kuna malumbano kuhusu hoja ya tundu lissu kutakiwa awasilishe ushahidi wa waziri kusema uongo. Aliyeanzisha vita ni moses machali aliyehoji inakuwaje lissu awasilishe ushahidi saa tano asubuhi hii wakati yeye ni mbunge na kikao cha bunge kinaendelea, kwa nini asipewe muda awasilishe baadaye. Mwenyekiti kakomaa lissu awasilishe ushahidi saa tano. Baadae kaibuka wenje kuomba kutoa hoja ya kuahirisha mjadala wa bajeti ili bunge lijadili jambo la dharura ambalo yeye amesema lina maslahi kwa taifa. Mwenyekiti amegoma na kusema mjadala wa bunge unaweza kuahirishwa tu pale nchi inapokuwa kwenye vita na kwa sasa nchi haiko kwenye vita. Pamoja na hayo wenje aliendelea kusimama na kutaka kutoa hoja yake lakini mwenyekiti akamtishia kumtumia askari kumtoa wenje nnje. Wenje hakusikia kaendelea kudai ni jambo la dharula ambalo lina maslahi kwa taifa. Baadae mwenyekiti kamuagiza surgent akamtoe wenje nje, sajent akiwa njiani kuelekea kumtoa wenje nje ya ukumbi wa bunge tanesco wakachukua umeme wao huku mitaa ya mabibo, hivyo sijui kilichoendelea baada ya hapo, naomba anayeendelea kutazama bunge atujuze nini kimeendelea.
Mwenyekiti wa Bunge amefuata ushauri wa Waziri Lukuvi kwa vile mke wa Lukuvi na watoto wako Bungeni hivyo mwenyekiti hakutaka kuona waziri anaaibika mbele ya mke wake, jambo la kujiuliza ingekuwaje kama Wenje naye mke wake na watoto wake wangekuwa Bungeni- pangechimbika.
hapo kwenye RED-alitakiwa aachwe asome wote hadi uishe-wananchi tusikie-lakini wao wanachofanya wanataka akaukabidhi-sasa akishaukabidhi hakuna atakaye usikia tena-maana mifano ipo-hata uongo wa pinda ulipo kabiziwa kwa spika-haukusomwa tena-so hoja ni kwamba aachwe ausome-tufahamu madudu ya hawa watu wa magambaUshahidi wa maneno hauwezi ukawa na maana yoyote. Kwa mbunge makini kama Lissu anapoongelea ushahidi nafikiri ni lazima awe na nyaraka zinazothibitisha hili. Na kama hauongozwi na ushabiki utakubaliana nami kuwa Lisu alishaanza kusoma hizo documents kuthibitisha kauli zake. Kwa hiyo alikuwa hapigi blabla za mdomo.
Tuombe MUNGUhuko tunakoenda na wenyeviti waliozubaa tutafika???
Wabunge wa Chadema wamezidi uhuni, muda wa ziada wa nini wakati Tundu Lisu alisema yuko tayari kutoa sasa hivi. Wanaharibu sana quality ya mijadala.
[/QUOTE]mwenyekiti wa leo ni yule aliyezubaa kuliko wenyeviti wote nadhani anaitwa sylivester mabumba mbunge wa dole.
Huu nao ni uongo and there are no statistics to substantiate the claims. Pamoja na CDM kuongeza viti bungeni bado hawajaweza kuipiku CCM na hii inadhihirishwa na idadi ndogo ya wabunge wa CDM ukilinganisha na CCM. Wangekuwa na busara, CDM wangetakiwa kuja na mkakati wa kujipanga ili kuongeza ushawishi wao kwenye jamii hasa kwa kutoa uwakilishi makini kama walivyofanya kina Slaa kuliko ulevi wanaoanza kuonyesha sasa.
we pimbi kweli, Mh. Tundu Lissu alikuwa tayari kutoa ushahidi pale pale, na wakati mwenyekiti akiwa amempatia muda wa kuanza kutoa ushahidi wa uongo wa Waziri, mwana-magamba mmoja akaomba taarifa, na kutaka maswali yaendelee na Lissu atoe ushahidi tym ingine, na mwenyekiti akakubaliana na taarifa ya Magamba mwenzie !sasa wewe unaongea nini, au unakurupuka tu
Mwenyekiti alikubaliana naye kwa sababu hoja hiyo ilizingatia kanuni na ratiba ya shughuli za bunge. Kila kitu kinapangiwa muda wake na hicho hakikuwa kipindi cha ushahidi kilikuwa kipindi cha maswali na majibu. Isije wewe ndo umefungwa na ushabiki huoni vitu katika upana wake.
Hebu fafanua huo ulevi ndugu!Maana hujaeleweka kabisa!Huu nao ni uongo and there are no statistics to substantiate the claims. Pamoja na CDM kuongeza viti bungeni bado hawajaweza kuipiku CCM na hii inadhihirishwa na idadi ndogo ya wabunge wa CDM ukilinganisha na CCM. Wangekuwa na busara, CDM wangetakiwa kuja na mkakati wa kujipanga ili kuongeza ushawishi wao kwenye jamii hasa kwa kutoa uwakilishi makini kama walivyofanya kina Slaa kuliko ulevi wanaoanza kuonyesha sasa.