Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Heshima sana wanajamvi,
Gazeti la Raia mwema limekuwa likichapisha makala ya Kachero wa jeshi la wananchi (JWTZ) aliyetekwa Uganda pamoja na wanajeshi wengine wawili ambao waliuwawa na majasusi wa Idd Amin kabla ya vita vya Kagera.
Nimekuwa nikifuatailia sana makala hizo kila Jumatano gazeti la Raia Mwema linapotolewa bahati mbaya kila nikimaliza kusoma naachwa na kiu kubwa kiasi naomba siku ziende haraka ili niweze kusoma makala zingine.
Natoa rai kwa wachapishaji wa gazeti la Raia Mwema kutuelekeza wapi tunaweza kupata nakala ya kitabu badala ya kuendelea kututesa na kutuacha na kiu isiyokuwa na sababu za msingi.
Nawasilisha.