Kitanzi kwa wafanyakazi nchini: Pensheni sasa mpaka ufikie miaka 55

Wewe acha kutuogopesha!! Mimi ninampango wa kwenda kuivuta next week..
 
ulikuwa na ulazima gani wakuanzisha thread mpya wakati kuna thread kama hii hapo chini?
 
Majungu fitna na wivu wa mifuko mingine baada ya NSSF kuonekana ni tishio katika uwekezaji.

Kuna jamaa yangu aliupopata nafasi ya kusoma akapewa chake full, niambieni ni mfuko gani ukitaka chako unapewa bila zengwe?

NSSF ndio mfuko wa aina yake maana ndani ya miezi 6 unakula full fungu lako tokea mwajili wako alipopeleka vithibitisho vya michango yako niambieni shirika gani lina speed kama hiyo?

NSSF muda wowote bila zengwe ukitaka kwenda kucheki michango yako unapata na full detail tena umekaa kwenye kiyoyozi bila urasimu kama mashirika mengine mara printer mbovu mara sahihi ya bosi ni shirika gani lipo hivyo?

NSSF ndio shirika pekee linalochangia maendeleo ya nchi kama wahisani kwa majengo. elimu na miradi mbali mbali ni shirika gani lingine lipo hivyo?

Narudia, WIVU, FITNA, MAJUNGU ni jadi ya watanganyika. mwacheni Dr. Rama achape kazi.

Shame.
 
Naru kuwa mpole hao watu wapo ata maishani mko bize na mambo ya maan anaanza kutupotezea!
 
Jamani nssf wapo poa.according to the research by audit firm,inasema nssf wanaweza kujiendesha miaka 15 bila kupokea michango kwa wanachama na kuwalipa bila kufilisika.halafu leo hii unasema wamefilisika.nssf cyo serikali ya bongo na uwekezaji wao una manufaa kwa watz cyo ccm.

If you can believe that you'll believe anything you are told!
 
Nimepanga kuchukua hela yangu comes 2015 nikasome masters! sasa hawa Jamaa wanataka kuniangusha sitakubali na haikubaliki! Tupinge kwa nguvu zote. Nisipofika hiyo age nani atasumbukia hiyo hela? wanataka kutudhulumu wanyonge hatutakubali.
 
Nssf ipo juu jamani siyo kama masharika haya mapya yaliyokuja sasa hvi. Nssf ina huduma nyingi zaidi ya hyo ya kulipa wastaafu.
Msiandike vi2 msivyönauhakika navyo. Nyambafu.

Read between lines from the thread,you will understand.
 
Naru kuwa mpole hao watu wapo ata maishani mko bize na mambo ya maan anaanza kutupotezea!
Tume ya katiba nae naona anaanza kunitafuta. Inauma sana yaani j'3 nilkuwa naongea na rafiki yangu mmoja yeye ni mfanyakazi wa serikalini na ana 48yrs akanambia anataka aache kazi ili angalau apate mafao yake ya NSSF yamsaidie kufungua biashara maana anadai mpaka sasa hana nyumba, watoto hawapati elimu bora na anazidi kuwa masikini. Leo hii hawa wapumbavu wanakuja na porojo za namna hii.
 
Last edited by a moderator:
Nimepanga kuchukua hela yangu comes 2015 nikasome masters! sasa hawa Jamaa wanataka kuniangusha sitakubali na haikubaliki! Tupinge kwa nguvu zote. Nisipofika hiyo age nani atasumbukia hiyo hela? wanataka kutudhulumu wanyonge hatutakubali.

Ndio tabia yao.
 
Sikulaumu kumtukana huyo "LOVI MEMBE" sio kosa lako ni kosa la kupotea kwa maadili katika taifa, viongozi wa kidini wote wamekuwa wanasiasa wamekimbia masinagogi wakatimkia kwenye ubunge, sasa unafikili taifa litapona?

maadili wamekosa wale wanaowaingilia wake zao kinyume na maumbile
 
Hii sheria ni kandamizi na haiendani na wakati tuliopo. Wanadhani kila mtu anafanya kazi serikalini? Nani anataka kutumikishwa hadi awe na umri wa miaka 55? Hawa wanaojaribu kufikiria kuzuia watu kuchukua pension zao hawana mawazo ya kijasilia mali na wana akili mgando. Kwa mfanyakazi mwenye mkataba wa miaka mitano na ameanza kazi akiwa na miaka 25 ina maana akifikisha 30 anamaliza mkataba wa kazi na kujikita katika biashara. Je asubirie kwa miaka 25 ndio aje alipwe pensheni yake? Huu ni uwendawazimu wa serikali ya CCM, hawana mawazo ya 21st century yenye kujikita zaidi kwenye kujiajili baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi ya kuajiriwa. Mfano mimi mzigo wangu saizi unakaribia 30M na lengo langu ukifika 40 miaka miwili ijayo niachane na kazi za kuajiliwa nikajasilie mali na nitakuwa nimebakiza miaka 20 kufika 55...
 
Kiukweli Pensheni ina umuhimu wake pia,Ila ishu hapa ni kwamba wachangiaji tunatakiwa tufaidi michango yetu wakati bado tuna nguvu na akili active.Inabidi mifuko iwe na options za kutukopesha kwa riba nafuu kwenye fedha zetu za michango ili tufanye issue zingine zenye tija while we can.
 
Hii nimeikuta kule Mwanahalisi;

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII

MAELEZO KUHUSU TAARIFA "CAG: NSSF HATARINI KUFISILIKA" ILIYOCHAPISHWA NA GAZETI LA WIKI LA MWANAHALISI TAREHE 18, APRILI 2012
UTANGULIZI Mnamo tarehe 18 Aprili, 2012, Gazeti la MwanaHALISI lilichapisha habari kwenye ukurasa wa 1 na wa 2 yenye kichwa cha habari ‘’CAG: NSSF HATARINI KUFILISIKA’’. Taarifa hii imezungumzia mambo makubwa mawili ambayo ni:


1) Serikali kushindwa kulipa deni la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma yaani UDOM

2) NSSF ipo hatarini kufilisika


UKWELI KUHUSU MADAI HAYO
Deni la Serikali Mnamo tarehe 20 Februari 2012, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali yaani Controller and Auditor General (CAG) aliwasilisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mwaka wa 2010/2011 kwenye Bodi ya Wadhamini ya NSSF.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi, kwa mara nyingine tena NSSF ilipata Hati Safi ya Hesabu yaani Unqualified Opinion. Hati hiyo ilitolewa baada ya ukaguzi wa kina ambao ulihakiki Hesabu za Shirika ikiwa ni pamoja na madeni ambayo NSSF inaidai Serikali kutokana miradi mbalimbali ambayo Shirika imeitekeleza kwa njia ya mkopo kwa Serikali.
Katika taarifa hiyo ya Ukaguzi, hakuna hata sehemu moja ambayo CAG ameripoti kuwa NSSF ipo hatarini kufilisika kwa sababu ya kutolipwa na Serikali au kwa sababu nyingine yoyote ile. Kimantiki, haiwezekani CAG atoe Hati Safi ya Hesabu kwa NSSF yaani unqualified opinion, halafu katika taarifa yake aripoti kuwa Shirika hilo lipo hatarini kufilisika! Hivyo basi SI KWELI kuwa CAG ameripoti kwenye taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za NSSF kuwa Shirika lipo hatarini kufilisika.

Kinyume na taarifa iliyochapishwa kwenye Gazeti a MwanaHalisi, historia inaonyesha kuwa Serikali imekuwa ikilipa madeni yake yanayotokana na miradi yake mbalimbali. Kwa mfano, mradi wa mabweni ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mabibo yaliyomalizika mwaka 2001. Gharama za mradi huo zilikuwa shs. 16.47 bilioni na riba ya mkopo huo ilikuwa shs. 9.7 bilioni. Napenda kuthibitisha kuwa Serikali imelipa deni LOTE ambalo lilimalizika mwezi March 2012. Hali kadhalika, mradi wa nyumba 252 za Dodoma zilizouzwa kwa Serikali mwaka 1994, ziliuzwa kwa shs. 2.5 bilioni na riba ya shs. 4.455 bilioni. Tunapenda tena kuthibitisha kuwa deni LOTE hilo lililipwa mwaka 2002.


Kuhusu deni la ujenzi wa UDOM, Serikali haijaanza kulipa deni hilo kwa vile kuna mgogoro (dispute) baina ya NSSF na Serikali kuhusu shs. 1.5 bilioni. Mara tu muafaka utakapopatikana deni hilo litalipwa kwa mujibu wa mikataba.


NSSF hatarini kufilisika


Kuhusu dai kuwa NSSF ipo hatarini kufilisika, hii pia si kweli. Kipimo kizuri cha uwezo wa kifedha wa mfuko (financial soundness) ni Tathmini ya Mfuko yaani Actuarial Valuation ambayo inafanywa kila baada ya miaka 3. Kwa upande wa NSSF, Actuarial Valuation ya mwisho ni ya mwaka 2010. Zoezi hili lilifanywa na Kampuni ya xxxxxxx kutoka Canada ambayo mwaka xxxxx iliteuliwa na Shirika la Kazi Duniani yaani International Labour Organisation (ILO) kufanya Tathmini ya Shirika la NSSF. Matokeo ya Actuarial Valuation inayoishia mwaka 2010, yanaonyesha kuwa Reserve Ratio ya NSSF ni 6.8. Tafsiri ya matokeo haya ni kuwa NSSF inaweza kumudu kulipa mafao YOTE kwa wanachama na kulipa gharama ZOTE za uendeshaji kwa miaka 6.8 bila kuingiza hata senti moja kwa maana ya ukusanyaji wa michango au mapato kutokana na vitega uchumi. Kwa mujibu wa vigezo vya Kimataifa, Reserve Ratio ya miaka 3 ni ushahidi tosha kuwa Taasisi husika ya Hifadhi ya Jamii ina hali nzuri sana kifedha. Kwa upande wa NSSF, Reserve Ratio ni 6.8.



HITIMISHO Taarifa iliyotolewa na Gazeti la MwanaHalisi imepotosha ukweli uliopo kwenye ripoti ya CAG na imetoa taarifa ambazo si za kweli kuhusu uwezo wa Shirika la NSSF kifedha. Napenda kuwataarifu wanachama wetu wote pamoja na wadau wote wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa Shirika lao bado lina uwezo mkubwa sana kifedha kama ambavyo Actuarial Valuation inavyoonyesha. Kwa upande wa deni la ujenzi wa UDOM, deni hilo litalipwa mara tu mgogoro uliopo hivi sasa utakapotatuliwa.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA
HUDUMA KWA WATEJA

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF) PO BOX 1322 DAR ES SALAAM
 
Back
Top Bottom