KITABU CHA MAY; A Long Way Gone(Historia Ya Kweli Ya Mdhara Ya Vita).

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena katika utaratibu wetu wa kushirikishana kitabu cha kujisomea kila mwezi. Kuanzia mwaka 2013 tumekuwa na utaratibu huu na karibu kila mwezi umetumiwa kitabu kizuri cha kujisomea. Je unasoma vitabu hivi vinavyotumwa? Kama ndio naomba uniandikie ni jinsi gani maisha yako yamebadilika kutokana na vitabu ulivyosoma mpaka sasa. Niandikie kwenye email makirita@kisimachamaarifa.co.tz Pia kama ulisoma vizuri kitabu cha mwezi uliopita niandikie ni mambo gani mazuri uliyojifunza kwenye kitabu kile. Nasubiri kusikia kutoka kwako.
Mwezi huu wa tano nilitoa zawadi ya kitabu PERSONAL MBA kile hakikuwa kitabu cha mwezi katika utaratibu wa kutuma vitabu, bali ilikuwa ni zawadi kwa wasomaji wote kwa imani kubwa mliyoijenga kwa mtandao huu wa AMKA MTANZANIA.

Kitabu cha kusoma mwezi huu wa tano ni kitabu A LONG WAY GONE. Kitabu hiki kinahusu historia ya vita nchini Sierra Leone. Historia hii inaelezwa na Ishmalel Beah ambaye kwa kipindi hiko cha vita alikuwa mtoto wa miaka 11.
Mimi binafsi sijawahi kushuhudia vita, ila naona tu kwenye vyombo vya habari. Lakini niliposoma historia hii ya kwenye kitabu hiki, niliona kama mimi nipo kwenye vita ile. Ni hadithi iliyojaa simanzi kubwa kuhusu madhara ya vita hasa kwa wanawake na watoto. Kuvurugika kwa familia na kuona ndugu zako wakiuawa kinyama mbele ya macho yako. Ni jambo la kusikitisha sana.
Kama nilivyoandika, vita hii ilianza Ishalel akiwa ni mtoto wa miaka 11, alitumia miaka miwili akikimbia kila siku ili kuokoa maisha yake. Hapo hakuwa na taarifa za familia yake iko wapi, kila mtu alitawanyika baada ya mashambulizi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza. Ishmalel alikimbia na kutembea usiku na mchana kwenye vijiji mbalimbali kutafuta usalama wa maisha yake. Yeye na watoto wengine hawakuwa na chakula wala pa kulala, yalikuwa ni maisha ya kuhangaika tu.
Vita hii ilikuwa ni kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la waasi. Waasi walikuwa wakiua watu kinyama na kukamata vijana na watoto na kuwafanya wapiganaji. Ishmalel alikimbia sana asiingie mikononi mwa waasi hawa. Katika kukimbia kwake Ishmalel na wenzake walijikuta walifanikiwa kufika kwenye kambi ya jeshi la serikali na hapo wakajua maisha yao yamepona. Kumbe hawakujua mambo yangekuwa magumu zaidi.
Mwanzoni walipofika kwneye kambi ile maisha yalikuwa mazuri, ila baadae kambi ile ilikaribiwa sana na waasi na wanajeshi wengi waliuawa na hivyo hakukuwa na jinsi bali kumchukua kila mtu anayeweza kupigana afanye hivyo. Hapa ndipo Ishmalel aliyekuwa na miaka 13, pamoja na watoto wengine, wawili walikuw ana miaka 7, walipoanz akupewa mafunzo ya kivita. Walipewa silaha ambazo zimewazidi kimo, walifundishwa kwa mbinu za chuki na hivyo akili zao changa zilipokea kila kitu walichoambiwa.
Ili kuondolewa hofu ya kuua watu, walipewa madaw aya kulevya na kuvuta bangi. Ishmalel anaeleza ni jinsi gani alikuwa akiweza kupita siku kadhaa bila ya kulala au hata kusinzia. Anaeleza ni jinsi gani baadhi ya nyakati alikuw akama anachanganyikiwa na kujikuta anapiga risasi hovyo.
Kitabu hiki kina mambo mazuri sana ya kujifunza na mengine yanasikitisha na unaweza hata kulia. Moja ya maeneo yanayosikitisha ni Ishmalel alipewa taarifa kwamba mama yake na mdogo wake wameonekana kwneye kijiji fulani. Alifurahi sana na akaanza safari ya kuelekea kijiji hiko. Ilikuwa ni safari ya usiku na mchana na ilichukua siku kadhaa. Alipokuwa amekaribia kabisa kijiji kile alisikia milipuko kuangalia ni waasi walikuwa wamekivamia na walichoma kila kitu kwneye kile kijiji.
Ushiriki huu wa kivita katika umri mdogo ulimletea madhara makubwa sana ya kisaikolojia Ishmalel, ilibidi apitie kipindi kirefu cha matibabu na ushauri ili kuweza kurudi katika hali ya kawaida.
Nisiseme mengi hapa ushindwe kukisoma kitabu hiki muhimu. Kisome kitabu hiki, mwanzo mpaka mwisho na utajifunza vitu vingi sana na umuhimu wa kutunza amani tuliyonayo kama nchi.
Kuna watu huwa wanasema Tanzania inabidi tupigane kidogo ndio tuheshimiane, hii ni kauli ya mtu ambaye hajawahi kuyaonja machungu ya vita. Vita isikie kwa mwenzako, ila inapokuwa kwako hiyo ni habari nyingine na sio habari nzuri kabisa. Tushirikiane kuilinda amani ya nchi yetu, kwa sababu zozote zile, tukaingia kwenye vita, watakaoumia sio watu waliosema tuingie kwenye vita, bali watoto wasiokuwa na hatia na masikini wasiojua maisha yao yanakwendaje. Nchi ikishaingia kwneye machafuko hata habari ya mafanikio utaisahau, kitu muhimu kwako itakuwa ni kuokoa maisha yako kwanza. Hutahitaji kuboresha biashara yako au kazi yako, hutahitaji kuboresha maisha yako zaidi, utakachohitaji ni kuhakikisha upo hai.
Kupata kitabu A LONG WAY GONE bonyeza hayo maandishi, kipakue na kisome. Pia tuma kitabu hiki kwa watu wote unaowafahamu na wahamasishe sana kukisoma.
Soma kitabu hiki na tushirikiane wote kuilinda amani ya nchi yetu, ndio kitu pekee kinachoweza kutufanya tufikie malengo na mipango tuliyojiwekea kwenye maisha yetu.
Nakutakia kila la kheri katika usomaji wa kitabu hiki na kufanyia kazi yale ambayo utajifunza.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
 
Back
Top Bottom