Kitenzi cha neno "mdahalo" kwa Kiswahili ni nini?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,002
112,627
Itabidi wadahaliane (msianze kunirushia madongo..hili neno nimelitunga mwenyewe nikimaanisha wa debate). Mdahalo ni noun, kwa kiingereza debate ni noun na verb. Sasa verb ya mdahalo kwa kiswahili ndo sijui...lol
 
Hatu-ku-dahil. Lakini unafahamu nini Mdahalo. Ni neno lilotoholewa kutoka katika neno -dahil (la kiarabu) lenye maana ya (kwa undani) Sasa ukilitumia neno hilo,katika ,mantiki ya kuuliza linamaana kumhoji mtu ili kuupata undani wake kuhusu jambo fulani. Mdahalo siyo Debate Bakita walichemsha pale. Na mimi msinidahili yakhe kwani mimi siyo Mjuzi wa Kiswahili.
 
Itabidi wadahaliane (msianze kunirushia madongo..hili neno nimelitunga mwenyewe nikimaanisha wa debate). Mdahalo ni noun, kwa kiingereza debate ni noun na verb. Sasa verb ya mdahalo kwa kiswahili ndo sijui...lol

Nyani, kwanza ukitupa maana ya neno ''verb'' ki-swahili nadhani itakuwa rahisi kwa sisi watu wa pwani (wenye asili ya kiswahili) kukufafanunulia utakalo kulijuwa.
 
Itabidi wadahaliane (msianze kunirushia madongo..hili neno nimelitunga mwenyewe nikimaanisha wa debate). Mdahalo ni noun, kwa kiingereza debate ni noun na verb. Sasa verb ya mdahalo kwa kiswahili ndo sijui...lol

Mmhh! Nilitaka kusema kitenzi chake ni "dahili", nikakumbuka kudahili ni kufanya "admission", na limekuwa ni neno maarufu kipindi hiki cha migomo ya vyuo! Kwa hiyo naendelea kukaa kimya nisikilize wengine!
 
Mkiacha kufanya rejea ya maneno ya kiingereza wakati mnatafuta kunyambulisha maneno ya kiswahili ndio mtapata ufumbuzi haraka
 
jamani Injili hakuna nyimbo mpya za Rose na Bahati Bukuku? Huu ni mwaka mwingine na nyimbo mpya jamani.
 
jamani Injili hakuna nyimbo mpya za Rose na Bahati Bukuku? Huu ni mwaka mwingine na nyimbo mpya jamani.
Nyimbo za Injili na Mdahalo wapi na wapi! Au ndio umeleta mada "tudahaliane"?
Asante NN kwa istilahi mpya. Ngoja tuone kama itakubalika. Utakuwa umechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza Kiswahili. lol
 
Neno hili limekuwepo ama limetungwa na wasomi wa bakita? Na tofauti gani ipo kati ya mjadala na mdahalo?
 
NOUN
Mpambano, Mfanano, Mchakato, Mdahalo

VERB
Pambana, Fanana,Chakata, Dahala
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom