Duh! Makampuni mangapi yanayoendeshwa na Wazungu ambayo yamekuwa na scandals mbali mbali katika uendeshaji? Wazungu si matatizo ya nchi yetu hata siku moja. Kule Rwanda hakuna Wazungu pamoja na wahutu na Watusi kuuana kwa idadi kubwa mwaka 1994 sasa hivi nchi yao inafanya vizuri sana katika sekta nyingi tu pamoja na kuwa hawana Wazungu. Kagame alikataa kabisa kuajiri Wazungu katika nafasi nyeti ndani ya Serikali yake.
Siye kila aliye ndani ya TANESCO na ana nafasi ya juu utendaji wake ni mbovu wengi tu ni wachapa kazi wazuri sana ila wanaangushwa na Serikali DHAIFU ambayo imeamua kuitumia TANESCO kama mradi wao wa kutajirika
Kama Rwanda wameweza kuinyanyua nchi yao katika sekta mbali mbali kwa kuwatumia wazawa, basi na Tanzania inaweza kabisa kufanya hivyo.
kupata scandal kwa kampuni siyo sawa na kushindwa ongoza kampuni
hapa TZ makampuni yanayo perfom better yanaendeshwa na wageni
mostly wazungu...
1.TBL
2.VODACOM
3.TIGO
4.AIRTELL
5.STANBINC
6.CITYBANK
7.NMB
8. na mengineyo meengi
nitajie wewe kampuni inayo chechmea bongo huku inaendeshwa na Wazungu....
tukubali tu kuwa 'the culture of efficiency' hatuna bado.....
tukubali kushindwa na ku 'import hiyo culture'
Nasita kukubali hayo kwa sababu najiuliza ni mpaka lini? Kumbuka tuko miaka hamsini sasa!
Halafu tatizo kubwa liko kwetu wenyewe watanzania. Hatuwezi kufanya kazi pamoja, tuna cancer ya kuchongeana sana. Tena hata kwa wageni, tunaudhaifu mkubwa sana katika hilo na imani za kichawi zimetawala mno hadi Bungeni.
Lakini nataka tu nikuambie kuwa yule Meneja wa NHC -Mchechu anafanya vizuri. Anaweza kuliendesha shirika la TANESCO.