Kitabu cha kumnunulia Kikwete ni: "Dead Aid" by Dambisa Moyo

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Katika pitapita mitaani nimekumbana na kitabu hiki. Nikaona labda JAMIIFORUMS ijitolee kununua hiki kitabu na apewe Rais wetu.

Pia kuomba idhini kiandikwe kwa Kiswahili na kuuzwa Tanzania na baadhi kwa Kiingereza ili watu wajue madhara ya misaada na jinsi madhara yasivyosaidia Africa. Hasa wale wa Rukwa waliotukana kuwa mnamwamndama Rais kwa kuleta misaada.

Someni hapa chini na mjitahidi kukinunua na kusoma:-

_________________________________
Dambisa Moyo is an economist and the author of Dead Aid: Why Aid is Not Working and How There is a Better Way For Africa, published in the spring of 2009. The book offers proposals for developing countries to finance development, instead of relying on foreign aid. It became a New York Times bestseller upon its release in the United Statesand remains a bestseller amongst Political and Economic books.Her book is published internationally by Penguin Books and in the United States by Farrar, Straus & Giroux.

In May 2009, TIME Magazine named Moyo one of the world's 100 most influential people. Reception Moyo's ideas are similar to those held by the Rwandan Government and President Paul Kagame. He says that "Dead Aid has given us an accurate evaluation of the aid culture today" Kagame also invited Moyo to Rwanda to discuss her thesis and bought copies of the book for his entire cabinet.
The President of Senegal, Abdoulaye Wade has expressed similar views on aid, with a particular focus on reducing protectionism and lowering trade barriers. Kofi Annan has said that "Dambisa Moyo makes a compelling case for a new approach to Africa".

The Cato Institute say that "no individual today is more effectively challenging the foreign aid establishment and the harm it inflicts on Africa than Dambisa Moyo"

Maelezo zaidi someni WIKIPEDIA au WWW yake:
 
Last edited by a moderator:
GT,
Huko naona wewe na Makamba mmefanya kweli kwa kumpaka mama.
Anachokisema mama ni kitu kweli, ila tatizo kubwa kwa wanasiasa na Wachumi, kila kitu huwa au hakiwezekani au chahitaji capital. Kama mngelikisoma kitabu na kufahamu kwa nini Kagame anakitumia sana kitabu hiki, labda mngeelewa maana ya kitabu.
Kuna sehemu ya picha, Mwanakijiji kaweka picha ya SHIMO, na shimo hilo liko Dar na hakuna wala aliyezungushia mbao kuzuia watu/magari yasidumbukie humo. Ilibidi msamaria mwema aweke TV karibu na shimo ili kuashiria magari yasidumbukie. Ukifuatilia sana, utakuta hata shimo wanasubiri MSAADA wa tape na mbao kutoka Sweden ili waweze kuzungushia hilo shimo. Kwa kuendekezwa na misaada, Tanzania tumelemaa kama mtoto wa bibi au kitindamimba......
Kuna haja Tanzania aje Rais mkorofi kama Mkapa ila anaipenda Tanzania na si kuiibia. Rais atakayesema "...Sitaki nisikie kuwa hili haliwezekani...."

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Mkuu Sikonge,,, unadhani mkulu ana muda wa kusoma kweli hii kitu!?
 
Mkuu Sikonge,,, unadhani mkulu ana muda wa kusoma kweli hii kitu!?
nakumbuka katika mikutano yake aliwahi kusema anapenda kusoma vitabu? hasa hasa ya kijeshi kama sikosei, na kwa kuwa kasomea uchumi basi niwazi anasoma vitabu vinavyo husiana na jambo hilo?
 
Kwa nini tuende mbali. Kitabu cha "KULI" kinatosha kuelewa nini kinaendelea Tanzania na Africa at large na kuonyesha ni kiasi gani "OUR LEADERS FAILED US"
 
Inabidi kwanza nikisome kitabu hicho....lakini mara nyingi mimi huamini kwamba matatizo ya Waafrika wanayajua Waafrika wenyewe..Kitabu hiki kinaweza kurudia mambo yote tunayojadili hapa JF kila siku.
 
Kwa nini tuende mbali. Kitabu cha "KULI" kinatosha kuelewa nini kinaendelea Tanzania na Africa at large na kuonyesha ni kiasi gani "OUR LEADERS FAILED US"

Naam "yana mwisho haya" alisema Kuli!
 
Mkuu Sikonge,,, unadhani mkulu ana muda wa kusoma kweli hii kitu!?

Si vibaya kama akinunuliwa na apewe rubani wake na mara anaposafiri, basi kwenye ndege apewe na asome. Sidhani kama safari nzima huwa anacheka safari nzima kutoka Tanzania-USA-Tanzania. Anunuliwe tu na apewe na kumwambia kuwa "Wanaoitakia mema Tanzania, wanataka TANZANIA IWE HURU KWELI". Hii Misaada au AIDS au CIDA kwa kweli inatuuwa sana kwa ndani.

Pia si vibaya kama Wabunge na Mawaziri na wao wakaSISITIZWA kukipitia hiki kitabu na kukisoma. Mie mwenyewe ntakitafuta kwa udi na uvumba nikisome na kujua mama anaTETA nini.
Mtanzania, nunua upate kitabu cha kusoma wakati unakuja kunitembelea Sikonge huku......
 
nakumbuka katika mikutano yake aliwahi kusema anapenda kusoma vitabu? hasa hasa ya kijeshi kama sikosei, na kwa kuwa kasomea uchumi basi niwazi anasoma vitabu vinavyo husiana na jambo hilo?

Mkuu Ingekuwa hivyo, tungeshasikia walau mara moja kamwambia rubani wa ndege ageuze arudi nchini!
 
Katika pitapita mitaani nimekumbana na kitabu hiki. Nikaona labda JAMIIFORUMS ijitolee kununua hiki kitabu na apewe Rais wetu.

Pia kuomba idhini kiandikwe kwa Kiswahili na kuuzwa Tanzania na baadhi kwa Kiingereza ili watu wajue madhara ya misaada na jinsi madhara yasivyosaidia Africa. Hasa wale wa Rukwa waliotukana kuwa mnamwamndama Rais kwa kuleta misaada.:

Sikonge, hata umpelekee na walimu wa walimu kumjuza na kumfunza, JK sikio la kufa...
Hata kikitafsiriwa kwa 'Kikwere' JK sio kutosoma tu, haelewi hata akisoma, akisomewa na akifunzwa ni mtu aliyekoma kuelewa. Naweza sema ni 'tasa' wa kuelewa
 
Kwa nini tuende mbali. Kitabu cha "KULI" kinatosha kuelewa nini kinaendelea Tanzania na Africa at large na kuonyesha ni kiasi gani "OUR LEADERS FAILED US"

Hata "pepo ya mabwege" ya Harrison Mwakyembe imekaa vizuri kama ni mtu wa kuelewa. Nyerere alifundisha, alihubiri,alihutubia na hawakumwelewa! Itakuwa hayo maarifa yaliyofichwa kwenye kitabu? Thubutu! mnunulie uone.
 
mi nadhani tumnunulie kitabu tumnunulia biblia takatifu pamoja na quran tukufu nadhani mjomba akivisoma mara kwa mara ataweza kupata huruma na mateso wayapatayo watanzania hasa wale wa kule north mara
 
Kazi kwelikweli...sio wote huwa tunasoma vitabu vyenye page zaidi ya tano. Tunasikiliza mziki wa asili kama sangula na mchiriku, Watching TV na kuchat kwa sms. Kusoma ni taabu kidogo.Nimeona aibu jinsi Al Gore anavyojituma kutafuta knowledge kwa kusoma...duuuh kumbe leaders read alot!!
 
Ina maana JK akisoma hicho kitabu na kufuata yaliyoandikwa, Tanzania itakuwa inaendelea?

Tusidanganyane hapa. Matatizo yetu ni sisi wenyewe na kama tungekuwa na vichwa vizuri tungeendelea bila au kwa kutumia misaada.
 
Sidhani kama anahitaji kusoma vitabu vya akina Dambisa ndo aelewe athari za misaada.
 
Bill Clinton aliwaambia WaRwanda kuwa:

"Kama mkikaa mezani na kuongea, hakuna uhakika kama mtakubaliana, ila msipokaa hiyo ni asilimia 100 kuwa hamtapatana..."

Hakuna anayesema tukimpa asome atabadilika. Ila kutokufanya hivyo ni asilimia mia moja kuwa ataendelea kwenda kufungua hotel za Kempinski na huku akidanganywa kwenda kufungua madaraja ambayo hayajaisha bado.

Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. Labda hiki kitabu chaweza kuwa ndiyo tundu letu bovu!!!!!
 
Back
Top Bottom