Kitendo kipi ni cha aibu zaidi?

Nimeingia kwa bahati mbaya,..kwani sikujua inazungumzia nini?...mimi hivi vitendo vinanichevua _natamani kama hayo maneno yasingekuwepo
 
Utamaduni wetu ni upi haswa?!Kuna siku niliuliza nikakosa jibu....

Yapo mengi yanayohusu "Utamaduni wetu" ila kwa context ya mada nijibu kwa kifupi kuwa: Ni ule unaopingana na vitendo vya kishoga na kubadili jinsi. Kwa wenzetu ruksa na ndo maana wanajitangaza hadharani na jamii inawajua wapo hata wengine wamepewa uaskofu nk.
 
Mkirua huo utamaduni ulijengeka lini ?!Maana sidhani kama haya mambo yalikuwepo zamani mpaka kufikia kuyapinga kwenye utamaduni wetu.
 
Mkirua huo utamaduni ulijengeka lini ?!Maana sidhani kama haya mambo yalikuwepo zamani mpaka kufikia kuyapinga kwenye utamaduni wetu.
Khaaaaaaa........ we kamshiki kangu ni noma aisee!... huachi kitu LOL
 
Mkirua huo utamaduni ulijengeka lini ?!Maana sidhani kama haya mambo yalikuwepo zamani mpaka kufikia kuyapinga kwenye utamaduni wetu.

Lizzy Utamaduni unatafsiriwa kama "The set of shared attitudes, values, goals, and practices that characterizes an institution, organization or group. Endapo jamii kwa asilimia kubwa inkubaliana na jambo fulani basi baada ya muda huo hugeuka kuwa utamaduni wa jamii husika. Endapo ushoga ni p[arrt and parcel ya maisha yetu kama watanzania na mtu haoni tabu kujitangaza na jamii haioni tabu kumu accomodate hadi anapewa madaraka then huo ni utamaduni wao. Hapa hatuhitaji documentation kama katiba. Tusisahau kuwa utamaduni hukua na unabadilika kulingana na wakati na mahali though misingi yake haibadiliki sana.

Kwa tafsiri hiyo hapo juu Ushoga na mambo yanayohusiana na hayo hauwezi kuwa sehemu ya utamaduni wetu kwan i ni jambo ambalo (pamoja na upya wake kwenye jamii yetu halikubaliwi na sehemu kubwa ya watu.
 
Mkirua asante ila tunarudi pale pale kwamba kama ni utamaduni unaenda ukibadilika na muda...yani nao unaenda na wakati.Hivyo basi huu nao umeenza kujiingiza kwenye utamaduni wetu...hata kama sio wa Kitanzania bali ni wa kundi fulani ndani ya Tanzania ...kama ambavyo mila na tamaduni za baadhi ya makabila zikivyo. Kwasababu tu baadhi ya mila na tamaduni za makabila mengine hazinihusu mimi siwezi kukataa kwamba nazo ni sehemu ya utamaduni wetu japo sio taifa zima linazozikubali na kuzifuata.

Hivyo hivyo kwa hawa watu...ndio maana siku hizi hata nguo wanaweza vaa vile wanavyopenda..kutembea tofauti na inavyoaminika mwanaume anatakiwa atembee...kuongea kwa madaha ya kike n.k mbele za watu...mitaani na hata majumbani.

Inawezekana wakawa hawakubaliki kwa asilimia kubwa ya Watanzania ila wapo watu wanaowakubali...na wao kama kundi wameufanya huu utamaduni kua wao.Kadiri kundi litakavyoongezeka ndivyo na utamaduni wao utavyoshika kasi ya kua kwenyr chati sawa na tamaduni zetu nyingine.
 
Back
Top Bottom