Kuharibika kwa Mimba: Fahamu Sababu, Kinga na Tiba za tatizo hili

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
MISCARRIAGE.jpg

Habari wakuu,

Hili ni tatizo linalomkabiri mchumba wangu hvyo nimelileta kwenu kuomba msaada wenu. Tatizo lenyewe ni: alianza kusumbuliwa na maumivu ya mgongo hvyo tarehe 11/6 tukaenda kupima na akaonekana POSITIVE, mimba ipo. Lakini ajabu tarehe 9-13 mwezi wa 7 akaona siku zake kama kawaida.

Mwezi wa 8 hakupata siku zake kama ilivyotarajiwa yan kati ya tarehe 6-10 hvyo 2kaamua kupima nyumban na majibu yakawa POSITIVE, tukaenda hospitali kupima tena majibu yakawa yaleyale-ipo mimba lakini ajabu tena tarh baada ya wiki mbili, yaani tarehe 21/8 akaona siku zake japokuwa haikuwa ya kawaida kwani ilianza matone ya rangi ya zambarau na kisha mabonge mabonge na maumivu makali na ilidumu kwa siku tatu tu.

Tarehe 11/9 akapima tena hospital na akaambiwa ni NEGATIVE, haipo. Lakini anajisikia kuchoka pia kichefuchefu na anakojoa mara kwa mara. Ndugu zangu tusaidieni hili ni tatizo gani, anasumbuliwa na nini na tutatatua vipi hili tatizo?

Mungu awabariki sana.

BAADHI YA MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU TATIZO HILI
Nina shemeji yangu ambaye ana tatizo ambalo tumeshindwa 2fanye nini naye! Ameolewa ni kama three yrz sasa, na ktk kipindi hiki tayari alishapata mimba takriban mbili! Mimba ya kwanza ilikaa miezi mitatu ikatoka na ya pili ilikaa miezi miwili pia nayo vivohivyo!

Mbaya zaidi ni maumivu makali ya 2mbo anayoyapata wiki mbili kabla hajaingia period mfululizo hadi atapoanza kubleed!

Tulipojaribu kuenda hosptl walimpima wakamwambia mayai yake hayakomai hivyo akapewa dawa a2mie lkn hakukuwa na changez! Pia 2livoenda tena wakasema anauvimbe kwenye kizazi ambao ndo unasababisha mimba kutoka, so wakashauri operesheni ifanyike lkn kabla ya kufanyika 2lienda hosptl zingine tofauti ili kuwa na uhakika wakadai uvimbe hawauoni! Tukarudi tena kwenye ile hosptl (waliyoona uvimbe) nao wakasema hawaoni tena huo uvimbe!

Aliulizwa kama kishawahi ku2mia dawa za uzazi wa mpango na historia yake ya mahusiano, kwa bahati nzuri au mbaya aliyemuoa ndie alikuwa mwanaume wake wa kwanza (kwa mujibu wa mumewe) na hivyo hakuwahi ku2mia hizo dawa! So plz ladiez & gentlemen, nahitaji msaada wenu ktk hili kwa namna yoyote unavyoweza kuwa unalifahamu au ulivonielewa kwani huyu binti anateswa sana na hii hali!!
Heshima mbele,

Kuna shost angu kapata miscarriage na sasa kakimbizwa hospitali na mumewe. hivi ni nini chanzo cha miscarriage? ili nami nichukue tahadhari kabla ya hatari? huwa nasikia wengine husema inasababishwa na kusafishwa mara kwa mara, kumeza dawa zenye uwezo wa kuharibu mimba je kuna ukweli hapa? MziziMkavu na Riwa msaada tafadhali na mwenye kujua pia anakaribishwa.
JF Doctors,

Naombeni ushauri kwani nina MYOMA inanisumbua sana, baada ya kupima nikakuta zipo 5 zenye size tofauti na kila nikipachikwa mimba hutokea miscarriage na nimeelezwa kuwa miscarriage hizo husabishwa na MYOMA zinagombania nafasi na mtoto na mwisho wa siku zenyewe hushinda.

Ninaacho omba kama kuna dawa ya kuziondoa kabisa ama ni lazima nifanyiwe operation?
Nawasilisha.
Natumaini ni wazima na mnaoumwa M/mungu awajaalie afya njema. Bila kupoteza muda naomba kuwasilisha tatizo linalomsumbua wifi yangu.

Ipo hivi huyo dada kila akipata ujauzito kwake ni shida, yaan ikitunga tuu yeye full kuumwa. Anashindwa kula na akiweza kula anatapika.Na ujauzito haufiki miezi 3 mimba inatoka.

Mpaka sasa anasema hii ni mimba ya tano inaingia na kutoka.Hospital akienda anapewa dawa lkn tatizo lipo palepale.
Sasa hivi ana mimba nyingine lkn wote tunawasiwasi kutokana na tatizo lake.

Naomba mnipe ushauri tufanye nini hii isitoke. Pia hospitali nzuri itakayoweza kumaliza tatizo lake.

Yeye anaishi Mlandizi.

Ahsanteni


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU
MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)
Tatizo la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi. Kutokana na maombi ya wasomaji wetu, tutalijadili kwa kina tatizo hili ambalo kitaalamu huitwa Miscarriage.

MISCARRIAGE NI NINI?
Kwa kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.

Inapotokea kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.

Katika hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha kifo.

NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).

NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE?

Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.

Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)
Hitilafu katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki 13.

Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya mtoto na kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.

2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency)
Homoni ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha ujauzito kuharibika na kutoka kabla ya muda wake.

MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)-2

NINI HUSABABISHA MIMBA KUCHOROPOKA?
Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha mimba kuharibika kisha kuchoropoka. Baadhi ni kama zifuatazo:

UMRI MKUBWA
Kwa kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli (sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.

MAGONJWA
Wanawake wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (obesity), Polycystic Ovary Syndrome, malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.

HITILAFU KATIKA KIZAZI
Baadhi ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.

MAAMBUKIZI YA BAKTERIA AU FANGASI
Maambukizi ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo husababisha mimba kuchoropoka.

Sababu nyingine ni pamoja matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):

1. KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI
Dalili kubwa za miscarriage ni mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo kwa mwanamke anapokuwa kwenye siku zake.

MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)-3

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):

1. KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI
Dalili kubwa za Miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.

2. MAUMIVU MAKALI YA VIUNGO
Dalili nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo, kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.

3. KUTOKWA NA UCHAFU SEHEMU ZA SIRI
Dalili nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.

ANGALIZO: Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote, anashauriwa kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.

Endapo mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.

MADHARA YA MISCARRIAGE
Kuna madhara mengi kiafya kwa ujauzito kuharibika. Miongoni mwa madhara hayo ni kuharibika kwa kizazi ikiwa mama hatasafishwa vizuri tumbo baada ya ujauzito wa awali kuharibika. Madhara mengine ni kuugua mfululizo baada ya ujauzito kuharibika ambapo mwanamke hushambuliwa na maradhi mbalimbali ya tumbo.

Madhara mengine ya ujauzito kuharibika ni kuathirika kisaikolojia kwa mwanamke husika. Madhara ya kimwili yanaweza kuisha haraka na kusahaulika lakini madhara ya kisaikolojia huchukua muda mrefu kusahaulika.

Baadhi ya wanawake waliopatwa na tatizo hili, hujisikia vibaya sana wanapokutana na wanawake wenzao wakiwa wajawazito au wakiwa na watoto wao wachanga, jambo ambalo husababisha msongo.
MIMBA KUHARIBIKA HUTOKANA NA SHIDA MBALIMBALI KATIKA UKUAJI WAMIMBA TUMBONI MWA MAMA

Mimba iliyoharibika wiki sita hivi baada ya kutungwa, yaani wiki nane hivi baada yahedhi ya mwisho.

Shamba la Mungu kwa watoto wasiozaliwa.

Mimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wamimba tumboni mwa mama.

Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.

Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.

Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile. Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.

Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema.

Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu au siriziki. Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine yakaingiliana.

Kati ya 10% na 50% ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.

Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito. Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa 61.9% ya uhamili ulipotezwa kabla

ya wiki 12, na 91.7% ya kuhabirika huko kulitokea bila ya dalili, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito.

Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi.

Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, hali ambayo husababisha angalau 50% ya kutoka kwa mimba mapema.

Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa ya mishipa (kama lupus), kisukari, matatizo mengine ya homoni, maambukizi, na matatizo ya chupa ya uzazi.

Umri mkubwa na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa pakubwa na mimba kuharibika ghafla.

Hiyo inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.
KUNA UWEZEKANO WA MIMBA KUHARIBIKA BILA MAMA KUJUA
Uwezekano wa mimba kuharibika bila mama kujua upo. Kitaalam hali hiyo inaitwa missed abortion.

Mapigo ya moyo kwenye ultrasound yanaanza kuonekana kuanzia wiki ya tano.

Kipimo cha ultrasound peke yake hakitoshi kufikia conclusion ya missed abortion kwa mara moja.

Kinachotakiwa kufanya ni kupima pregnancy hormone, hCG level kwenye damu. Kipimo iko kirudiwe baada ya masaa 48 au 24. Kama ujauzito uko salama, pregnancy hormone inakuwa imedouble kwa kipindi hicho. Ikipungua au kubaki pale pale basi hiyo ni missed abortion na mama atatakiwa kusafishwa.

Iwapo hakuna huduma ya kupima pregnancy hormone, basi rudia ultrasound baada ya wiki moja.

Pia ulizia kama hiyo ultrasound ina function ya colour doppler inayowezesha kuuona moyo kwa uhakika.

Ushauri: iwapo mama hana tatizo usikimbilie kumsafisha bila kupata confirmation ya mimba kuharibika kwa vipimo angalau viwili vya ultrasound na/au pregnancy hormone.

Pole kwa changamoto.
SABABU MOJA YA MIMBA KUTOKA NI HII
Wadau wa JF, samahani Kiswahili changu ni kibovu, ila napenda kuchangia kama ifuatavyo: Sababu moja ya miscarriage hii hapa: Uzazi wa mwanamke (cervix), unaweza kuwa wazi (gaping). Hiyo inasababisha miscarriage bada ya myezi miwili au 3, fetus ao kijacho kikianza kuwa na uzito (weight). Huyo uwazi wa cervix, unafanya mtoto / kijacho atoke tu bila mama kufanya kazi inayo hitaji nguvu ao laa. Kuna technics moja wapo ya kukikinga kijacho kisitoke iitwao "Strapping" ao "cerclage" kwa lugha ya French. Wanashika mwisho wa uzazi, wanaufunga na nyuzi maalum (hapana ya kushona nguo aiseee!). Sometime utaombwa kulala kwenye kitanda ambacho kimewekewa mawe chini ya miguu (head side) ili uwe umelala miguu yako na tumbo vikiwa juu kidogo ukilinganisha na kichwa cako. Halafu utapewa some aspegic ili mzunguko wa damu uendelee vizuri; utapewa pia na follic acid (ni vidonge) japo sijuwi inasaidia nini. At the end utajifunguwa tu, kwa hiyo usikate tamaa. I am not a doctor; but I know this method exists. Should there be a Dr mdau, please check what I've written and contribute.

Merci beaucoup!
UMUHIMU WA UANGALIZI KIPINDI CHA UJAUZITO
Nini maana ya Uangalizi unapokuwa mjamzito?

Hii ni kutunza afya yako wakati wa mimba ili kuongezea tokeo la kupata mtoto aliye na afya. Haya ni baadhi ya mambo yotakayokuwezesha kuwa na mimba iliyo na afya na kujifungua vyema.

Anza kujitunza mapema na kwa kawaida. Hii inaweza husisha uchunguzi na vipimo kuhakikisha kijusi/mimba ina afya na vipimo kuhakikisha mwili wako unafanya kazi ipasavyo.

Hakikisha unakula chakula kilicho na protein, matunda, mboga, nafaka na madini ya calcium kijusi/mimba hupata chakula chote kutoka kwako, hivyo chagua chakula kitakachokupa afya. Jaribu kula mara tatu kwa siku na mara sita vipimo vidogo vidogo kama una matatizo ya uchefuchefu au kuhara.

Daktari wako anaweza kukushauri unywe vitamini zilizo na chuma (iron) na folic acid ili kusaidia kukuzuia kupatwa na upungufu wa damu. Vitamini hizi pia hulinda kijusi kutokana na magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo.

Jaribu kufanya kazi itakayokuhitajia nguvu zako kwa dakika 30 siku kadhaa kwa wiki. Mazoezi husaidia kupatia misuli yako nguvu itakayotumika wakati wa kujifungua na kuhufanya uwe na raha/rafaja wakati wa mimba.

Kuogelea, kutembea na mazoezi mengine hukufaa sana wakati wa mimba. Hakikisha umeongea na daktari wako kabla hujaanza zoezi lolote.

Kunywa aghalabu bilauri 6-8 za maji kila siku; na bilauri nyingine kwa kila saa litumiwalo katika mazoezi. Hili hukuzuia kuishiwa na maji mwilini, ambalo unaweza kusababisha mkazo hivyo kujifungua kabla ya muda wake kuwadia.

Pata/ongeza uzito ufoao. Kwa wanawake wengi, hii uwa kilo 11-16. Daktari wako atakusaidia.

Pata pumziko. Wakati wa mimba unaweza kupata mabadiliko ya hormon, ambayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya tabia yake (furaha na hasira) jichunge kimwili na kiakili.

Ambia daktari wako kama unatumiwa vibaya (abuse). Hili linapoendelea wakati wa mimba hukuweka wewe na kijusi hatarini ya kuharibika kwa mimba au kujifungua mtoto aliye na uzito mdogo isivyotarajiwa.

Ongea na daktari wako kuhusu kazi uifanyayo na usalama wa kazi hiyo. Wanawake wengi walio na mimba iliyo na afya wanaweza kuendelea na kazi yao ya kawaida hata wiki za mwisho za mimba.Mkuu charminglady
UNAFAA KUJIEPUSHA NA MAMBO HAYA KIPINDI CHA UJAUZITO

Usijiweke hatarini wakati wa mimba. Tumia wakati huu kufanya mabadiliko fulani maishani yako:

Acha kuvuta sigara* - uvutaji wa sigara wakati wa mimba huongezea hatari ya kuharibu mimba, kujifungua

kabla ya wakati ufaao, kuzaa mtoto aliye na uzito mdogo isivyotarajiwa, SIDS na matatizo mengine.

Usinywe pombe unywaji pombe wakati wa mimba huweza kusababisha kasoro ambazo haziwezi kuzuilika kama kupungukiwa na akili.

Usitumie dawa za kulevya Bangi, Cocaine, Heroin, Speed, PCP na dawa zingine za kulevya zaweza

kusababisha kuharibika kwa mimba, kuzaa kabla ya wakati ufaao na kasoro zingine. Mtoto anaweza pia kupata

Matatizo ya kusoma (kuelewa) na anaweza kuzaliwa akiwa mzoevu* kwa dawa hizi ongea na daktari wako kama wataka kuacha kutumia dawa hizi.

Punguza au acha kutumia kafeini ipatikanayo katika kahawa, chai, vinywaji chocolate na dawa ziuzwazo dukani.

Usile samaki, kuku au nyama nyingine ya mnyama kama haijaiva vizuri.

Jiepushe na kemikali zenye sumu kama kuua za wadudu, rangi, vyuma kama lead na mercury.(Bidhaa nyingi za nyumbani zilo na tahadhari kwa walio na mimba) Bidhaa hizi kama hauna uhakika.

Jiepushe na bafu ya pipa (tub) na Saunas za maji moto. Hizi huongezea hatari ya kuharibika kwa mimba na kasoro zingine za uzazi.

Usioshe au kushika kisanduku cha paka wako. Hili linaweza kuambukiza maradhi yanayoweza kusababisha kasoro za uzazi. Pia valia vifuko vya mikono (gloves) unapofanya kazi shambani au mahali paka wako huwa.
PREGNANCY AND MISCARRIAGE

A miscarriage is the loss of a fetus before the 20th week of pregnancy. The medical term for a miscarriage is spontaneous abortion, but the condition is not an abortion in the common definition of the term.According to the March of Dimes, as many as 50% of all

pregnancies end in miscarriage -- most often before a woman misses a menstrual period or even knows she is pregnant. About 15% of

recognized pregnancies will end in a miscarriage.More than 80% of miscarriages occur within the first three months of pregnancy. Miscarriages are less likely to occur after 20 weeks gestation; these are termed late miscarriages.

What Are the Symptoms of a Miscarriage?

Symptoms of a miscarriage include:

  • Bleeding which progresses from light to heavy
  • Severe cramps
  • Abdominal pain
  • Fever
  • Weakness
  • Back pain
If you experience the symptoms listed above, contact your obstetric health care provider right away. He or she will tell you to come in to the office or go to the emergency room.

What Causes Miscarriage?

The causes of miscarriage are not well understood. Most miscarriages that occur in the first trimester are caused by chromosomal abnormalities in the baby. Chromosomes are tiny structures inside the cells of the body which carry many genes. Genes determine all of

a person's physical attributes, such as sex, hair and eye color, and blood type. Most chromosomal problems occur by chance and are not related to the mother's or father's health.Miscarriages are also caused by a variety of other factors, including:
Infection
  • Exposure to environmental and workplace hazards such as high levels of radiation or toxic agents
  • Hormonal problems
  • Uterine abnormalities
  • Incompetent cervix (the cervix begins to widen and open too early, in the middle of pregnancy, without signs of pain or labor)
  • Lifestyle factors such as smoking, drinking alcohol, or using illegal drugs
  • Disorders of the immune system, including lupus
  • Severe kidney disease
  • Congenital heart disease
  • Diabetes that is not controlled
  • Thyroid disease
  • Radiation
  • Certain medications, such as the acne drug Accutane
  • Severe malnutrition
In addition, women may be at increased risk for miscarriage as they get older. Studies show that the risk of miscarriage is 12% to 15% for women in their 20s and rises to about 25% for women at age 40. The increased incidence of chromosomal abnormalities contributes to the age-related risk of miscarriage.There is no proof that stress or physical or sexual activity causes miscarriage.

How Is a Miscarriage Diagnosed and Treated?

Your health care provider will perform a pelvic exam and an ultrasound test to confirm a miscarriage. If the miscarriage is complete and the uterus is empty, then no further treatment is usually required. Occasionally, the uterus is not completely emptied, so a dilation and

curettage (D&C) procedure is performed. During this procedure, the cervix is dilated and any remaining fetal or placental tissue is gently

removed from the uterus. As an alternative to a D&C, certain medications can be given to cause your body to expel the contents in the uterus. This option may be more ideal in someone who wants to avoid surgery and whose condition is otherwise stable Polisi
HOW IS A MISCARRIAGE DIAGNOSED AND TREATED?

If a miscarriage was not confirmed, but you had symptoms of a miscarriage, bed rest may be prescribed for several days, and you may be admitted to the hospital overnight for observation. Blood work to determine the amount of a pregnancy hormone (hCG) is checked to

monitor the progress of the miscarriage.When the bleeding stops, usually you will be able to continue with your normal activities. If the cervix is dilated, you may be diagnosed with an incompetent cervix and a procedure to close the cervix (called cerclage) may be

performed if the pregnancy is still viable. If your blood type is Rh negative, your doctor may give you a blood product called Rh immune globulin (Rhogam). This prevents you from developing antibodies that could harm your baby as well as any of your future

pregnancies.Blood tests, genetic tests, or medication may be necessary if a woman has more than two miscarriages in a row (called repeated miscarriage). Some diagnostic procedures used to evaluate the cause of repeated miscarriage include endometrial biopsy (a

procedure involving the removal of a small amount of tissue from the lining of the uterus for study under a microscope), hysterosalpingogram (an X-ray of the uterus and fallopian tubes), hysteroscopy (a test in which the doctor views the inside of the uterus

with a thin, telescope-like device inserted through the vagina and cervix), and laparoscopy (a surgical procedure in which the doctor views the pelvic organs with a lighted device).

How Do I Know if I Had a Miscarriage?

Bleeding and mild discomfort are common symptoms after a miscarriage. If you have heavy bleeding, fever, chills, or pain, contact your health care provider right away. These may be signs of an infection.

Can I Get Pregnant Following a Miscarriage?

Yes. At least 85% of women who have miscarriages have subsequent normal pregnancies and births. Having a miscarriage does not necessarily mean you have a fertility problem. On the other hand, about 1%-2% of women may have repeated miscarriages (three or

more). Some researchers believe this is related to an autoimmune response.If you've had two miscarriages in a row, you should stop trying to conceive, use a form of birth control, and ask your health care provider to perform diagnostic tests to determine the cause of the miscarriages.

How Long Will I Have to Wait Before I Can Try Again?

Discuss the timing of your next pregnancy with your health care provider. Some health care providers recommend waiting a certain amount of time (from one menstrual cycle to 3 months) before trying to conceive again. To prevent another miscarriage, your health care

provider may recommend treatment with progesterone, a hormone needed for implantation in the uterus.Taking time to heal both physically and emotionally after a miscarriage is important. Above all, don't blame yourself for the miscarriage. Counseling is available to

help you cope with your loss. Pregnancy loss support groups may also be a valuable resource to you and your partner. Ask your health care provider for more information about these resources.

[h=3]Can a Miscarriage Be Prevented?[/h]Usually a miscarriage cannot be prevented and often occurs because the pregnancy is not normal. If a specific problem is identified with testing, then treatment options may be available.
Sometimes, treatment of a mother's illness can improve the chances for a successful pregnancy. Miscarriage Symptoms, Causes, Diagnosis, and Treatment
 
Kwa maelezo yako,hiyo mimba ni kama imeshatoka mabonge ya damu na maumivu. Ingekuwa bleeding ndogo ndogo, uwezekano wa mimba upo.lakini mabonge ya damu na maumivu juu, ni kama mimba imeharibika, cha muhimu asichoke kwenda hospitali kupata uhakika zaidi.
 
Pole kaka. I experienced something similar to that a few months ago tofauti ni kuwa mimi sikuona period zangu kabisa. I went to three different doctors na wote walisema mimba inatoka sikuamini coz nilikuwa nableed kidogo kidogo(spot bleeding bila maumivu yoyote). Finally nilipata maumivu makali sana ya tumbo na nikafanyiwa D & C ikawa ndo mwisho wa habari. Nakushauri umpeleke huyo dada hospital mapema iwezekanavyo coz unavyoelezea ni kama mimba imeshatoka.
 
Pole kaka. I experienced something similar to that a few months ago tofauti ni kuwa mimi sikuona period zangu kabisa. I went to three different doctors na wote walisema mimba inatoka sikuamini coz nilikuwa nableed kidogo kidogo(spot bleeding bila maumivu yoyote). Finally nilipata maumivu makali sana ya tumbo na nikafanyiwa D & C ikawa ndo mwisho wa habari. Nakushauri umpeleke huyo dada hospital mapema iwezekanavyo coz unavyoelezea ni kama mimba imeshatoka.
<br /> <br / Asante sana kwa ushauri wako mzuri na leo tutaenda tena hospital kwa uchunguzi zaidi japokuwa nakosa kuamini tena hospital maana napata majibu tofauti tofauti kwa the same problem.
 
Asante sana na ubarikiwe kwa maelezo yako,.leo natarajia kwenda hospital tena kwa uchunguzi zaidi.
 
Kajole,

Pole sana mkuu, pia mfikishie pole shemeji. Inatokea kwa wanawake wengi kupata kama damu ya hedhi akiwa na ujauzito mchanga (mwezi wa kwanza na/au wa pili), lakini huwa kidogo kiasi tu cha kustain chupi, na inaweza ikaendeana na siku zake za kawaida za hedhi au tofauti kidogo.

Lakini inapokuwa kiasi cha kutoa mabonge ikiambatana na maumivu makali ya tumbo la chini/uzazi...ni dhahiri hapo mimba inatoka na anahitaji kwenda hospitali haraka, aonwe na daktari wa magonjwa ya wanawake na amfanyie ultrasound kuhakikisha imetoka yote. Mimba zinapotoka zina tendency ya kubakiza uchafu kidogo (retained products of conception), na hizi husababisha bleeding kubwa sana ghafla au kwa muda mrefu. Na pia mimba nyingine haiwezi tunga mpaka hiyo product/uchafu utoke. Kama ipo basi atasafishwa (D & C), na hizo risk zote zitakuwa zimeondoka.
 
Pole sana mkuu, pia mfikishie pole shemeji. Inatokea kwa wanawake wengi kupata kama damu ya hedhi akiwa na ujauzito mchanga (mwezi wa kwanza na/au wa pili), lakini huwa kidogo kiasi tu cha kustain chupi, na inaweza ikaendeana na siku zake za kawaida za hedhi au tofauti kidogo.

Lakini inapokuwa kiasi cha kutoa mabonge ikiambatana na maumivu makali ya tumbo la chini/uzazi...ni dhahiri hapo mimba inatoka na anahitaji kwenda hospitali haraka, aonwe na daktari wa magonjwa ya wanawake na amfanyie ultrasound kuhakikisha imetoka yote. Mimba zinapotoka zina tendency ya kubakiza uchafu kidogo (retained products of conception), na hizi husababisha bleeding kubwa sana ghafla au kwa muda mrefu.

Na pia mimba nyingine haiwezi tunga mpaka hiyo product/uchafu utoke. Kama ipo basi atasafishwa (D &amp; C), na hizo risk zote zitakuwa zimeondoka.
Asante sana na pole zimefika kwa shemeji yako,.leo tunatarajia kwenda hospital,ntarudi na feedback kuwajuza zaidi.
 
The same happened to my wife pole sana, hi hali inawatokea sana wanawake wakati wa mimba changa miezi 2-3. na kwa jinsi inavyo onekana ni kwamba mimba imekwishatoka (miscarage). Maumivu ya tumbo la chini na kutoa damu ya mabonge ni dalili za miscarage. Pole sana mkuu.
 
Kajole, bado hujaanza safari ya hosp? pole sana,wahi hosp na dr afanye yanayohitajika asije akapata maambukizi.wakati damu inaanza kutoka wakati akiwa mjamzto,alipaswa aambiewe cha kufanya.pengine alihitaji bed rest. msijali,mungu ndo mgawa baraka ya watoto.mtafanikiwa kwa wakati ambao sio wa kuchelewa wala wa kuwahi. kila la kheri.
 
Pole sana! wahi kwa madaktari bingwa wa kinamama hiyo mimba yaelekea imekwisha toka na asipowahi kuchekiwa itamletea madhara mengine, kawaone madaktari mapema usiogope garama za kuwaona okoa maisha ya mwenzi wako.
 
Tafadhali onana na dokta anayehusika na masuala ya uzazi kwa akina mama kwa ushauri na vipimo zaidi.
 
Pole ndugu yangu, wadau wote wametoa ushauri mzuri ambao utanisaidia na mimi pia maana mchumba ame-experience the same thing leo asubuhi na ilinifadhaisha sana nashukuru kwa ushauri ambao nimeupata kupitia ujumbe wako.
 
Jaman asanteni sana wote kwa ushaur na mawazo yenu ambayo kwa kweli ni constructive sana na yametupa faraja na kutupungua maumivu kwa kiasi fulani. Ok mchumba ndio ametoka hospitali na majibu aliyopewa ni haya: kapimwa na ni negative-HAKUNA MIMBA wala tatizo lolote tena ktk mwili wake maana yake imetoka na kuhusu maumivu na dalili nyingine ni kwamba atakuwa anakaribia kupata HEDHI nyingne tena yan anarudi ktk mzunguko wake wa kawaida.

Mungu awabariki sana na kiukweli JF ni mambo yoooote!
 
Mkuu,

Hao madaktari hawakumfanyia UTRASOUND mkeo inavyo onyesha tayari mkeo ameshapata abortion kulingana na maelezo yako. Lakini kama utaenda Hospital Fanya ultrasound, i mean lower abdominal ultrasound to check for uterus size and other things.

Pia wanaweza kucheck Viginal kwa sababu inaweza kuwa incomplete abortion, Na kama ni complete abortion wataangalia then itakuwa saafi kabisa na tatizo hilo ina sababu nyingi. Katika suala la kuchoka ni kutokana na loss of blood so anatakiwa kupata fluid ya kutosha kama replacement

Note Utrasound ndo confirmation test vingine miyeyusho tu.
 
&lt;br /&gt; &lt;br / Asante sana kwa ushauri wako mzuri na leo tutaenda tena hospital kwa uchunguzi zaidi japokuwa nakosa kuamini tena hospital maana napata majibu tofauti tofauti kwa the same problem
Nenda mkuu then usisahau kurudi ulete riport mkuu.
 
Nenda mkuu then usisahau kurudi ulete riport mkuu.

Dio, asante sana kwa yote pia nilienda jana hosp na feed back nimeandika hapo juu. Nimeeleza alichosema doctor,.kwa kifupi amesema kuwa hana tatizo lolote kwa sasa ila ni kweli mimba imetoka kama wachangiaji weng walivyoona.

Pia kuhusu kuchoka, maumivu ya kichwa, kukojoa mara kwa mara anadai ni kwa sababu anakaribia kupata hedhi nyngne na kurudi ktk mzungu wake wa kawaida. Tunawashukuru wanaJF wote kwa kweli mnafariji na kusaidia sana kwa michango yenu.
 
Mkuu Hao madaktari hawakumfanyia UTRASOUND? Note Utrasound ndo confirmation test vingine miyeyusho tu.[/QUOTE] Mkuu Rodcones, mi sielewi ni kwanin madaktar wote 2naoenda wanakwepa kupiga ultrasound, hata jana 2memueleza ni vizur kama atapgwa ultrasound akasema atatumia kipimo cha kawaida tu na kikishndwa kutoa matokeo ndo atapga ultrasound (2mekuwa 2kielezwa hvyo na zaidi ya madaktar 3 2liowaona).

But 2tapima kwa kipimo hcho tarh 20/9 pale KCMC maana 2natarajia kwenda huko kwa kazi nyingine hvyo 2tafanya na hilo. Nazidi kuwaombea baraka na moyo huo huo wa kusaidiana.
 
Hebu jiulize, kwa nini mimba huwa zinaharibika? Unaweza kukadiria, kwa siku moja ni mimba ngapi huwa zinaharibika? Ukienda kumuuliza mtaalamu yoyote wa tiba, atakutajia sababu nyingi sana zinazopelekea mimba kuharibika ikiwemo ile ya mimba kuharibika yenyewe au kuharibiwa kwa makusudi. Lakini bado jibu halijajibiwa, kwa nini iharibike yenyewe au iharibiwe? Je, kuharibu (kutoa) mimba kuna ubaya gani? Huo ubaya unaouona wewe, unafikiri huyo anayetoa hiyo mimba anauona pia? Kama hauoni kwa nini?

Je, ni kweli kilicho kibaya/kizuri kwako na kwa wengine kiko hivyo? Kwa nini?. Jiulize tena. Hivi kama kusingekuwa na kuharibika au kuharibiwa kwa mimba dunia ingekuwaje? Bila shaka ingekuwa imemalizika kutokana na wingi wa watu. Nasema hivyo kwa sababu, ukiangalia idadi ya mimba zinazoharibika na zinazoharibiwa kwa siku moja zinaweza kuwa sawa au ni nyingi kuliko idadi ya watoto wanaozaliwa kwa siku moja.

Lakini si mimba zote zinaweza kuharibika au kuharibiwa, kuna zingine huharibika kirahisi sana hata kama mwenye nayo ataitunza kama yai, kuna zingine huharibiwa kirahisi sana hata kwa kunywa dose ya kawaida ya dawa au kwa kufanya kazi nzito kidogo, unafikiri ni kwa nini? Mfano; mama anaweza akawa anafanya kazi nzito kila siku, akanywa dawa za kila aina au akatumia kila njia kuharibu mimba aliyonayo ikiwemo ile ya kwenda kwa madaktari lakini mimba isiharibike, unafikiri ni kwa nini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom