa fidia zao ambazo wamekuwa wakisotea kwa miaka 12 sasa.
Aliongeza kuwa baada ya kujikusanya mahali hapo, baadaye walitokea askari polisi na kuwataka waendelee kukaa kwa amani wakimsubiri rais, lakini walishangaa kuona magari ya FFU yakiwatangazia watawanyike na walipokaidi, wakaanza kupigwa mabomu ya machozi.
Askari walifika eneo hilo na magari kama sita hivi, likiwemo gari lenye maji ya kuwasha na ma-defender mengine ya kawaida, baadaye wakamkamata Mwenyekiti wao Magnus Mulisa na wengine ambao ni Mapunda, Ally na Gobali.
Ndipo vurugu zilipoanzia kwani watu hao wakapigwa na kuanza kumwagiwa maji ya kuwasha, na hali iligeuka ilikuwa na kuwa mbaya sana katika eneod hilo.
Mwenyekiti wa waathirika hao alieleza kwa kusikitishwa kwake na kipigo walichopata kwani hakukuwa na dalili zozote za uvunjifu wa amani hasa ikizingatiwa kuwa lengo lao lilikuwa kumwona Rais Kikwete ili awasaidie.
"Tukio la leo limetufanya tukose imani na Jeshi la Polisi kwani hakututarajia kwa nchi kama yetu inayofuata utawala wa sheria, kutufanyia hivi, nasi tunaisubiri Serikali ya CCM mwakani kwenye uchaguzi ili tuiadhibu," alisema.
Kabla ya sakata hilo katika wiki iliyopita, wakazi hao zaidi ya 1,000 walifungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi ili kupewa ufafanuzi wa sheria ipi kati ya ile ya mwaka 2001 na ya 1967, inayostahili kutumika kuwalipa fidia ili kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waliamua kufungua kesi hiyo ili kujua mahakama itachukua uamuzi gani kati ya sheria hizo mbili itakayotumika kuwalipa fidia mana serikali inataka kuwalipa fidia kwa sheria ya mwaka 1967 na kugoma kuchukua malipo na kutaka sheria hiyo ibadilishwe.
Kwa miaka 12 sasa, wakazi wa Kipawa wamekuwa wakisotea malipo ya fidia kutokana na mpango wa serikali kutaka kuwahamisha ili kupisha upanuzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3339298&&Cat=1