Kiswahili Mtaani

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Wanangu wa FB niliwaambiwa juzi juzi hapa. Kwamba mwaka umeisha, kuna mchizi akaibuka, na kunipa zake zile. Unajua zipi? Kwamba:

...enething kan chenji enetaim!

Big up kwa wana wote waliorekebsha kimtindo, hata kama malengo hayakutimia lakini safari huanza na hatua, kilichobaki kwa sasa, ni kucheki situesheni za kuselebreti kuvuka mwaka na wana.

Hizi ni Bata za msingi kabisa ambazo kimsingi inabidi ziambatane na shukrani pia kwa mtu mzima Saa Godi.

Hivi naeleweka?

Najua kuna watakaoanza kuniletea zile za kidiiiiingi, kwamba kula Bata ni anasa, ...shauri zenu, mtadedi bila hata kutesti, hizi bata ninazoongelea wanangu, sio zile za deile neva misi wakati laifu yenyewe haieleweki.

Wans in a momenti sio mbaya wanangu, kuselebreiti. ..

Lakini kama vipi, mnaweza kunipotezea tu, Zee la Nyeti kitu gani bwana?

Enewei tuendelee na stori, tangu jana mwanangu Mr II a.k.a Sugu yuko tauni, tunaangalia jinsi ya kufanya maangamizi, Diamond Jubilee inageuka kuwa ile ya zamani, yenye nyomi la kutosha, na washkaji wa longtaimu, shoo za maana za rap ya kibongo.

Kama ulikuwa hujafaidi show ya Hip Hop, hebu ibuka tuone....

Mwana anaangusha albam ya 10 kwenye gemu, huku full kubaniwa kudadadeki na washkaji, ukikutana nao kitaani wanakuchekea, kazi yako wanaijua, lakini dizaini....

Lakini mwana kakomaa mpaka leo, laifu mtoni, lakini anakuja bongo kufanya uzinduzi, ..kisha anasepa, anakuja kuwaambia wanawe kwamba muziki bado upo, na bado ana mzuka nao.

...ndo hivyo!

Bongo si mnaijua?

Stori sasa...

Siku hizi mwanenu nimekuwa mtu wa ndefu kichizi, ..ruti zangu? Kama una pumzi fupi bora uachane na huu muziki kudadadeki. Uliza wikiendi nilikuwa wapi? Jeti, Lumo huko unaambiwa kwa wabishi. Kila wakiambiwa wahame, watu wapi, ..wanataka kukomaa, na makazi yao..

Haukamu unihamishe kwa buku salasini? Gavamenti vipi?

Basi nikawa skani na wana tunachonga embe, tunapeleka puani, ..huku stori zinaenda. Unaona bwana?

Ila wanangu waliniboa bwana, kuna mwana kahamia kitaani juzi juzi, dizaini mwana kagradueti last yia, kakamatia ajira samwea.

Umeona?

Sasa wanangu ndo' kama hivyo watu wa kijiwe nini, mwana yuko juu. Unaambiwa wana wanam'maindi kuliko maelezo. Full kumzingua... mara wamkabe.... mara waibuke ghetto kumzingua, dizaini wanahisi wakimzingua zingua sana wanaweza kuwa juu kuliko yeye.

Si unajua tena akili za kijiwe?

Mi bwana si unaninyaka? Nikawachenchia wanangu, ..haukamz?

Laifu mbona sio hivyo, mwana kama huyu ilibidi awe mshkaji ili kama kuna michongo miwili mitatu, anawakamatisha, ..si ndio?

Nika-wachana wana unaambiwa, chana mbaya kisha nikasepa. sasa kama wamenimaindi kivyao...
 
Kiswahili lugha nzuri naipenda, naipenda,
na ngonjera darasani nazo nyimbo,
nitaisema popote X2
Ee Mungu nipe uwezo!!!
Du mwana hapo umeniacha kwenye mataa kinamna..ila ivyo ivyo nimekunyaka kiasi!
 
Tafu sana.ila everisingi iko korekti..babu una wa expeliensi na lugha ya mtaa.haha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom