Kitabu cha hadithi ya Kiswahili ya Willi Gamba kinahitajika haraka

Dada Cheusi;
Naona kama kwa level na umri uliofikia haustahili tena kusona vitabu au novel za kiswahili, waachie kindergatten na shule za Msingi.
Nakushauri badala yake usome novel za James Hardley Chase zipo nyingi mtaani zimezagaa, utapata satsfaction mara 10 zaidi ya kurudia kusoma hiyo novel ya kiswahili.

Kumbuka pia kuwa Musiba alikuwa anaiga utunzi wa Chase, ndiyo maana akaweza kutunga novel zilizoweza kukuvutia. Just imagine kusoma novel za yule aliyeigizwa na Musiba sijui itakuwaje. Try it out and you will tell me.

Umenikera sana na dharau zako....eti za kiswahili waachie chekechea....kwanini usifikiri hata za kina chase wanasoma chekechea wa kwao? Ina maana ukishalevywa na Chaseism basi vya nyumbani vya kuchambia eti?
 
Kikwetu kwetu tuthamini vya kwetu .Kila mtunzi ana vionjo vyake awe chase au Sheldon kuna ladha tofauti. Nilipata kusoma novel ya vincent teresa "my life in the mafia "ni true story ukisoma god father ambayo ni fiction zote nilizipenda kutokana na ueledi wa watunzi. Musiba ana nafasi yake katika fasihi ya tanzania kama sio duniani kote kwa wanaojua lugha yetu adhimu.
Cha msingi tumpe ushirikiano muhitaji na si kumkatisha tamaa ni sawa mtu ana hamu na togwa kisha wamwambia anywe soda.
 
Hicho ni "Njama". Kama ingekuwa nchi nyingine, marehemu Musiba angekuwa ni milionea ($$ wise).

Sio kweli,kwenye njama hakuna mhusika yeyote mwenye jina la Tausi.kuhusu musiba kuwa milionea ni kweli,Tanzania bado hatuna utaratibu mzuri wa kuwafanya watu wenye vipaji wafaidike navyo ipasavyo.
 
Kuhusu la uhusika kwa upande wa wanawake njama alikuwapo zawadi na pia veronica amadu toto la freetown na alikuwa mpelelezi, hofu alikuwa mtoto nyaso na kikosi cha kisasi alikuwa tete na mwadi tausi ndo kikomo nadhani hayo ndio nayakumbuka coz ni miaka mingi.
 
Huyo anataka kitabu cha "HOFU" au "KUFA NA KUPONA" maana kati ya vitabu hivyo kuna warembo Nyaso na Tausi maana mwenyewe nimesoma miaka 17 iliyopita.
Hicho.ni kikomo kuna willy na tausi
Njama kuna willy na.veronica amadu
Hofu kuna willy na nyaso
kikosi.cha kisasi kuna willy na tete
 
Hicho ni "Njama". Kama ingekuwa nchi nyingine, marehemu Musiba angekuwa ni milionea ($$ wise).
Ni.kikomo.sio njama..njama kuna.veronica amadu na zabibu hakuna tausi
Vinapatikana wapi? Hiyo ndo swali la msingi
Hivyo vitabu ni ngumu sana kuvipata madukani hususan dar kwani vilipigwa marufuku wakati wa nyerere kuwa vinafundisha mbinu za kijasusi. Arusha niliwahi kukiona njama na hujuma. Dar nimezunguka sijaviona
 
Dada Cheusi;
Naona kama kwa level na umri uliofikia haustahili tena kusona vitabu au novel za kiswahili, waachie kindergatten na shule za Msingi.
Nakushauri badala yake usome novel za James Hardley Chase zipo nyingi mtaani zimezagaa, utapata satsfaction mara 10 zaidi ya kurudia kusoma hiyo novel ya kiswahili.

Kumbuka pia kuwa Musiba alikuwa anaiga utunzi wa Chase, ndiyo maana akaweza kutunga novel zilizoweza kukuvutia. Just imagine kusoma novel za yule aliyeigizwa na Musiba sijui itakuwaje. Try it out and you will tell me.
Kwa nini Jamii forum Hamna kitufe cha dislike? Itaokoa muda WA kuandika kama hivi!
 
Dada Cheusi;
Nakushauri badala yake usome novel za James Hardley Chase zipo nyingi mtaani zimezagaa, utapata satsfaction mara 10 zaidi ya kurudia kusoma hiyo novel ya kiswahili.
Napata mashaka kuamini kama kweli wewe ni msomaji wa novel na ni kweli umesoma novel za Chase na Elvis Musiba za kutosha,story telling style za Chase na Musiba ni tofauti sana na wala huwezi kuwalinganisha na hata ladha ya vitabu vyao ni tofauti kila mtunzi kati ya hao wawili ana ladha yake.Pia usitake kumuaminisha Mtoa uzi kwamba James H Chase ndio mkali katika utunzi wa novel, hiyo inaonyesha kabisa hujakutana na novel za wakali mkuu.Tafadhali jaribu kutafuta novels za hawa wachache kidogo halafu fanya ulinganifu na novel za James Chase (Robert Ludrum,Edgar Wallace,Andrew Neiderman, Ian Fleming,Sydney Sheldon)kisha rudi hapa umshauri tena mtoa mada vitabu vya kusoma.
 
Musiba aliandika vitabu vingi vinavyohusu Will gamba mplelezi mashuhuri barani africa ambaye alikuwa anateketeza mfumo wa kijasusi wa kuwaua wapigania uhuru enzi hizi -- kati ya hivi unataka kibabu kipi?

Kikomo
Njama
Kikosi cha kisasi
Hujuma.
Mie nataka vi3 kati ya ivyo.mana naskia musiba ni hatar katika utunzi.
 
Hicho ni "Njama". Kama ingekuwa nchi nyingine, marehemu Musiba angekuwa ni milionea ($$ wise).
Hata hivyo Musiba alifariki akiwa milionea. Kitaaluma alikuwa Mhasibu aliyeanzia TAZARA. Baadaye akaondoka na kwenda kwingine ambako alifanikiwa sana kiuchumi. Aliwahi kufikia kuwa Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture
 
Kikosi cha kisasi nilikisoma nikiwa primary nilikuwa natumia kibatari kusoma ucku ikifika asubuhi pua nyeusi kwa moshi wa kibatari....ukisoma hicho kitabu hutaki kuacha...vp nani anavitabu vya Joram Kiango
 
Kama kuna Mwl au mwanfunzi unayemjua yupo MINAKI high school mwambie akuchekie kama bado zipo kwenye maktaba yao ile kuukuu, nilizisoma mara ya mwisho 2009 nilipomaliza kidato cha sita pamoja na safari ya GULIVER na NCHI YA VIJITU.

Vyote nya Wile Gamba na mengine mengi, nilikipenda simu ya kifo kwa mzee Jacob, Muuaji Fabian Andrea Mbozia + Agness (FAMBO)
 
Musiba aliandika vitabu vingi vinavyohusu Will gamba mplelezi mashuhuri barani africa ambaye alikuwa anateketeza mfumo wa kijasusi wa kuwaua wapigania uhuru enzi hizi -- kati ya hivi unataka kibabu kipi?

Kikomo
Njama
Kikosi cha kisasi
Hujuma.
Mkuu kuna hiki kitabu kinaitwa NI LAZIMA AFE alikiandika nani kama umeshawahi kukisoma?
Humo ndani kuna kundi la kijasusi linaitwa ALIKIONA chini ya kapteni Gilo kama sijakosea ni hadithi ya kusisimua kweli kweli....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom