Hakuna kitendo kilichonishangaza kama cha Jemsi Mbatia kufungulia kesi H. Mdee hasa kwa kuwa wote wanajiita wapinzani na lengo lao ni kuitoa CCM madarakani. Kitendo kile kinanifanya kutambua uwezo mdogo wa baadhi ya wanaojiita wanasiasa, kwa sababu mimi natoka jimbo hilo na kama kweli Mbatia angelikua na uwezo wa kiuongozi angepaswa kuwa na ulewa kidogo tuu usihitaji shahada yeyote kuwa hata leo hii uchaguzi wa jimbo la kawe ukirudiwa hana uwezo wa kumshinda H. Mdee kwa sasa jinsi anavyokubalika nasisitiza kwa sasa. Hili nimeliona wakati wa kampenini na hata sasa kule site wanasema Mbatia hawezi kushinda anafanya kazi aliyotumwa na CCM.
Pili angepaswa kujua kuwa kitendo cha kumfungulia kesi mbunge mwenzake wa upinzani kinafanya aonekane yeye anafanya kazi kwa kivuli cha CCM hivyo kumpunguzia heshima kwa wanaounga mkono upinzani. Hawa ndio wanasiasa wa tanzainia wenye kudai wana sera mbadala wa hizi za CCM lakini jambo dogo kama hili hawawezi kusoma alama za nyakati.
Tujadili