Kitchen Party

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuhusu kitchen party. Nini maana yake? Je, ni sawa na unyago? Maana unakuta mwanamke anayefanyika kicheni pati, ni mjuzi wa mambo ya mapenzi na unyumba kuliko hata wanaomfundisha. Majuzi mtaani kwetu kuna mwanamke ambaye anaishi kama kimada na jamaa flani kwa miaka 7. Sasa wameamua kubariki ndoa yao. Cha kushangaza anafanyiwa kichen pati. Ya nini hasa?
 
Kwa nini hasa inaitwa "Kitchen party"?

Ni kwamba hakuna tafsiri yake kwa Kiswahili? Na kama haina tafsiri kwa Kiswahili, kwa nini?
 
Nasikia ipo kwaajili ya zawadi zaidi. . .maana hata kama ni mafunzo huwezi jifunza yanayohitajika ndani ya ndoa kwa masaa machache tu ndani ya siku moja, tena siku ambayo hata akili haijatulia.
 
Kichen Part za siku hizi zipo kibiashara zaidi. Yaani mwali apate vyombo.

Hakuna mafunzo yoyote, wizi mtupu.
 
kitchen party ni party ya jikon with nia ya kumfunda mwali vitu vya jikon ndio maana inafanywa hadharan na KUMPA ZAWADI zinazotumika zaidi jikoni, ila kuna nyingne inaitwa inner party yan party ya ndan hii hufanywa chumban tena na wamama wa karbu kabsa with nia ya kumfunda mwali mambo muhimu ya ndoa ambayo hayawez kuongelewa hadharan
 
Kwa nini hasa inaitwa "Kitchen party"?

Ni kwamba hakuna tafsiri yake kwa Kiswahili? Na kama haina tafsiri kwa Kiswahili, kwa nini?

kiswahili chake JIKO MTAWAZO. lengo lake ni kumpatia zawadi bibie japo huambatana na mafunzo.
 
kiswahili chake JIKO MTAWAZO. lengo lake ni kumpatia zawadi bibie japo huambatana na mafunzo.

Sasa kwa nini hizo shughuli huitwa kwa lugha ya kigeni ilhali zina jina kwenye lugha yetu?

Au kuziita hivyo ndo usasa zaidi?
 
Hata hiyo inner party ni uzushi tu. Kitu gani mabinti wa siku hizi hawakijui ktk 6x6?
 
Kuna bed party pia siku hizi kwa ajili ya wanaume.Ni usasa tuliounakiri bila kutazama maudhui, na kama tujuavyo nguo ya kuazima haisitiri ******..tumeongeza na yetu ...kama zawadi na nasaha za kizushi kwa muda mfupi halafu the rest watu wanaserebuka! Sijui kama mhusika atakuwa ameelewa kwa kipndi kifupi mbaya zaidi ukute tayari ni nunda..duh
 
Hii bed party ni sawa na bachelor's party?
 
Hiyo bed party itakuwa pouwa ukiletewa na mtu wa kumdunda mara ya mwisho kabla ya kuoa. Is kuweka mapazia around huku watu wanasubiri.

Itakuwa lazima ina rahaaaaa
 
i dont see the meaning of it na sidhani kama ina umuhimu ni mambo ya kuiga tu
 
Back
Top Bottom