Che Kalizozele
JF-Expert Member
- Jul 20, 2008
- 777
- 49
Kuna wakati huwa nahisi labda kiswahili kina upungufu wa maneno, ingawa kuna nyakati zingine huwa nagundua ni uchovu wangu tu katika kuifahamu lugha hii adhimu ndo unanisumbua ila kiswahili kuna uwezekano kikawa kimekamilika.
Kwa sasa nina tatizo la kiswahili kutumia vitu katika kueleza aina za rangi. Hii inanipa shida kwa kuhisi inawezekana kiswahili hakina maneno ya kuelezea rangi hizi. Mfano rangi ya zambarau, rangi ya damu ya mzee, rangi ya kijivu. Kama kuna mtu anajua maneno yanayotambulisha rangi hizi, tafadhari naomba unielimishe.